Mkuu wa Wilaya Iringa, Richard Kasesela amtukana dereva bajaji mbele ya vyombo vya habari

Status
Not open for further replies.

misimajumbasita

Senior Member
Jun 10, 2018
157
272
Kwanza naanza kwa kumpa sifa Mungu wetu muweza wa yote kwa kutuepushia mbali na upepo wa Jobo Tanzania ni salama

Kama kichwa cha habari kinavoeleza mkuu wa Wilaya ya Iringa ndugu Richard Kasesela akiwa anaendelea kuongea na madereva bajaji katika mkutano huo, Mkuu huyu wa wilaya alisikika akimuambia mmoja wa dereva aliyeudhuria huo mkuatano “ TULIZA MATAKO YAKO WEWE”

Waandishi sote tulibaki mdomo wazi na kufanya mkutano huo wa Mkuu wa Wilaya na madereva bajaji kuishia hapo. Video itawajia punde

Mkutano ulijiri tu Mara tu baada ya bajaji kufanya mgomo wilayani hapo.

Zaidi, soma: Uungwana: DC wa Iringa Mjini Richard Kasesela aomba radhi kutokana na kuteleza kwa ulimi wake


 
Hajui kucheza na nyakati huyo!!
Jobo kapita nae mzima mzima hata asisibiri teuzi.
 
Kasesela alipata kiki alipokuwa anamtukana Msigwa. Sasa hivi Msigwa hayupo ameanza kutukana madereva bajaji.

Asichokijua Kasesela ni kuwa kugombana na madereva bajaji ni sawa na kugusa mboni ya mbunge wa Iringa mjini Jesca Msambatavangu.

Juzi Jesca alipambana na Kasesela na RPC hadi vijana wa bajaji wakarudi barabarani.

USHAURI WANGU: Iringa bado ni mji mdogo sana wawaache vijana wajiajiri ikiwemo kuendesha bajaji. Abiria ndio achague apande bajaji au daladala. Pia Iringa foleni hamna sijui KASESELA ANAWASHWA NA NINI?
 
Hakuna tusi hapo, nikiungo cha binadamu wa jinsia zote wanazo, ingelikuwa ametaja kiungo cha jinsia nyingine kwa mtu wa jinsia nyingine tungesema amemtukana.
 
Status
Not open for further replies.
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom