Display Name
JF-Expert Member
- Feb 11, 2014
- 423
- 451
Baada ya jana kukutana na kuzungumza na Watumishi wa Halimashauri ya Wilaya ya Songwe jana.
Leo Juni 25,2021 Mkuu wa Wilaya ya Songwe Simon Simalenga amefanya ziara kwenye Kata ya Mwambani ambayo inaundwa na Vijiji vya Iseche, Mbala na Mwambani.
Katika ziara hiyo ambayo aliambatana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Songwe ililenga kwanza kujitambulisha kwa Wananchi ikiwa ni mara ya kwanza kwa kiongozi wa Serikali kufika katika eneo hilo na pili ililenga kukagua maandalizi na kuwahamasisha Vijana kushiriki kwenye mafunzo ya Jeshi la Akiba kwa mwaka 2020/2021
Katika mafunzo ya Mwaka huu Wilaya ya Songwe inatarajia kufanya mafunzo kwa vijana zaidi ya 700 chini ya Wakufunzi kutoka JWT chini ya Meja Joel F. Cibaya
Wilaya hii ina jumla ya Tarafa 2 zenye Kata 18 na Vijiji 43