Mkuu wa Wilaya ya Geita Mwalimu Herman Kapufi asitisha vibali vya waganga wa jadi

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,397
JAMII LEO


Mkuu wa Wilaya ya Geita Mwalimu Herman Kapufi amesitisha vibali vyote vya waganga wa jadi katika wilaya ya Geita mpaka pale waganga hao watakapoomba vibali upya vitakavyokuwa na mchujo kuanzia ngazi ya kijiji mpaka mkoa.

Hatua hiyo imetokana na kukithiri kwa mauaji ya mara kwa mara yanayohusishwa na imani za kishirikina, ambapo matukio ya kuchinjwa walinzi, mauaji ya vikongwe ni matokeo ya waganga wa jadi na wapiga ramli chonganishi.

Baadhi ya wananchi wakiwemo viongozi wa dini na waganga wa jadi wamesema wamefurahishwa na agizo hilo la Mkuu wa Wilaya kwani itasaidia kuwabaini waganga wa jadi bandia hivyo kurudisha heshima na imani ya wataalamu wa tiba asili kama ilivyokuwa zamani.

Matukio ya mauaji yanayoambatana na imani za kishirikina katika wilaya ya Geita yanaendelea kushamiri ambapo waathirika wakuu ni vikongwe na walinzi sambamba na agizo la kusitishwa kwa vibali pia Mkuu wa Wilaya ametoa agizo la kufungwa kwa majumba ya starehe yasiyo na vibali vya kukesha ifikapo saa sita kamili usiku.

Chanzo: ITV
 
Ni mwanzo mzuri sana. Maana wengine hawana maana ramli za ajabu ajabu zinazosababisha mauaji kwa watu wasio na hatia.
 
Back
Top Bottom