Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,622
- 8,410
Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Arusha (APC), kimepanga kumfikisha kwenye vyombo vya sheria Mkuu wa Wilaya Arumeru, Alexander Mnyeti, kwa kutoa amri ya kumuweka mahabusu mwandishi wa Kituo cha Televisheni cha ITV, Khalfan Lihundi.
Mnyeti aliingia kwenye mgogoro na waandishi wa habari Mkoani humo mwishoni mwa mwaka jana, baada ya kuwaamuru Polisi kumuweka ndani mwandishi huyo kwa kudai kuwa amekuwa akiandika habari za uchochezi.
Akizungumza katika maadhimisho ya uhuru wa Vyombo vya habari duniani, Mwenyekiti wa APC, Claud Gwandu, alisema kwa kuwa imepita miezi mitatu bila Mnyeti kuomba radhi, wameamua kuchukua hatua za kisheria.
"Tulimpa miezi mitatu aombe radhi ili tuendelee kufanya kazi zake kwasababu alitukosea, lakini nasikitika kuwatangazia kuwa mpaka sasa amekataa kuomba radhi, kuna baadhi ya taasisi zimetoa wanasheria wao ili kuhakikisha huyu bwana mkubwa mwenye kiburi anachukuliwa hatua anazostahili”, alisema.
Chanzo: Kwanza Tv