Kifaru86
JF-Expert Member
- Apr 22, 2017
- 1,734
- 3,802
Mwanaume ukiwa na pesa kuna mambo mengi yanajificha nyuma ya paziaaa
Wanawake sio watu wa kuwaamini
Sent using Jamii Forums mobile app
Wanawake sio watu wa kuwaamini
Mkuu wa wilaya mstafu nchini, Peter Toima anadaiwa kusalimisha silaha yake mbele ya jeshi la polisi mkoani Arusha baada ya kudaiwa kumtishia mkewe wa ndoa Mara kadhaa, Philomena Toima.
Hatua ya kiongozi Huyo mstaafu kusalimisha silaha yake inakuja kufuatia kumpiga Mara kwa Mara mkewe na kisha kumtishia kwa silaha hiyo jambo lililopelekea mwanamke huyo kuwasilisha malalamiko mbele ya jeshi hilo.
Mnamo mwaka Jana mke wa kiongozi huyo (Philomena) alifungua jalada la shambulio lenye kumbukumbu nambari KML/RB/137/2019 katika kituo cha polisi cha Komolo wilayani Simanjiro akilalamika kushambuliwa sehemu mbalimbali mwilini mwake.
Katika tukio hilo Philomena alimlalamikia mmewe kutokuwa mwaminifu kwenye ndoa yake baada ya kudaiwa kuchepuka na mwanamke aliyetambulika kwa majina ya Scolla Mollel.
Philomena alidai kwamba matatizo hayo yalianza pale mme wake alipomwajiri mwanamke huyo ambaye kwa sasa amezaa naye mtoto mmoja katika taasisi waliyoianzisha ya ECLAT Foundation kama mtunza fedha.
Taarifa za uhakika zinadai kwamba Toima alikabidhi silaha yake hivi karibuni mbele ya jeshi la polisi mkoani Arusha na kutakiwa kuripoti Mara kwa Mara.
Hatahivyo,taarifa hizo zimeeleza kwamba polisi wanaendelea kuchunguza jalada lililofunguliwa mbele ya jeshi hilo na endapo wakikamilisha watamfikisha kiongozi Huyo mstaafu mahakamani.
Pichani chini ni mkuu wa wilaya mstaafu nchini Peter Toima akiwa na mkewe .
Picha nyingine ni mwanamke anayedaiwa kuwa na mahusiano naye na kupelekea kuvuruga ndoa ya wawili hao,Scolla
Mollel.View attachment 1421409View attachment 1421410View attachment 1421411
Sent using Jamii Forums mobile app
Sent using Jamii Forums mobile app