Mkuu wa wilaya Kinondoni alivyodhalilisha walimu siku ya Jumatatu Machi 7, 2016

Neyonzima

Member
Jun 11, 2015
67
129
Ndugu wakuu,
Jumatatu ya tar 7 March 2016 mkuu wa wilaya ya Kinondoni akiwa amebebana na waandishi wa Habari ambao aliwalipa alikwenda shule ya Msingi Tumaini iliyopo Kawe kupata maoni ya walimu kuhusu mpango wake wa nauli bure , walimu wote wakitoa maoni yao walipinga mpango huo wakimwambia wenyewe hawana shida na nauli na wala hawataki vitambulisho vyake ambavyo walimu hao waliviita ni vya udhalilishaji japo walimu wawili tu ndio waliunga mkono tena kwa unafiki.

DC huyo akaanza kuwatolea lugha chafu walimu hao tena mbele ya waandishi wa habari akisema ninyi ni wajinga , hamna elimu , hamjasoma na kashfa nyingine kibao kama nyie ndio mmetengeneza Makonda ambao hawajasoma na maneno mengi ya kashfa ambapo walimu hao walikaa kimya.

Kilichosikitisha walimu hao ni jinsi taarifa hiyo ilivyopotoshwa kwenye taarifa za Habari kwani walichukua kipande kile tu cha walimu waliomsifia kwa unafiki.

Kwa kweli walimu hao walichukizwa na yeyote ambaye yupo tayari kuwasaidia anaweza kwenda pale shuleni tumaini kupewa taarifa zaidi hapa nimeweka kwa kifupi sana.
 
Tunaomba waandishi wa Habari walio huru wafatilie udhalilishaji uliofanywa na dc na wauweke wazi , walimu wamekua wakidhalilika kila uchao bila jamii kuangalia ya kwamba hawa ni watu wenye mchango mkubwa katika kuzalisha wasomi na watendaji wazuri katika jamii
 
DC mwenyewe lofa ungetegemea lugha gani toka kinywani kwake.
 
Kwaiyo DC ataenda kila shule kuukizia mpango wake walimu wameupokeleaje? Hapo umechemka
 
walimu tuna hali ngumu, walimu na sisi pia tuna umuhimu, walimu, tutazua kitimutimu walimu hadi wizara ya elimu walimu. wagosi wa kaya hao nadhan mnaikumbuka hii ngoma enz hizo. ukiwa mwalimu nchi uthaminik kabisa
 
Nasema na ntazidi kusema shida ya mwalimu siyo sh 800| kwa siku wao wasikimbie majukumu yao nakuusukumia mzigo watu binafsi
 
Angemobilise walimu wote waongezewe pesa flani kama transport allowance kwny mishahara yao
 
Naona wanasiasa wanatafuta kiki kwa kuwatumia walimu.....Magufuli,Janeth,Majaliwa mko wapi? Walimu wenzenu mbona wanageuzwa jalala na wanasiasa uchwara!
 
Kwaiyo DC ataenda kila shule kuukizia mpango wake walimu wameupokeleaje? Hapo umechemka
Hizi zinaitwa conclusion za kinyumbu-nyumbu. Mtu unasoma habari halafu unawehitimisha kwa mtanzamo wa kijinga kabisa. Kwa kuwa alienda shule A basi ataenda kila shule.... Ni kama nyumbu anajiambia kwa kuwa nyumbu wamekurupuka basi ni lazima atakuwa simba. Soma tena: Inaonekana alienda pale ku-record ''show'' ya kuweka kwenye TV ili Magufuli azidi kumpenda! Ndio maana akanunua na ''mbwa wa habari'' ili wamsaidie malengo yake.
 
Kweli kabisa udhalilishaji alioufanya DC kwa walimu hao wa shule ya msingi Tumaini sio wa kufumbia macho, baada ya udhalilishaji huo na dc kuondoka ndipo walimu wakamuita mwalim mkuu wao kumuomba awasilishe hoja/lalamiko lao la kutukanwa na dc ndipo mwalim Mkuu huyo akawajibu walimu wake kua anaogopa bifu na mkuu wa wilaya kwani atamshugulikia ipasavyo na ye ana familia inayomtegemea kwa iyo yaishie hapo hapo
Je CWT mko wapi kutetea haki za walimu
 
Tena dc huyo akaongezea kwa sababu mmetengeneza makonda ninyi wenyewe kwa ujinga wenu ndio maana leo mnaogopa kwenda ku wa face kwenye madala dala , Aisee huyu dc alikosa adabu walimu wengine ni kina baba na kina mama wenye umri wa kumzaa kabisa
 
Kweli kabisa udhalilishaji alioufanya DC kwa walimu hao wa shule ya msingi Tumaini sio wa kufumbia macho, baada ya udhalilishaji huo na dc kuondoka ndipo walimu wakamuita mwalim mkuu wao kumuomba awasilishe hoja/lalamiko lao la kutukanwa na dc ndipo mwalim Mkuu huyo akawajibu walimu wake kua anaogopa bifu na mkuu wa wilaya kwani atamshugulikia ipasavyo na ye ana familia inayomtegemea kwa iyo yaishie hapo hapo
Je CWT mko wapi kutetea haki za walimu
Mkuu wa wilaya si mwajiri wa mwalimu,huyo Mkuu wa Shule ni mpuuzi,bado walim wana nafas ya kufikisha malalamiko yao kwa Waziri wa Utumishi wa Umma bi Angellah Kairuki na kwa Waziri Mkuu
 
Kama idea haiwezi kuwa implemented itakuwaje nzuri?
Ngoja nikupe mfano ,kumfikisha mwanamke kileleni kunaweza kufanyika kwa njia nyingi ,sasa badala ya wewe kucheza na parts husika unaishia kumvuta nywele ama kumsugua unyayo kwa brashi ukitegemea atafika unaweza ukawa sahihi ila njia uliyotumia haito kufikisha kwenye malengo yako kirahisi
 
Walimu waongezwe mishahara,wao ni watu wazima kuhusu usafiri budget yao watajuwa wenyewe kuliko kuwadhalilisha namna hii,kama kweli Makonda una nia ya kuwasadia walimu nunua mabasi specheli kwa ajili ya kusafirisha walimu tu,mbona sisi hapa wizara ya nishati tuna staff bus?Walimu msikubali huu uzalilishaji wa kuvalishwa vitambulisho vyenye number ya simu ya Makonda
 
Back
Top Bottom