Mkuu wa wilaya ya Bariadi nakuunga mkono 100% kwa hili la watendaji wa Tume ya Madini kuwaingilia

Feb 14, 2021
61
125
Nimesoma taarifa za kikao kilichohusisha viongozi wa serikali ya mkoa wa simiyu na wizara ya madini chini ya kaim Afisa madini wa mkoa Ndg. Kumbulu.

KWANINI NAUNGANA NA MKUU WA WILAYA MH. KISWAGA

Mtu yeyote afatilie leseni zote za madini katika nchi hii, na wavumbuzi wa madini katika leseni hizo. Lakini pia fuatilia kujua iwapo mtu anapopewa leseni ya utafiti kama anafanya huo utafiti au uchimbaji wenyewe kama siyo kutegesha.

Baadhi ya maafisa madini katikaTume ya Madini, kwa kushirikiana na viongozi baadhi vigogo wizara ya madini wengi wamekuwa wakichukua reseni baada yawachimbaji kugundua madini. Maana haiingii hakilini kama mtu ulichukua leseni kwanini usifanye kazi wakati huo?

Maeneo mengi mazuri yenye madini ambayo tume na wizara inayajua , imewapa jamaa zao leseni bila kuzifanyia kazi, halafu mwananchi mnyonge akigundua wao ndo wanawahi kuchukua %

Kwahili DCK iswaga lala nao maafisa madini hao, wala wasikutishe kukushtaki wewe, hizo mbinu chafu zinafanyika maeneo mengi katika nchi hii.

Hata buyo afisa madini hajakurupuka kukutishia kushtakiwa, huyo ananguvu yakigogo mnufaika nyuma yake.

Komaa nao mkuu ili mbivu mbichi zijulikane, kuna mtu mkubwa kwenye hilo dili ambaye yupo wizarani, maana imefika sehemu wachimbaji wamekuwa manamba wa viongozi wa hii wizara.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom