MR.NOMA
JF-Expert Member
- Feb 1, 2014
- 338
- 504
-MKUU wa Wilaya ya Songea Pololet Kamando Mgema amezungumza na waandishi wa habari mkoani Ruvuma jioni hii ofisini kwake kuhusu zoezi la kufungwa kwa vibanda vya biashara vilivyopo soko kuu Manispaa ya songea lililofanyika siku ya jumamosi tar 11/02/17.
-Amesema kuanzia Julai 2016 mpaka Januari 2017 halmashauri ilishindwa kukusanya zaidi ya Tsh.milioni 145 kama kodi kutoka kwa wapangaji wafanyabiashara katika vibanda vya soko hilo.
-Amesema zoezi la kukusanya kodi lilishindikana kutokana na uongozi wa umoja wa wafanyabiashara hao kuwazuia wafanyabiashara kusaini mikataba ya mpangishaji(serikali) na hivyo kutolipa kodi ya pango.
-Ametoa rai kwa wafanyabiashara kusaini mikataba na kulipa kodi ya pango wanalodaiwa ili vibanda vyao vifunguliwe.