Mkuu wa wilaya na chuo kikuu binafsi. TCU mko wapi?

MIGNON

JF-Expert Member
Nov 23, 2009
4,083
5,064
Kwa karibu mwezi mzima wanafunzi wanaosoma Chuo Kikuu cha ERKENFORDE Tanga walisimamishwa masomo na baada ya majadiliano yakihusisha wanafunzi,TCU na uongozi wa chuo wanafunzi wameamriwa kuandika barua yakuomba msamaha.Cha ajabu ni kuwa wanafunzi wana ji commit kwenye ofisi ya mkuu wa wilaya kuwa hawatashiriki tena mgomo.
Mkuu wa wilaya anahusika vipi katika utawala wa CHUO kikuu binafsi?Je waliharibu mali yoyote kiasi ambacho kamati ya Usalama ya Wilaya inashawishika kuingia?
Kwa TCU kama regulatory authority kwa nini isiwe inamaliza mambo haya yenyewe bila kuingiza ngazi nyingine?
Naomba kuwasilisha mliopo Tanga mtujuze zaidi.
 
Inavyoelekea Tanga hakuna wa JF.Kama wapo nahisi wantembelea mahusiano na naniii
 
Hizo ni ishu za kimenagement TCU haihusiki nazo tafadhali, management ya chuo ihusike nazo na kama chuo kimeona kumtumia mkuu wa wilaya ni sahihi hiyo ni jukumu lao, mwishowe mtasema TCU iwe inasuluhisha hata ugomvi wa mtu akiachana na girlfriendd wake au boyfriend wake ilimradi tuu wako chuo....
Vyuo vina hati idhini ambazo ndio zinawapa AUTONOMOUS right kuhandle mambo yao kiimtazamo wao.
 
Mkuu wa Wilaya ni mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya. Naona ni ok tu.
 
Kama ndio njia waliyoona inafaa na wanafunzi wameikubalia na chuo kimeridhika na mkuu wa wilaya amekubali, tatizo liko wapi?
 
Cha ajabu ni kuwa wanafunzi wana ji commit kwenye ofisi ya mkuu wa wilaya kuwa hawatashiriki tena mgomo.
Mkuu wa wilaya anahusika vipi katika utawala wa CHUO kikuu binafsi?
Kwa katiba yetu mbovu mkuu wa wilaya ndo mwenyekiti wa ishu zote za usalama za wilaya....
 
Mkuu wa wilaya ana jukumu la kuhakikisha kuna amani na utulivu katika jamii aliyopo, hivyo kwa kuwa vitendo vyo migomo na maandamano mara nyingine huambatana na uvunjifu wa amani anawajibika kuhakikisha wahusika wanajifunga kutoshiriki katika vitendo hivyo mbele yake ili watakaporudi chuoni amani na utulivu viwepo haijalishi ni chuo cha binafsi au serikali.
 
Kwa karibu mwezi mzima wanafunzi wanaosoma Chuo Kikuu cha ERKENFORDE Tanga walisimamishwa masomo na baada ya majadiliano yakihusisha wanafunzi,TCU na uongozi wa chuo wanafunzi wameamriwa kuandika barua yakuomba msamaha.Cha ajabu ni kuwa wanafunzi wana ji commit kwenye ofisi ya mkuu wa wilaya kuwa hawatashiriki tena mgomo.
Mkuu wa wilaya anahusika vipi katika utawala wa CHUO kikuu binafsi?Je waliharibu mali yoyote kiasi ambacho kamati ya Usalama ya Wilaya inashawishika kuingia?
Kwa TCU kama regulatory authority kwa nini isiwe inamaliza mambo haya yenyewe bila kuingiza ngazi nyingine?
Naomba kuwasilisha mliopo Tanga mtujuze zaidi.

Nilisema kuwa vyuo vingine sio vyuo. Why dont they abandon this stupid so called university!

Hii ni shule ya sekondari, njoo muone you will never believe your eyes! Watoto msome mweze kwenda vyuo vyenye sifa za kweli. Huyu ame- fluke akapata usajiri- hopeless
 
Back
Top Bottom