Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo wajua jinsi wafanyakazi wasio kuwa na mikataba wanavyopoteza haki zao?

B

Binti Msichana

Member
96
250
Katika hali ya kusikitisha katika wilaya yako wafanyakazi wengi wamekuwa wanafanya kazi bila ya mikataba ya ajira hivyo kujikuta wanapoteza haki zao za msingi.

Baadhi yao wamefanya kazi muda mrefu mwisho wa siku wakiumia kazini, au kuacha na kufukuzwa kazi wanakosa hata mafao yao kwani hawachangii hata katika mifuko ya hifadhi ya jamii.

Hali hii imeshamiri sana katika sekta binafsi na shule mbalimbali zilizo chini ya Mkurugenzi wa Bagamoyo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Bagamoyo amejiweka pembeni katika kuajiri watumishi wasio walimu katika shule hizi, matokeo yake wakuu wa shule wamepewa jukumu la kuajiri wafanyakazi hawa hasa walinzi na wapishi.

Kinachosikitisha wafanyakazi hawa wakati mwingine wakuu wa shule wanashindwa hata kuwalipa mishahara yao na stahiki nyingine kama likizo.

Shule ya Dunda kuna huyu mpishi anaitwa Bibi Shange, amefanya kazi hapo shuleni kwa zaidi ya miaka kumi lakini kwa nyakati tofauti hakulipwa mishahara yake, na hakuwa na mkataba wa ajira.Alipojaribu kudai mishahara yake kwa mkuu wa shule aliambulia maneno machafu na kufukuzwa kazi bila ya kulipwa hata senti tano ukizingatia wakati huo alikuwa anauguza mtoto mchanga, na hakuwa na pesa ya matibabu ya mwanae.

Haki ya bibi huyu aliyefanya kazi miaka kumi imepotea, licha ya nguvu zake alizotumia kwa muda mrefu akiwahudumia walimu na wanafunzi.

Siwezi kusema shule haikuwa na pesa, pesa zilikuwepo kwani kwa nyakati tofauti wanafunzi wanachangishwa pesa , mfano wanafunzi walichangishwa shilingi 1000 kila mmoja kwa ajiri ya walimu wa masomo ya sayansi mwaka Jana, isitoshe kuna wanafunzi wa boarding wa kidato cha nne nao walichangishwa shilingi 5000 kila mmoja kwa ajili ya kununua taa moja ya energy server , hivyo pesa ilikuwepo.Nakumbuka walikuwa wanafunzi waliomaliza 2016.

Vilevile kuna mlinzi mmoja anaitwa mzee Shirima naye amefanya kazi kwa muda mrefu bila ya mkataba , huku akikosa kulipwa baadhi ya mishahara.Huyu mzee naye kafanya kazi zaidi ya miaka 10, matokeo yake akaamua kuacha kazi bila hata ya kupewa haki yake.

Cha kushangaza bado kuna walinzi wengine wanafanya kazi bila ya mikataba ya ajira, walinzi hawa wamekosa molari ya kazi mpaka kazi zao za ulinzi zinafanywa na walimu wanaopiga doria usiku na mchana bila ya malipo ya ziada.

Wito wangu jukumu la ajira la watumishi wasio walimu katika mashule wasiachiwe wakuu wa shule, jukumu hili ni la Mkurugenzi.

Hivyo Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo nakuomba usimamie suala hili la kuhakikisha katika Wilaya yako hakuna mtu anayefanya kazi bila ya mikataba ya ajira iwe sekta binafsi au serikalini.

Naunga mkono kauli ya Waziri Mkuu ya kuagiza wakurugenzi wote nchini kuwapa mikataba ya ajira watumishi wasio walimu katika halmashauri.
 
Lambardi

Lambardi

JF-Expert Member
10,587
2,000
Nenda kwa DC itisha camera ndio wata fanya haraka sana!! Bila media hawa fanyi kitu Kiki tuuuu ndio mwendo wa sasa

Forum statistics

Threads
1,424,602

Messages
35,068,211

Members
538,026
Top Bottom