Mkuu wa wilaya awapiga marufuku walimu kuzuia kuandikisha wanafunzi kisa vyeti vya kuzaliwa

comrade igwe

JF-Expert Member
Jan 12, 2015
7,295
3,945




Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Fadhili Nkurlu amewapiga marufuku walimu wakuu wa shule za msingi na sekondari kuzuia kuandikisha wanafunzi wa kidato cha kwanza na darasa la kwanza hadi wawe na vyeti vya kuzaliwa.

Nkurlu alitoa agizo hilo baada ya baadhi ya wazazi na wanafunzi kufika ofisini kwake kusaka vyeti na wengine kulalamika kitendo cha walimu kuwazuia kuanza kidato cha kwanza.

“Ni marufuku kwa mwalimu yeyote au kiongozi kuzuia wanafunzi kuandikisha kwa madai ya cheti cha kuzaliwa kama wanataka kujiridhisha wapate barua kutoka kwa mwenyekiti wa kitongoji au watendaji wa kijiji na siyo cheti hicho,” alisema Nkurlu.

Mmoja wa maofisa elimu kutoka Halmashauri ya Mji wa Kahama, Aruko Lukolela alisema agizo la mkuu wa wilaya litatekelezwa mara moja.
 
Bila cheti cha kuzaliwa linazaliwa tatizo la kukinzana majina mwisho wa siku na kuonekana labda mtu ana cheti feki...
 
Hakuna hoja hapo.
Toka lini kujiandikisha mpaka uwe na cheti cha kuzaliwa?

Mmoja wa ma DC ambaye anatapatapa hana lolote lile jipya.
 
Serikali ya matamko kila kiongoz ana maamuzi yake.
Hapo bado Malaika mkuu wa Lizaboni hajasema
 
Nafikiri hujaelewa hoja mkuu,
DC kazuia wale waliokuwa wanataka mpaka mtoto awe na cheti za kuzaliwa na badala yake kasema waandikishwe bila hilo sharti la kuwa birth certificate.

Hakuna hoja hapo.
Toka lini kujiandikisha mpaka uwe na cheti cha kuzaliwa?

Mmoja wa ma DC ambaye anatapatapa hana lolote lile jipya.
 
Back
Top Bottom