Donatila
JF-Expert Member
- Oct 23, 2014
- 7,563
- 21,665
Mkuu wa wilaya ya Arusha Fadhili Nkurlu amesimamisha shughuli za uchimbaji katika machimbo ya moramu katika kata ya Moshono Mkoani Arusha kwa kipindi cha mwezi mmoja kupisha wakandarasi kuweka sawa machimbo hayo ambayo yanachimbwa bila kufuata utaalamu hali ambayo inadaiwa inaweza kuhatarisha uhai wa maisha yao.
Katika kipindi cha mwaka 2013 machimbo hayo yaliuwa wachimbaji 13 hali ambayo ilimfanya waziri mkuu mstaafu Peter Pinda kuyafunga mpaka yatakaporekebishwa ndiyo wachimbaji hao waendelee na uchimbaji ingawa inadaiwa wachimbaji hao hawakufuata maagizo mpaka hivi sasa kwani waliendelea na shughuli za uchimbaji.
Akizungumza wakati akifunga machimbo hayo mkuu wa wilaya ya Arusha Fadhil Nkurlu alisema kuwa mazingira ya wachimbaji hao ni mabaya na yanahatarisha maisha yao kwa kiasi kikubwa na kwamba hawana utaalamu wa kutosha juu ya namna bora ya uchimbaji wa moramu hiyo mbali na kuchimba kinyemela toka kauli ya waziri mkuu kutamkwa.
Alisema kuwa ameamua kufunga machimbo hayo kutokana na oanagezeko kubwa la vifo linalosabibishwa na uchimbaji wa moramu usiozingatia sheria na kanuni .
Naye kamishina msaidizi wa madini kanda ya kaskazini Elias Kadabila alichukuwa fursa hiyo kuwaomba wananchi kufuata maelezo ya mkuu wa wilaya ili waweze kuchimba kuchimba kwa usala ambapo alisema kuwa pia iatawasaidia kuepukana na maafa au vifo vinavyotokana na uchimbaji holela.
Aidha pia aliuomba uongozi wa mtaa pamoja na wachimbaji hao kutoa ushirikiano ili kuweza kuwapisha wakandarasi kutengeneza machimbo hayo kwa muda wa mwezi mmoja .
Gazeti hili pia liliweza kuzungumza na baadhi ya wachimbaji hao ambapo walisema kuwa hawakubaliani na agizo hilo la mkuu huyo kwakuwa uchimbaji huo ndiyo ambao unawafanya kumudu gharama za maisha na kusomesha watoto na kwamba serikali iangalie namna nyingine.
"kwakweli tunaomba serekali iangalie tena na tena swala hili kwani sisi wananachi ndio tunategemea maachimbo haya kwani ndio yanatusaidia tunaweza kula ,kusomesha watoto ,kujenga naweza sema kiujumla kuendesha maisha yetu"Alisema Lowayani Metili
Ipo haja ya wachimbaji hao kupisha marekebisho hayo yatakayofanywa na serikali kwa manufaa yao na uhai wao kwani kuendelea kuchimba wakati wanahatarisha maisha yao ni jambo la hatari Zaidi kwani wahenga wanamsemo usemao UHAI NI BORA KULIKO KIFO.