Mkuu wa Wilaya Kinondoni afanya doria na Polisi saa 8 usiku

Egnecious

JF-Expert Member
Jul 8, 2015
875
960
DC KINONDONI AFANYA DORIA NA POLISI SAA 8 USIKU

*Avamia baa za usiku Oysterbay
*Ni zile zinazokera wananchi kupiga mziki kinyume cha sheria
*Mameneja, ma DJ waswekwa lupango

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh. Ally Hapi jana usiku majira ya saa 7 na 8 alifanya doria ya kushtukiza maeneo ya mitaa ya Oysterbay, Masaki na Kinondoni akiwa na kikosi cha Polisi cha Doria za usiku.

Akiwa amevalia kofia ya kapelo huku akifuatiwa kwa nyuma na gari la polisi, katika doria hiyo Mh. Hapi alivamia kwa kushtukiza eneo Oysterbay ambalo lina Club za usiku zinazopiga muziki nje kinyume na taratibu.

Mh. Mkuu wa Wilaya alifika katika club za Next Door na Samaki Samaki ambapo na kukuta muziki mkubwa ukipigwa na wahusika bila hofu na kuagiza polisi kuwakamata mameneja wote wa club hizo pamoja na wapiga muziki (DJ's) na mashine zao za muziki ambapo walipakizwa kwenye gari la polisi kimya kimya.

Hapi aliwaeleza wahusika hao kuwa hawezi kukubali kuona sheria zinavunjwa na wananchi wanateseka kwa adha ya kelele za muziki zinazosababishwa na club hizo licha ya kuonywa mara kadhaa kuacha tabia hiyo.

"Mmepewa onyo mara kadhaa na polisi, lakini mnafanya jeuri. Sasa nimekuja mwenyewe, na nitahakikisha mnalala rumande weekend hii ili muheshimu sheria tulizojiwekea.." alisema DC.

Mkuu huyo wa Wilaya ya Kinondoni akiwa na kikosi cha doria waliwafikisha kituo cha polisi cha polisi cha Oysterbay watuhumiwa hao na kuelekeza walale korokoroni huku taratibu nyingine zikisubiriwa.

DC Hapi alitembelea pia maeneo ya Masaki na mitaa mingine ya Kinondoni kabla ya kwenda kupumzika.
32f99c69b0c74d506f380b73a50dd13d.jpg
 
kinondoni mkwajuni inaongoza kwa vibaka usiku..badala akawakamate wale vibaka pale mkwajuni anaenda kuwakamata watu wanaoburudika club.. watu wengine hopeless kabisa

Hujui kuwa vibaka hushinda hizo baa za usiku sana wakivuta muda giza liingie watoke waanze kukaba watu!
 
Ila hili la baa, hasa bar na gesti kuwa maeneo ya makazi ya watu kero, kwanza wengi wao wanachelewa kufunga pili Kuna vitendo vya ngono vinaendelea, watu wanainamishana vichochoroni, watoto zetu wakipita wakienda shule wa naziona, mm mwezi wa nne Kuna dogo kwa macho yangu ana miaka mitatu nimwona kashika kondom iliyokwisha tumika bahati nzuri nilimuwahi, nikamlazimisha aitupe na siku nyingine asijaribu kuokota. Mimi hapa mtaani kunabaa mbili mita 30 Kutoka home na gest mita ishirini, alichokifanya muheshimiwa ni kizuri ila hiyo staili inaweza mghalimu, wanaweza wakamdhulu, waandae sheria zitakazo wabana wenye baa na wahakikishe zinafuatwa atakayenda kinyume ashughulikiwe
 
Bado nashangazwa na watu wachache humu.....wao kutokana na kulewa siasa kila jambo kwao ni negative....
Watu walikuwa wanalalamika sana kuhusu hizi kelele na hatimaye hatua zimechukuliwa.....
 
kampuni za bia zitashuka mauzo kama night club zitafungiwa ngoja tuone mwisho wake

Kwani wanywaji wanafuata makelele?

DC alichofuata ni kuzuia makelele na sio kufungia night club. Ikiwa wanywaji wanafuata makelele ya muziki basi ni kweli mauzo yatashuka kwani wapenda makelele hawataenda sehemu isiyo na makelele.

By the way hii biashara ya night club imevamiwa na wahuni tu... Biashara hii inahitaji uwekezaji ikiwemo sound proof (ukumbi wa kuzuia sauti) hall. Sasa mtu anaweka makuti tu naye anaita night club, muziki mkuubwa.

Funga kabisa ndugu DC Happy.
 
Ni jambo zuri kuzui makelele hayo. Ila pia hawa wakuu wetu wana malengo ya muda mrefu na priorities kweli? Bosi wake naye.alianza kwa ishu kibao sasa hivi hata hasikiki. Ishu kubwa kwa wananchi kwanza ni usalama wao ila hili sioni likipewa kipaumbele.na yeyote sio sijui ni kwanini. Anyway hii.ndio ile something is better than nothing na wengi hawajiulizi kwanini ukabali kidogo wakati unaweza fanya zaidi.
 
Huku mtaani kwetu mchana kimyaa, ngoja usiku ifike hatulali ni mashindano ya muziki kwenye bar
 
Back
Top Bottom