Mkuu wa Wilaya Arumeru unapaswa kuwajibishwa kwa mtoto aliyetoa mimba

kifupi kirefu

JF-Expert Member
Oct 29, 2018
539
3,507
Nimemsikia MKUU WA WILAYA YA ARUMERU akizungumza kwenye vyombo vya habari akijipongeza kumzuia mtoto kufanya mtahani lakini pia akilazimisha kuwa taarifa hizo alizipata kwa kufanya uchunguzi wakati mama mzazi anakiri ndiye aliyefika kwa mkuu wa Wilaya kuomba kibali Cha mtoto kurudi shule.

Ni Jambo la kusikitisha kwa kiongozi huyu kushindwa kuelewa kwamba mipango na shinikizo lake lililopelekea binti kutoa mimba lingeweza kupelekea binti huyo kupoteza maisha. Badala ya kufanya kazi Kama mzazi anafanya kazi kwa msukumo binafsi wa kutetea nafasi yake

Mkuu wa Wilaya anapaswa kuwa na Siri, mama wa watu kaenda kwake kwa uchungu wa yaliyompata mwanaye badala ya kuweka Siri unamkamata na kumwita waandishi wa habari.

Tunakwenda wapi?
 
Yan huu ni upumbavu,.mtoto atoe mimba awajibishwe Mkuu wa wilaya??

Tutumie logic kabla ya kupost ujinga
 
kaazi kweli kweli!
Halafu kuna mtu analinganishwa na Mwalimu Nyerere, Hivi Mwalimu wanamjua au wanamsikia?, yaani mteuliwa aonee wananchi hivihivi halafu mwalimu amtazame tu, thubutu!, Yaani mbele ya Mwalimu ilikuwa bora uliibie shirika la Umma kuliko ajue kuwa unanyanyasa watu!
 
Nimemsikia MKUU WA WILAYA YA ARUMERU akizungumza kwenye vyombo vya habari akijipongeza kumzuia mtoto kufanya mtahani lakini pia akilazimisha kuwa taarifa hizo alizipata kwa kufanya uchunguzi wakati mama mzazi anakiri ndiye aliyefika kwa mkuu wa Wilaya kuomba kibali Cha mtoto kurudi shule.

Ni Jambo la kusikitisha kwa kiongozi huyu kushindwa kuelewa kwamba mipango na shinikizo lake lililopelekea binti kutoa mimba lingeweza kupelekea binti huyo kupoteza maisha. Badala ya kufanya kazi Kama mzazi anafanya kazi kwa msukumo binafsi wa kutetea nafasi yake

Mkuu wa Wilaya anapaswa kuwa na Siri, mama wa watu kaenda kwake kwa uchungu wa yaliyompata mwanaye badala ya kuweka Siri unamkamata na kumwita waandishi wa habari.

Tunakwenda wapi?
Ni matokeo ya kuteua mtu kwa kutumia sifa moja tu ya uropokaji! Huyu DC hana sifa za kuwa hata mjumbe wa nyumba kumi...inashangaza mno awamu hii kukusanya viongozi wa ajabu ajabu...maadili hawana, hekima hakuna, upstairs weupe..Mungu atusaidie sana!
 
Back
Top Bottom