Mkuu wa Wilaya ya Bukoba apingana na wananchi wake, aunga mkono kumegwa kuunda mkoa wa Chato

Kiturilo

JF-Expert Member
Sep 27, 2021
405
2,000
Hoja ya ukabila kuhalalisha mkoa wa CHATO haina mashiko.
Tujiulize faida ya kuanzisha mkoa huo kwa Taifa ni nini?
Tusikurupukeee! Tujenge uchumi kwanza hayo ya mikoa na wilaya yatafuata.
Kuanzisha mkoa ni gharama kubwa sana! Mpaka leo tuna mikoa mipya kadhaa iliyoanzishwa kwa JAZBA za kisiasa haijaweza kusimama kikamilifu kuwa mikoa, mfano mingi bado ofisi za wakuu wa mikoa zimejiegesha kwenye majengo ya watu. Nyumba za watumishi SHIDA! Huko hatujakamilisha mnataka kuanzisha mikoa mingine! Ni nani aliturogaaaaa?
Mkoa mpya wa Simiyu umesimama imara kuliko hata Shinyanga kwa sasa.
 

Kabende Msakila

JF-Expert Member
Oct 7, 2020
658
1,000
Wenyewe wanasemaje?

Habari za leo Friends of Bukoba.

Hii hapa ni video ya watetezi wa Mkoa wa Kagera zidi ya hujuma za Mkoa wa Chato.Tunawashukuru wote walioshiriki ikiwa ni pamoja na:

(1) Mh. Bernedetha Mushashu (Mbunge viti maalum)

(2) Mh. Charles Mwijage (Muleba Kaskazini)

(3) Mh. Dr. Oscar Kikoyo (Mbunge Muleba Kusini)

(4) Mh. Jackson Rweikiza (Mbunge Bukoba Vijijini)

Shukrani kwa wote walioshiriki katika kupinga kumegwa kwa Mkoa wa Kagera ili kuunda Mkoa wa Chato. Hawa wenzetu wamepigana sana kutetea maslahi ya Mkoa wa Kagera na hasa zile wilaya zinazobaki zisizohofishwe kiuchumi, kisiasa na utamaduni. Kama mtakavyoona kwenye hiyo video, sasa mambo yote yanakwenda ngazi za juu za serikali kwa majadiriano na maamuzi. Kulingana na mtazamo wangu kuhusu maandishi na hotuba za watetezi mbalimbali, petition ya FOB, na hoja hafifu za wawakilishi wa Wilaya za Biharamulo na Ngara, katika mantiki ya kawaida sioni jinsi mtu anavyoweza kuruhusu kumegwa Mkoa wa Kagera. Itabidi uwe kipofu au kiziwi kufanya hivyo baada ya mambo yaliyoandikwa na kusemwa. Hata Hivyo, katika mfumo wa kerikali kama ya Tanzania ambapo mtu mmjo ana mamlaka kamili ambayo siyo lazima yategemee mawazo ya wengine au kundi (absolute power) lolote linawezekana. Therefore, keep our "fingers crossed".

ANGALIZO

Jambo la kushangaza sana katika hii video ni kuona Mkuu wa Wilaya ya Bukoba (Mr. Moses Machali) akiwa msemaji mkuu na mkeleketwa wa kuunga mkono kumegwa kwa Mkoa wa Kagera na kumaanisha kwamba wale waliotoa hutuba za kupinga mkoa isimegwe ni wakabila. Nimejaribu kuangalia huyu mtu ni nani. Huyu ni mtu mwenye umri wa miaka 40, mzaliwa wa Kigoma na alikuwa Mbunge wa Kasulu. Alikuwa mwana chama wa CHADEMA (2007 - 2010), NCCR-Mageuzi (2010 - 2015), ACT Wazalendo (2015 - 2016) na CCM (2016-).

Hii ni rekodi mbuvu sana kwa mtu mwenye umri wa miaka 40. Mtu mwenye msimamo, busara na imani thabiti katika kitu chochote huwezi kuhama kirahisi namna hiyo. Kwa mantiki hii, huwezi kuwa kiongozi wa kundi au jumuiya yoyote kama mtazamo wako unakinzana ma matakwa au mahitaji ya kundi and jumuiya hiyo. Hii ndiyo maana ameshindwa kujua kwamba kama Mkuu wa Wilaya ya Bukoba ambayo ni moja ya wilaya zinazopinga kumegwa Mkoa wa Kagera kwa vile zitaathalika kiuchumi, hawezi kusimama hadhalani na kutoa hutuba kuunga mkono kudhohofishwa kwa Mkoa mama wa Wilaya yako. This cannot happen in public!

Unaweza kuwa na mtazamo tofauti na vilevile unaweza usiipende sehemu na watu ambao umekabidhiwa kuwaongoza, lakini inabidi ufiche hiyo nia yako kama inakinzana na matakwa ya watu wako. Je, huyu mtu anamtazamo gani kuhusu maendeleo ya Wilaya ya Bukoba na Mkoa wa Kagera kwa masuala mengine zaidi ya Mkoa kumegwa? Is this a person you can trust to defend you and resolve your problems? Ningekuwa Rais wa Tanzania, huyu mtu ningemuondoa kwenye hiyo nafasi siku hiyohiyo kwa vile ameonyesha kwamba hana maslahi ya sehemu na watu anaowaongoza.

Deogratias

Canada

Wengi tunagoma kuwa na mkoa kama huo - huwezi kumtoa mwananchi wa Kakonko pembezoni na kumrudisha pembezoni kupata huduma.

Iwapo haipo kisiasa basi Biharamuo kunatosha kuwa Mkoa
 

Bejamini Netanyahu

JF-Expert Member
Aug 7, 2014
60,210
2,000
Mtu aliyetuaminisha kuwa fragmentation ya nchi kwenye vipande vingi vya kiutawala ndiyo kuleta maendeleo alitupotosha sana.

1. Chombo kinachobeba agenda ya maendeleo ya wanachi ni Halmashauri za Wilaya, Miji, Manispaa na Majiji.
2. Halmashauri hizi ndio zinazosimamia elimu, Afya, Kilimo, Ardhi, Maendelo ya Jamii, Biashara, Utamaduni na michezo, n.k
3. Pesa za maendeleo hupewa halmashauri tajwa hapo juu
4. Mikoa ina kazi nyepesi ya uratibu
5. Ukitaka kuleta maendeleo kwa wananchi unawapa halmashauri nyingi , ili agenda za maendelo zitekelezwe kwa ufanisi zaidi ndani ya eneo dogo la kiutawala
Ni gharama tupu
 

Bejamini Netanyahu

JF-Expert Member
Aug 7, 2014
60,210
2,000
Huwezi kupingana na serikali kwenye mipango yake ya maendeleo, Kwanza ardhi ni mali ya serikali sisi tumepangishwa kwa mkataba inaweza ikabadili matumizi ipendavyo, mipaka yote ni serikali inaamua kulingana na mipango yake kizuri zaidi hakuna mwananchi anayepokonywa ardhi ya serikali aliyokodishiwa kwa ama customary au tenure au registered title (Granted tenure). Waache siasa za maji taka waruhusu kukua kwa miji ilitokea hivyo simiyu, Manyara, Geita nk lakini sasa ukifika miji imekuwa bora na ya kisasa kuliko hata ile ya zamani.

Serikali locuta est, causa finita est

Hakuna jipya ni kuongeza gharama kwa wananchi
 

JF Member

JF-Expert Member
Dec 14, 2014
5,132
2,000
Sumu iliyoanzishwa na JPM kuitoa Chato Biharamulo bado inaendelea! SSH Anapaswa kuwa makini! Kuongeza mkoa wa CHATO ni kuwaongezea Watanzania gharama ambazo hazina sababu na zinaweza kuepukika.
Ghalama gani? Mshahara wa Mkuu wa Mkoa?

Kuna faida nyingi sna kuwasogezea wana nchi huduma za kiserikali. Kwanza ni kuwatoa kwenye ujinga. Maeneo mengi yaliyoko mbali na serikali wananchi wengi ni mbumbumbu kabisa. Yaani hawajua hata kama kuna serikali. Wala hajui dunia inaenda je.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom