Mkuu wa wilaya aingia darasani-afundisha hesabu za maumbo

MAKOLE

JF-Expert Member
Feb 5, 2012
618
280
Chalii amenijuza kuwa Mkuu wa Wilaya Korogwe ameingia darasani kufundisha hesabu za kujumlisha darasa la saba na maumbo darasa la sita kufuatia mgomo wa walimu. Mkuu huyo aliingia kupiga nondo hizo katika shule ya msingi Mazoezi-Mbeza iliyopo katikati ya mji wa Korogwe.
 
yaani nchi hii sanaa kila mahali kuanzia magogoni mpaka huko korogwe
 
Wangekuwa wanamajukumu kama haya tungeona sababu za cheo hiki kuwepo. Yani kigezo cha kuchaguliwa kuwa mkuu wa wilaya ni lazima uwe unajua fani mbalimbali, na pale mapungufu yanapojitokeza unakwenda kuziba faster Mfano walimu wakigoma, madaktari, maengineer nk, basi maramoja wakuu hao wanaenda kuziba mapengo hayo.
 
Sasa huyo hapo bado kachemsha angetangaza wakuu wa wilaya nchi nzima washike huo wadhifa alafu baada ya wiki watupe ripoti ya chaki imekaaje,waache kujaribisha mambo badala ya kumshauri DHAIFU atatue tatizo la msingi.
 
Hongera mkuu wa wilaya!!! Inanikumbusha PROFESA SARUNGI wakati akiwa PWANI hospitali ya TUMBI inamtambua....wakati wa AJAL YA TRENI DODOMA alishiriki kwa kiwango cha juu....huku magari ya wabunge yakichukua jukumu la AMBULANCE
 
sio kila anayejua kusoma na kuandika afaa kuwa mwandishi,vivyo hivyo si kila ajuaye kusoma na kuandika anafaa kuwa mwalimu,na lazima itambulika kuwa ualimu si fani ya kila mtu,mi naona atakuwa alikuwa anawafundisha vijana ufisadi na udhaifu tu
 
Aisee sasa mkuu wa wilaya anafundisha shule nzima? syllabus ya madarasa yote.
 
Mrisho Gambo ana uzoefu gani wa ualimu huyu kama hawalostishi watoto bure?
Mwanasiasa na chaki wapi wapi, aache hizo bana, atawafundisha watoto abc's za kuiba!
 
Siasa tu hizo!!Anatafuta umaarufu na kesho tena aende kufundisha na je atafundisha masomo yote?
 
Ao walishaambiwa sio mtaji,ata kura zao sio dili..teh teh,ngoja tuone ndo kwanza episode ya kwanza..
 
Nampongeza kwa ujasiri wake manake kufundisha si mchezo, Subirini akiandika refund ndio mtajua kwamba alikuwa anafundisha kwa moyo au alikuwa anapiga dili zake, vipi yule engineer mfagiaji wa barabara yeye hajaenda kufundisha mkoani kwake?
 
Duh!huyo mkuu wa wilaya ana kiherehere kweli,anaujua vizuri syllabi ya shule za msingi?nini wanapaswa kufundishwa na nini hawapaswi kufundishwa?je kipi kinapaswa kutangulia kufundishwa na kipi kifuatie?
 
Duh! Hii kali... Tanzania zaidi ya uijuavyo. Ningependa mgomo uendelee na huyo mkuu wa wilaya aendelee na chaki, ili ashuhudie ziro
 
Chalii amenijuza kuwa Mkuu wa Wilaya Korogwe ameingia darasani kufundisha hesabu za kujumlisha darasa la saba na maumbo darasa la sita kufuatia mgomo wa walimu. Mkuu huyo aliingia kupiga nondo hizo katika shule ya msingi Mazoezi-Mbeza iliyopo katikati ya mji wa Korogwe.

Je, ana taaluma ya ualimu? Kama alikuwa mwalimu kwa nini aliacha kazi hiyo? Na huko ofisini kwake kamwachia nani?
 
Bwana misosi sasa naimba ...Nitoke vipiiiii......aka kasongi nimekamiss...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom