Mkuu wa Wilaya Monduli aupotosha uma kuficha madhambi yake

kingaimtoto

New Member
Sep 30, 2021
2
1

Mgogoro wa Ardhi kati ya matajiri na uma wa Eng'arooji ulianza mwaka 2016 kutokana na watu wachache matajiri kujitwalia Ardhi ya uma kinyume na sheria.

Baadae kutokana na mgogoro huo, watu hao walitengeneza tuhuma dhidi ya Mwenyekiti wa kijiji kutaka kumdhoofisha katika kuipigania Ardhi hiyo ya uma.

Kutokana na tuhuma hizo mapema 2018 vyombo vya Uchunguzi vilitumwa kwenda kuchunguza tuhuma hizo na zilionekana hazina Ushahidi. Ni tuhuma tu za kumfifisha katika kupigania Ardhi ya wananchi wake.

Kuhusu Waziri wa Ardhi Lukuvi, alifika Eng'arooji na kufuta hati za watu hao kwani zilionekana kwamba hazikufuata utaratibu. Lukuvi hakuwahi kuzomewa au kunyimwa ushirikiano kama ambavyo Mkuu wa Wilaya anapotosha uma.

Kuhusu fedha za mfadhili, mfadhili yule alikua akilipia vifaa vya ujenzi pale Bulk na Serikali ya Kijiji kwenda kuchukua vifaa vya ujenzi. Hakuna fedha zilizowahi kupokelewa na Mwkt kama ambavyo Mkuu wa Wilaya anapotosha uma. Jengo lipo na ujenzi wake umesimamiwa na wataalam wa Halmashauri. Pia Ofisi ya ukaguzi wa ndani walishaenda na hawakukuta kitu.

Kuhusu michango, ni uongo mtupu. Mwenyekiti hakuwahi kuchangisha mchango wowote tofauti na zile shilingi 10000 ambazo ni za Wilaya nzima na zinapelekwa kwenye akaunti ya Halmashauri.

Ni kweli mara kadhaa kutokana na Mgogoro huo, aliekua Mkuu wa Mkoa wa Arusha aliagiza Mwkt akamatwe na kufunguliwa mashtaka ili kumfifisha katika kudai Ardhi hiyo ya wananchi lakini hujuma zake hazikufanikiwa.

Baada ya kutofanikiwa, siku waziri amekuja kuhitimisha utatuzi wa mgogoro huo alimuacha pale Nanja Sekondary na kwenda kutaka kumvua Mwkt madaraka na hilo nalo halikufanikiwa kwani baada ya wananchi kugundua njama zake ovu walitawanyika na hivyo hakumkuta mtu kwenye Mkutano uliokua unamsubiri Waziri Lukuvi.

Baada ya Mkuu wa Mkoa kukosa namna hiyo ovu ya kumvua Mwenyekiti alienda kuandika barua hiyo inayosemwa na Mkuu wa Wilaya. Barua hiyo iliandikwa kuhusu Serikali ya wakati huo.

Ikumbukwe kwamba hii ni Serikali mpya baada ya uchaguzi wa serikali za mitaa kufanyika mwaka 2019.

Kuhusu Mkuu wa Wilaya kurushiwa mawe, Mwenyekiti wa kijiji hahusiki kwani baada ya Mkuu wa Wilaya kuamuru akamatwe alikua mikononi mwa OCD na OCD alimuachia baada ya vurugu kuzuka. Tuhuma za Mkuu wa Wilaya dhidi yake ni za uongo na za kubumba.

Wananchi wa Eng'arooji wanajiuliza kwamba namna pekee hii Ofisi ya Mkuu wa Wilaya inaona kumaliza mgogoro wa Ardhi ni kumvua Mwenyekiti madaraka ambayo ndiyo matakwa na maelekezo ya Matajiri waliopora Ardhi??

Kuna maswali ya kujiuliza na Mkuu wa Wilaya alipaswa kujiuliza kabla ya kujiingiza kwenye mambo ambayo yanamfanya aonekane amehongwa kuwahujumu wananchi walio wengi

1.Kama hizi tuhuma za toka mwaka 2018 Zina ukweli kwanini vyombo vya Uchunguzi havikupeleka ukweli huo na Mwkt na Wenzake kupelekwa mahakamani??

2. Kama wananchi wana shida na Mwenyekiti kwanini 2019 walimchagua tena kwa kura zote bila hata moja kudondoka?

3. Kama wezi hawa wa Ardhi walikua na uhalali kwanini Waziri alifuta hati zao??

4. Je yeye pekee ndiyo mkuu wa Wilaya amekuwepo Monduli toka tuhuma hizi zitoke??

5. Je huyu Mwenyekiti wa hatokani na Chama Cha Mapinduzi na kama kulikua na ukweli wa madai hayo mbona kimempitisha tena kwa kishindo???

Kama Mkuu wa Wilaya anauhakika na madai haya iundwe tume huru ya kuchunguza jambo hili kwani tayari ana chuki na Mwenyekiti wa Kijiji Eng'arooji.

Ni Mimi mwananchi wa Monduli




no_photo.png
ReplyForward







 
Tulijua tu haya na ndiyo maana DC alikua anatoa povu ....Ametumia nguvu kubwa sana kujitetea. Rushwa ni mwana haramu
 
DC WANGU MONDULI AMEPOTOSHWA

Nawasalimu kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania!!!

Kwanza napenda kusema sikusudii wala sipendi kujibishana na mkuu wangu wa wilaya Kwenye vyombo vya habari.

Lakini nimelazimika kusema kidogo ili kuondoa upotoshwaji mwingi aliosema DC Kwenye taarifa yake kwa vyombo vya habari jana.

Kitu ambacho nimeshangaa na kujiuliza mimi ni nani mpaka DC akanituhumu tena Kwenye vyombo vya habari na bila kunipa nafasi ili na mimi nihojiwe.

Cha ajabu vyombo vyote vya habari wanatishwa wasitoe taarifa ya upande wetu.

Na mimi nimeamua kutumia kalamu yangu kujibu baadhi ya hoja alizozitoa kwa kisingizio eti waliomtangulia walikosa muda wa kushugulikia.

Naomba kusema tuhuma hizi sio mpya zimetengenezwa tangu 2017/18 ili kuzima mgogoro wa ardhi uliopo kati ya wenye fedha waliopora ardhi ya kijiji na wananchi.

Kwa bahati mbaya sana ofisi ya DC kwa muda wote umekuwa upande wa waporaji na sisi wananchi kukosa msaada kila walipofika katika ofisi hizo.

Nimekuwa mhanga kwa jambo hili nimetengezewa kesi nyingi nimepelekwa mahakamani nilinyimwa dhamana nilikaa magereza mara kadhaa na kutengenezewa kesi ili tu ninyamaze Lakini kwa kuwa nilipewa dhamana na wananchi wenzangu nimekataa dhuluma hizi na nipo tayari kuteswa kufungwa tena kupewa kesi tena au kufukuzwa Lakini sintauza haki za wana Eng'arooji leo wala kesho.

Jambo lingine katika hili ambalo DC hajui ni kwamba tuhuma hizi nimeshachunguzwa mara tatu na takukuru na sijakutwa na hatia.

Hata ofisi ya ukaguzi wa ndani walishanihoji mara nyingi na hawakuona Cha maana kinacholalamikiwa namshauri DC achukue taarifa hizo katika ofisi hizo wala asipoteze muda mwingi.*

Mikono yangu ni misafi naamini taarifa zipo mh DC angezisoma.

Labda niseme kwa ufupi hoja hizi za kutengeneza ili kunivunja moyo japo zinaniimarisha.

1.kwamba tawi langu la ccm limenilalamikia
Kwanza dc sio msemaji wa ccm malalamiko yaliopelekwa ccm yatashugulikiwa na uongozi wa ccm na sijawahi kuulizwa na chama nashangaa dc anataka pia kuwa katibu wa ccm na msemaji wa ccm.
Hata hivyo atambue tawi la engarooji limenipendekeza kugombea uwenyekiti wa kijiji 2019 na niliteuliwa na nikashinda kwa zaidi ya asilimia tisini Kwenye kura za maoni.

Siamini chama ingemwamini mbadhirifu
Kwa hili nawaachia chama waseme zaidi .

2.Hoja ya kunisimamisha madaraka kwa mujibu wa sheria wenye mamlaka wa kuniondoa ni wale walionipa ridhaa au chama changu kilichonichidhamini
Nashauri dc mambo mawili anipeleke, mbele ya umma wa engarooji akawahoji kwa mujibu wa sheria wakapige kura ya kuniondoa.

Namwomba asinionee kwa kuwa ana mamlaka na nguvu ya dola atumie njia ya haki kuniondoa
Aniandikie tuhuma zangu nizijibu na mwisho aje mbele ya mkutano bila mitutu ya bunduki
Au ikimpendeza anipeleke katika chombo cha haki ambayo ni mahakama nikajitetee asitumie mamlaka yake vibaya ili kutuondoa Kwenye hoja ya msingi.

Pamoja na kwamba hii imefanyika kwa nia ovu ili kijiji kikose uwakilishi mahakamani.

3.kunyang'anya watu ardhi na kugawa kwa watu
Niambiwe ardhi kiasi gani na ni ya nani na nimempa nani na kama kuna ushahidi utolewe.

Mgogoro ninaujua ni ule wa ekari 1285 za kijiji ambayo waporaji wamechukua na kesi ipo mahakamani namwomba dc kama wao wameshindwa kutatua waiachie mahakama uhuru wa kuamua kesi ndio chombo cha juu Chenye kutoa haki.

Namwomba asiingilie hili jambo lipo mahakamani na anajua.

Tumeenda huko kwa kuona huku ktk ofisi yake tumekosa msaada huko nyuma japo tulionyesha imani kwake alipokuja Lakini imekuwa tofauti.

4.Hoja ya 150 milioni
Nyumba hizi zilijengwa na wageni wa Robin Hunt Safaris kwa kununua vifaa kumlipa fundi na ikisimamiwa na mhandisi wa wilaya
Hakuna sh hata moja nimepokea wala kijiji kimepokea kwa mfadhili bali walijenga nyumba na nyumba zipo engarooji zinatumika.

Kwa hili wakaguzi walikuja na takukuru pia. Labda kama kosa langu kukubali nyumba hiyo zijengwe basi niambiwe.

Wafadhili wapo waulizwe kama nilishika hata shilingi.

5.Hoja ya mapato na matumizi na hoja ya kuchangisha michango bila kibali
Nitazijibu kwa pamoja.

Sijawahi kuchangisha fedha yeyote niliomba ushahidi hakuna nilichunguzwa na takukuru huko nyuma sikuwa na hatia hoja hii ni ili kufifisha mapambano dhidi ya ardhi yetu na hii haiwezi kutuzuia.

Fedha zilichongwa ni sh 10000 ya kila mwananchi wa mondul na zinasimamiwa na wilaya sisi tulikabidhi huko.

7.Kuchukua mifugo na kuuza hii nayo naipuuza kama ambavyo nilipuuza tangu mwanzo

Kuhusu kufoji mihutasari mimi sio mwandishi wa mihutasari na hata hivyo vipo vyombo vya kuchunguza. Viachwe vifanye kazi.

Najiuliza kama Mh DC angekuwa na nia njema kwanini asingewapa vyombo vinavyohusika nafasi ya kuchunguza kabla ya kuchukua hatua hii haraka ya ghafla inatoka wapi.

Ndio tunapata hisia kuna msukumo wa rushwa katika ofisi yake na hili nilimwandikia kumtahadharisha wapo watu wanauza,Mifugo ili kuleta fedha katika ofisi yako.

Mwisho niseme nimwombe tena dc aache mahakama itoe haki na kama tuhuma dhidi yangu zenye mshiko Uchunguzi huru ufanywe ili niwe na Imani maana Kwa Sasa Ofisi yako inachuki na Mimi.

Wenu

Ngalama Mapema.
Mwenyekiti Kijiji Cha Eng'arooji
 
Tajiri akitoka mahakaman akiomba kesi ifutwe maana mkiti ameondolewa kisa kijiji hakina mwakilishi
Tuliwaambia nia ya kikao cha dc ni kufifisha kesi ya kijj

IMG-20210930-WA0028.jpg


IMG-20210930-WA0027.jpg
 
Hapa nimeagiza popcorn na sharubati ya ubuyu.

DC anaogeshwa wimawima hadharanj.

Kayataka
 
Hapa mkuu wa Wilaya ya Monduli ameharibu mno. Inabidi tu aondolewe kwa ajili ya kulinda intergrity ya ofisi ya DC. Kuna harufu ya vipande vya shekeli kutumika.
 
Vitus vinaendelea kuja. Hilo kundi la wananchi walikua na Lukuvi. Yeye DC anapotosha kwamba eti Waziri hakupewa ushirikiano. Rushwa mwanaharamu

IMG-20210929-WA0114.jpg
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom