Mkuu wa wilaya ya Arumeru na mapinduzi ya kilimo Arumeru

yamindinda

JF-Expert Member
Jul 29, 2011
1,581
1,318
MKUU wa Wilaya ya Arumeru Mhe. Jerry Cornel Muro ameweka DHAMIRA yake ya kimkakati ya kubadilisha sekta ya KILIMO kutoka kilimo cha kutegea MSIMU na badala yake sasa Wilaya ya Arumeru itakuwa na kilimo cha moja kwa moja ambacho amekipa jina la OTESHA KISHA VUNA HALAFU OTESHA TENA. Mhe. Jerry Cornel Muro, katika kuhakikisha mkakati huo unafanikiwa na unakiwa endelevu ameamua kuhusisha Wadau mbalimbali wa sekta ya kilimo kuanzia Wakulima , Taasisi na Wizara za Serikali zinazohusiana na Kilimo, Mbegu, Masoko pamoja na Taasisi za Fedha, ambazo zitakuwa na wajibu wa kubadilisha mtazamo wa Kilimo cha Arumeru.

Kwa kuanzia, Mhe. Jerry Cornel Muro ameamua kuzishirikisha Taasisi za kitafiti za kilimo ambazo zitalazimika kufanya utafiti wa kina katika kufikia Azma hiyo, ikiwemo kushauri namna bora ya kutekeleza mkakati huo katika ngazi ya wilaya, ambapo amefanya ziara katika Taasisi ya Utafiti ya Mazao ya Kilimo Africa (IITA) Iliopo jijini Dar es salaam, na kukubaliana kuanzisha ushirikianona taasisi hiyo yenye ofisi zake Wilaya ya Arumeru.

Akizungumza mara baada ya kutembelea maabara mbalimbali na kuzungumza na watumishi wa Taasisi hiyo Mhe. Jerry Cornel Muro amesema dhumuni la kutembelea taasisi hiyo ni ili kujifunza na kujionea jinsi kazi zinavyofanywa katika Taasisi hiyo ya Kilimo.

......”Leo nimejionea kazi inayofanywa hapa makao makuu lakini pia nimekuja kuweka mshikamano nakuongeza ushirikiano ambao unalenga pia kuwanufaisha wananchi wetu ambao ndio walengwa wakuu”...... alisema Mhe. Jerry Cornel Muro.

Aidha, Mhe. Jerry Cornel Muro amemshukuru Rais Wa Jamhuri ya Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, kwa kuanzisha kituo hicho kwaajili ya utafiti na maswala yote yanayohusu kilimo.

..........”Nianze sana kwa kumshukuru Mhe. Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, lakini nimshukuru mtangulizi wake Rais Kikwete kwakuliona hili nakuona kuna uhitaji wa sisi Tanzania kuwa na senta hii kwa ajili ya utafiti na maswala yote yanayohusiana na kilimo"........... alisema Mhe. Jerry Cornel Muro.

Hata hivyo Mhe. Jerry Cornel Muro alisema kuwapo kwa taasisi hiyo kutasaidia kutoa fursa kwa wakulima nakuweza kupata elimu na mambo mbalimbali yanayohusuana na tafiti na ugunduzi katika sekta hiyo ya Kilimo.

.........”Ujenzi wa Kituo hiki katika Nchi yetu ya Tanzania imetupa fursa sisi Kama watendaji wa Serikali kuweza kunufaika moja kwa moja na uwepo wa Taasisi hii Tanzania, Kwa mkoani Arusha ipo katika wilaya yetu ya Arumeru imesaidia pia kutoa fursa kwa wakulima wetu kuweza kupata kipaumbele katika Mambo mbalimbali yanayohusiana na tafiti na ugunduzi wa maswala mbalimbali katika sekta ya kilimo”.......... alieleza Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe. Jerry Cornel Muro.

Awali akimkaribisha Mhe. Jerry Cornel Muro katika ofisi za Mkuu wa Taasisi hiyo inayohudumia nchi za ukanda wa Africa Mashariki Dkt. Victor Mayong mbali na kuipongeza serikali ya awamu ya tano katika kutengeneza mazingira bora yanayovutia uwekezajo kwenye Kilimo amesema wao wataendelea kushirikiana na serikali pamoja na nchi za Africa Mashariki katika kupambana na changamoto zenye viashiria vya kupunguza uzalisha wa chakula yakiwemo magonjwa kwenye mimea, na kusisitiza lengo la taasisi yao ni kubadili mfumo wa kilimo cha Africa na kuongeza uzalishaji wa mazao

Imetolewa Na:-
Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Arumeru,
Jumatano Machi 27, 2019.

1553755469294.png


1553755512731.png


1553755537630.png


1553755572541.png
 
Hiyo ni sarakasi tu, 50% ya ardhi ya Meru ni maji na hakuna kitu serikali imewafundisha wananchi kuyatumia angalau hata kunyeshea vumbi, wewe mwenyewe nje ya ofisi yako pana mfereji wa maji lakini hakuna hata mche wa ua..vumbi hadi kwenye viti...sikuelewi ujue...ama unatafuta kujulikana kwamba nawe upo.
 
Asisahau na viwanda vya kuongeza thamani ya mazao ya hao wakulima.

Loyalty To country Always,To government When it deserves
 
Back
Top Bottom