Mkuu wa wilaya Mbeya awatusi waalimu

mikela
Dr Norman Sigalla, Mkuu Wa Wilaya Mbeya. "Ualimu Ni Fani Ya Watu Waliofeli Hivyo Hawana
Sababu Ya Kudai Nyongeza Ya Mishahara".

Mkuu, matusi tu? Mwenzake alishawacharaza viboko kule Bukoba na kusema "message sent", sijui kwa nani! Na wazazi wa Morogoro Manispaa walishawahi kuwatia "adabu" walimu wa shule moja hapo Manispaa kwa kuwapa mkong'oto. Vituko na dharau kwa walimu ni vingi sana. Dharau kwa walimu na kupuuzwa kwao kumeshazoeleka na walimu wameshakuwa sugu kwa hilo. Siku hizi imefikia hatua kwamba "kumtukana na kumdharau mwalimu" haileti "tija" na ni ushamba! Kwa walimu haina "noma". Kazi ni moja tu. Ni kupeleka sekondari "wasiojua kusoma na kuandika" kwa kwenda mbele! Walimu wameshasoma alama za nyakati! Walishapewa busara ya mbayuwayu-"akili ya kupewa....wanachanganya na ya kwao!" Mungu ibariki Tanzania!
 
Dr Norman Sigalla, Mkuu Wa Wilaya Mbeya. "Ualimu Ni Fani Ya Watu Waliofeli Hivyo Hawana
Sababu Ya Kudai Nyongeza Ya Mishahara".

Mkuu hata kwa Phd holder kuwa mkuu wa wilaya pia ni tusi. Unless u-Phd wake uwe ni wa kupewa au ndio uwe kama wa maji marefu.
 
Hawa wakuu wa wilaya wa safari hii hawaishi vituko,
Mara huyu kamkwida diwani, mara huyu kamwambia mewnzake ana degree ya chupi, sasa uyu tena ana watusi walimu.
Kweli wateule wa JK wanadhirisha sababu za wao kuteuliwa.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Unajua bosi wako akiwa hayuko serious hata subordinates nao wanakuwa hawako serious
Sikutegemea kauli itoke kwa DC
 
Hakika nawaambia, miaka ijayo Tanzania itakuwa ni nchi yenye maajabu mengi sana Duniani.Watalii wataongezeka kuja kuona maajabu yetu!Ehe, nchi yangu!
 
Dr Norman Sigalla, Mkuu Wa Wilaya Mbeya. "Ualimu Ni Fani Ya Watu Waliofeli Hivyo Hawana
Sababu Ya Kudai Nyongeza Ya Mishahara".

Mkuu hapo kwenye red, namjua huyu kanjanja vizuri sana hana phd ya kweli ni hizi za magumashi za kufanyia siasa ambazo ziliibuka kwa wingi kuelekea uchaguzi mkuu wa 2005. Ni msanii tu, mkewe kweli ana shule ni mwanasheria hajachonga vyeti kama huyu kimburu. Mkewe ni Pindi Chana ambaye nasikia anajipanga kumng'oa Deo Filikunjombe jimbo la Ludewa. Let's wait and see!
 
Mama yangu weee!! Huyu mkuu wa wilaya amesahau kuwa hata mpigania uhuru wetu Hayati Julius Kambarage Nyerere alikuwa ni Mwalimu lol!. Kamtusi hadi Nyerere huyu jamaa.
 
Mmmmmh! kwa zamani hii ingenikasirika sana na kuhisi walimu wamedhalilishwa sana, lakini kwa miaka ya hivi karibuni hasa serikali hii ya awamu ya nne nadahni kuna ka ukweli ndani yake! si ni kweli wanaojiunga na ualimu hasa wanaomaliza kidato cha nne wengi wao ni waliopata daraja la nne la hatari! si tunawakumbuka wale walimu wa miezi sita walipewa a.k.a ya walimu wa voda fasta!
 
Ni ulevi wa madaraka huo, mimi sijawahi kusikia dr au profesor ni mkuu wa wilaya na wanalipwa vizuri kuliko dr au pro au eng, akili kama hizi zinazidi kuwapa wazungu jeuri ya kutuita nyani, sasa kauli hi ilipaswa kusemwa mtu? Waafrika tunatukanwa kwa sababu ya kauli kama hizi yeye mwenyewe utakuta ni form 4 anatukana form 4
 
pole sana mama yangu ngoja mimi nikuombe msamaha maana hilo nyangau haliwezi kuomba msamaha maana limezoea vyeo vya kupewa pumbavu sana hilo jitu
 
Dr gani huyu uchwara?? Akili yake iko katikati ya mapaja!! Anadharau walimu?? Yeye una u-dr wake fake amezalisha wasomi wangapi??
 
Halafu huyu ndo mwakilishi wa rais katika wilaya,
WANAFUNZI WAKIFELI ANALAUMU WAKATI KESHATOA KAULI ZA KUWAVUNJA MOYO WAFANYAKAZI!
SAWA TUAMINI NIKWELI NI FANI YA WALIOFELI JE? HAWANA MAHITAJI SIMPLY KWA SABABU WAMEFELI?
HAKIKA UKIWA CCM HATA UKIWA DR HUWEZI TOFAUTISHWA NA DARASA LA SABA KWA UJENGAJI WA HOJA....
 
Halafu huyu ndo mwakilishi wa rais katika wilaya,
WANAFUNZI WAKIFELI ANALAUMU WAKATI KESHATOA KAULI ZA KUWAVUNJA MOYO WAFANYAKAZI!
SAWA TUAMINI NIKWELI NI FANI YA WALIOFELI JE? HAWANA MAHITAJI SIMPLY KWA SABABU WAMEFELI?
HAKIKA UKIWA CCM HATA UKIWA DR HUWEZI TOFAUTISHWA NA DARASA LA SABA KWA UJENGAJI WA HOJA....
Jina lake hilo(sigara)limempa saratani ya fikra.Anaona ukuu wa wilaya ndi kafikaaa.
 
Tuongee ukweli kutokana na maslahi duni watu wengi wanaochukua fani ya ualimu ni wale waliofeli na kukosa nafasi ya kuendelea na elimu ya juu ila mkuu wa wilaya alitumia lugha kali kwa idadi ya walimu tulionao zaidi ya robo tatu ni wale waliopata division four lakini akiwa kama sehemu ya serikali angepigania walimu waboreshewe maslahi ili tupate walimu waliofaulu vizuri(heshima ya walimu irudi)
 
Back
Top Bottom