Mkuu wa Wilaya Monduli, Frank Mwaisumbe aliyepopolewa Mawe na wananchi afunguka, ampiga chini Mwenyekiti wa kijiji

Dc asijitetee, WENDA hao Wana kero zao sugu ,ambazo hazijapatiwa majibu, kwa tz ukiona mwananchi,au wananchi wafanya hivi, jua Kuna Jambo,tatizo la viongozi ni kukimbilia kujikosha

Acheni Mambo mepesi ,Sasa Kama Kuna tatizo na unamsimamisha MWENYEKITI si ndo unazidisha chuki KWA wenyenchi, ?

Ilikua ni kumuita MWENYEKITI na kujua tatizo na jinsi ya kulitatua Basi ,hivi tz busara KWA viongozi alikufanazo Nyerere?
Nyerere ndio alikuwa na busara??

Mijitu mko brainwashed sana. Huyo Nyerere aliwahi kumuita mpigania uhuru mwenzie (kiongozi) Malaya
 
Mkuu wa wilaya ya Monduli Mkoa wa Arusha ,Frank Mwaisumbe amemsimamisha kazi mwenyekiti wa Kijiji cha Engaroji ,Ngarama Mapema Kwa tuhuma mbalimbali ikiwemo kuhamasisha wananchi kushambulia Kwa mawe msafara wake na kuvunja vioo vya magari likiwemo gari lake la ofisini.

Akitoa ufafanuzi Mbele ya waandishi wa habari ofisini kwake , Mwaisumbe alisema kuwa Septembe 24 mwaka huu akiwa na kamati ya ulinzi na usalama wilayani humo wakienda katika kijiji hicho Kwa lengo la kubaini tuhuma mbalimbali za ubadhilifu wa fedha zinazomkabili mwenyekiti huyo.

Mbali na hayo walifuatilia utekelezaji wa agizo la waziri wa Ardhi ,Nyumba na maendeleo ya Makazi, William Lukuvi ,ambaye aliwaagiz wataalamu wa Ardhi wilayani humo kusaili watu wote waomiliki Ardhi katika kijiji hicho.

Alisema akiwa anahutubia wananchi hao katika mkutano wa hadhara kijijini hapo,,ghafla wananchi walianza kumshambulia kwa mawe ambaye hata hivyo alifanikiwa kukimbia,ndipo walipohamishia hasira zao kwa kupopoa Kwa mawe magari kadhaa ya msafara huo na kuvunja vioo vya magari hayo likiwemo la kwake.

Kadhalika wananchi hao walifanya uharibifu wa kukatakata mabomba ya maji na kutoboa mateki katika eneo la mfanyabiashara wa Madini ambaye ni mwanakijiji mwenzao Paulo Narida ambaye alidai wanamgogoro naye wa muda mrefu wakimtuhumu kujimilikisha eneo la Kijiji lenye ukubwa wa ekari 700 kinyume na utaratibu.

"Nikiwa nahutubia wananchi hao walitaka ufafanuzi kuhusu mgogoro wa Ardhi na Mkazi mwenzako Paulo Narida wanayemtuhumu kijimegea ardhi yao yenye ukubwa wa ekari 700 ,niliwajibu kuwa siwezi kuongelea jambo lililopo mahakamani ndipo walipopandwa na jazba wakidhani namtetea na kuanza kunishambulia Kwa mawe"alisema.

Mkuu huyo wa wilaya alidai kuwa katika tukio hilo hakuna aliyejeruhiwa ila baadaye ofisi yake ilifanya uchunguzi na kubaini kwamba mwenyekiti huyo wa Kijiji , Ngarama Mapema Kwa kushirikiana na mfanyabiashara Paulo Narida ndio wanaoandaa na kuwachochea wananchi waweze kuwazomea viongozi wanaofika kijijini hapo Kwa maslahi yao.

Alisema mbali ya yeye kupopolewa Kwa mawe pia waziri Lukuvi,Mkuu wa wilaya aliyepita waliwahi kukumbwa na kadhia ya kupokelewa Kwa mabango na baadaye kuzomewa mpango aliodai unaratibiwa na Mwenyekiti huyo Kwa kushirikiana na mfanyabiashara huyo ambaye pia gari lake lilipasuliwa vioo siku ya tukio.

Mwaisumbe ameiagiza taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa Takukuru,wilayani humo pamoja na mkuu wa polisi wa wilaya kuchunguza tuhuma zinazomkabili mwenyekiti huyo na kuchukua hatua.

Mkuu huyo alidai kuwa mwenyekiti huyo anatuhumiwa Kwa makosa mbalimbali yapatayo sita kati ya Saba yaliyokuwa yanamkabili ikiwa ni pamoja na ubadhilifu wa shilingi milioni 150 fedha zilizotolewa na mfadhili kwa ajili ya ujenzi wa Nyumba ya walimu .

Pia kutoitisha mkutano wa kusoma mapato na matumizi katika kipindi Cha miaka mitatu, kutoitisha mkutano mkuu Kwa ajili ya kutoa maamuzi mbalimbali ikiwemo ya ardhi,kugawa Ardhi kinyume na utaratibu,kuchangisha michango Kwa wananchi Bila kuwa na kibali Cha mkuu wa wilaya ,kunyang'anya mifugo na kuiuza Bila kufuata utaratibu .

Akizungumza kwa njia ya Simu mwenyekiti huyo alisema kuwa hatambui taarifa za kusimamishwa uongozi na mkuu wa wilaya alidai kuwa yeye bado ni kiongozi wa wananchi na anaendelea na majukumu yake kama kawaida.

Katika Hali isiyokuwa ya kawaida wananchi hao baada ya kutenda kosa la kushambulia viongozi wa kamati ya ulinzi na usalama wa wilaya na kuvunja vioo vya magari walijikusanya na kuandamana Makao makuu ya ccm mkoa wa Arusha ambapo walipokelewa na Katibu mkuu Musa Matoroka ambaye Hata hivyo aligoma kuongelea mazungumzo yake na wananchi hao.

Kamanda wa polisi Mkoa wa Arusha Justine Masejo alisema jeshi Hilo limewahoji watu kadhaa na linaendelea kufanya uchunguzi juu ya tukio hilo.

View attachment 1957236View attachment 1957238
Hapo ndipo unapoona umuhimu wa Raisi kuzunguka kutatua migogoro ya wananchi

Ukweli ni kwamba huwezi kutegemea wateule wako kwa 100%, na pia Raisi kwa mamlaka makubwa aliyonayo, anampa uwezo mkubwa wa kutatua matatizo kuliko RC, DC au Mbunge

Anayeumia na nchi ni Rais kwa 100%
 
Back
Top Bottom