Mkuu wa Wilaya Lushoto, Kalisti Lazaro azindua zoezi la vitambulisho vya Wajasiriamali

waziri2020

Senior Member
May 31, 2019
190
451
Mkuu wa Wilaya ya Lushoto ndugu Kalisti Lazaro leo Jumatatu tarehe 28/06/2021 alifanya Kikao cha Utambulisho na Wafanyakazi wa Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto.

Pamoja na kufanya Kikao cha Utambulisho na Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto pia alizindua Mafunzo Kwa Watendaji Kata kwa ajili ya Ugawaji wa Vitambulisho vya Wajasiriamali kwa Mwaka 2021

Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ya Lushoto aliwahasa Watumishi wa Halmashauri Kufanyaka kazi kwa Bidii na Maarifa na kuzingatia Sheria, Kanuni, Taratibu na Miongozo mbalimbali ya Serikali katika kuwatumikia Wananchi.

Pia aliwasihi Watumishi kuachana na Tabia ya kufanya kazi kwa Mazoea na Kuchongeana bali Wadumishe Ushirikiano, Mshikamano katika Kazi.

Mkuu wa Wilaya aliwasihii Watumishi Watimize Wajibu wao na Wajikite katika kutatua Changamoto na Kuondoa Kero za Wananchi kwa Kutatua Migogoro mbalimbali kwenye maeneo yao ya kazi.

Aliwatakia Mafunzo mema Watendaji wa Kata na kuwataka Kusimamia vema na kwa Ufasaha Zoezi la Ugawaji wa Vitambulisho vya Wajasiriamali bila kuleta Manung'uniko na Upendeleo.

IMG-20210628-WA0021.jpg
IMG-20210628-WA0022.jpg
IMG-20210628-WA0023.jpg
 
Back
Top Bottom