Mkuu wa Wilaya Kinondoni, Daniel Chongolo aagiza kukamatwa kwa Wanaume wanaonunua Changudoa

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Mkuu wa wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, Daniel Chongolo ameagiza polisi kata ya Kijitonyama kuwakamata wanaume wanaonunua machangudoa.

Chongolo ametoa agizo hilo leo Jumanne Novemba 6, 2018 kwa mkuu wa kituo cha polisi Kijitonyama, Said Lujuo wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa shule ya Msingi Kisiwani.

Kauli hiyo ya Chongolo ameitoa baada ya mkazi mmoja wa mtaa wa Nzasa kulalamikia suala la biashara ya ukahaba kukithiri kwenye mtaa anaoishi.

“Ikifika jioni tunashindwa kutoka nje na watoto wetu maana mambo yanayofanyika ni aibu, machangudoa wamejaa na hata tukipiga simu polisi wanawakamata na kuwaachia ndani ya muda mfupi,” amesema mkazi huyo.

Akizungumzia hilo, Lujuo amesema polisi huwa wanawakamata machangudoa lakini faini wanazotozwa ni ndogo na wanazilipa kwa haraka na kuachiwa.

“Pia hawa watu wana vigogo wao ndio wanawawezesha na kuwalipia faini ili waendelee kuwepo,” amesema.

Kufuatia hilo, Chongolo ameagiza wakamatwe na wanaume na wawekwe hadharani.

“Wakikamatwa wanaume na kuwekwa hadharani itakuwa funzo kwa wengine na makahaba hao watakosa wateja.”

“Polisi nendeni kwenye huo mtaa na mie nitakuja kuangalia hali ilivyo,” amesema Chongolo.

Chanzo; Mwananchi
 
Hii kuleta wakuu wa wilaya kutoka mikoani kuja kuongoza jiji la dar inakuaga nuksi sana.

Wanakuaga washamba wa jiji ...wanaleta hulka za mikoani hapa mjini.

Makahaba wanasaidia sana ..tuwape credits for that!
 
Nahisi hawa wakuu hawajui hata nini maana ya maendeleo na wanapaswa kufanya nini na kuachana na nini, uchangudoa ulikuwepo, upo na utakuwepo milele na Nchi zinging ni sehemu ya utalii...waache usani na wawaze masuala ya msingi kama maji, elimu bora, usafiri bora wa umma na barabara....si machangudoa hakuna aliewahi shinda hiyo vita....
 
Wakati huo huo Mh.Pohamba ameahidi kusaka Mabasha wote wanaonunua Mashoga Na kuahidi kuanza Operation ya kuwasaka Mara Moja

Team Makiki
 
Hii kuleta wakuu wa wilaya kutoka mikoani kuja kuongoza inakua nuksi sana.

Wanakua washamba wa jiji ...wanaleta hulka za mikoani hapa mjini.

Makahaba wanasaidia sana ..tuwape credits for that!
Sasa wewe nenda udakwe na changu wote mnaonyeshwa kwenye media kwa ile style ya kamanda muroto
 
Sheria zetu haziko hivyo kama huyo mkuu wa wilaya ya Kinondoni anavyotaka... akasome katiba vizuri aliyoiapia...

Sheria haikatazi kutongoza... Tuna bora viongozi na sio Viongozi bora yaani ni makapi tupu
 
Sasa wewe nenda udakwe na changu wote mnaonyeshwa kwenye media kwa ile style ya kamanda muroto
We matako unafikiri mimi wa kuja kama wewe....

ACP Charles Kenyela alitushindwa Kinondoni sembuse huyo mbwiga wa Dodoma.. Kenyela alikua RPC wa kinondoni mikwara mingi mbona alisanda...

i bet enzi za kenyela ulikua hujaja mjini kwa shemeji yako bado eti?

Chizi wewe mimi najua haki zangu kama Raia unafikiri nikiwa under arrest naropoka kama wewe....

Ndo mana mnaishia kuvungwa kwa ulimbukeni....
 
Tatizo la kiungo cha mwili kama makalio au K kujifanya mjuaji kuliko mikono na kichwa. Makalio yataendelea kua makalio yake ni uchafu tu
 
Back
Top Bottom