Mkuu wa wilaya aamrisha nesi kuwekwa ndani kwa kosa la kuuza nguo kazini

Kosa lipo, shida ni namna alivyokamatwa nakufungwa pingu kwa nyuma kama jambazi hatari.
 
Kinachoniuma zaidi, katoka kumsaidia mgonjwa kujifungua na amekutwa anajaza form, ikimaanisha kakutwa akiwa anatekeleza majukumu yake. Sijajua atashtakiwa kwa kosa la kuhifashi nguo kwenye makabati au kufanya biashara hospitali.

Nna dhambi nyingi napambana nazo lakini hii ya kuwachukia polisi itanipeleka kuzimu nisipokua makini. Nawachukia polisi sana, najua sio jambo zuri lakini siwezi kuficha chuki yangu dhidi yao.


Mkuu kuna jamaa zangu wanapanga kumtenga kaka yao ambaye ni askari polisi, nikiwauliza kosa hakuna anayeniambia ila moja kaniambia wanakutana ili kumtenga rasmi na familia yao. Sasa hii chuki dhidi ya askari inapitiliza kiasi, kumbukeni hawa ndg zetu nao ni kama watumwa tu wanatekeleza wanachoambiwa hata kama ni kuzuri au kibaya.
 
Acheni kutetea ujinga wa huyo nesi!

Ni kweli, niliwahi kuona Muhimbili, nesi akikataa kumhudumia mama aliyekuwa ana lalamika kitandani wodi ya kina mama, kisa alikuwa anatanganza biashara yake ya nguo.
Hakuna biashara kazini, afanye kazi aliyoajiriwa kufanya, inafikia wakati hupati huduma kama hujamuungisha biashara.
 
Mbona mawizarani kuna watu wanauza asali na vingine vingi tu lakini hawakamatwi Tena wateja wakiwa ni makatibu na mawaziri ukiwa na ELIMU Ndogo ni lazima ufanye vitu vitakavyo muaibisha aliye kuamini na kukupa kazi
 
Best employers always will be in the private sector!

The government is on the verge of becoming the worst employer in the land!

Mpaka mkuu wa wilaya kumfunga nesi umepita grupu kubwa sana la watu kumkuta yeye!

Unamfunga nesi wa zamu unawaacha mkuu wa hospitali,daktari mkuu wake,mkuu wa manesi,daktari wa zamu,etc.Watu kama kumi hivi!

Hii staili ya utawala inaitwa "Ubambuzi"!Yaani unakaa msituni,swala wakipita unakurupuka na mmoja,tena yule mvivu kukimbia ndio unamtaka!

Hhahahahaahaaaa
 
Kosa ni kosa. Kutoshughulikia makosa mengine hakualalishi makosa mengine.

Huyu nesi kavunja sheria na wajibu wake wa eneo la kazi, sheria ifuate mkondo wake.

Watanganyika bado mnaendeshwa kwa hisia, acheni kutetea ujinga.
 
Kinachoniuma zaidi, katoka kumsaidia mgonjwa kujifungua na amekutwa anajaza form, ikimaanisha kakutwa akiwa anatekeleza majukumu yake. Sijajua atashtakiwa kwa kosa la kuhifashi nguo kwenye makabati au kufanya biashara hospitali.

Nna dhambi nyingi napambana nazo lakini hii ya kuwachukia polisi itanipeleka kuzimu nisipokua makini. Nawachukia polisi sana, najua sio jambo zuri lakini siwezi kuficha chuki yangu dhidi yao.
Sasa polisi ulitaka wakatae kutii ORDER ya boss wao ?

- Tatizo ni utawala mbovu wa CCM unaolazimisha KUFUKARISHA kila MTU, Wakikukuta unapambana KUJIKWAMUA, Unapigwa MTAMA mmoja MATATA, ndio maana hata pesa zenu za FAO LA KUJITOA wamedhulumu., Lengo ni watu waishi kama SHETANI
 
Acheni kutetea ujinga wa huyo nesi!
Watanganyika bado wanaendeshwa kwa hisia, wamezoea kuishi kama wanyama yani bila kufuata sheria, sheria ikifuatwa wanaanza kulalamika na kupinga. Hawajui wanataka nini

Huyu nesi, pamoja na hali zao kuwa ngumu, kafanya makosa acha sheria ifuate mkondo wake
 
Mbona hata huku kwetu manesi wanauzia sana wazazi nguo za watoto wachanga?? Je kuna wagonjwa waliolalamika?? Ss tunaona wanatusaidia, tunarudi nyumbani mtoto kapendeza kavaa soksi, kofia na baby shawel nzuriii!!!
Kuna watu hata hawajui mtt akizaliwa anapaswa kuvaa nn hana hata muda wa kwenda kununua ila anajua mke wngu akifika hosp nitapata hii huduma pale pale ,,inarahisisha sana

Je alikuwa anauza nguo muda wa kutoa huduma? Hapana ...kakutwa akijaza kadi katoka kuzalisha hahhahaaaa jeshi la polis na wenye kujibebea mamlaka ipo siku yenu
 
Labda kwa kuwa hajalipa kodi ya hiyo biashara, kwamba pengine alitakiwa kutafuta eneo maalum, amuweke mtu wa kuuza ili serikali ipate chake, na Mtz mwingine mmoja kupewa ajira.
 
Huyu mkuu wa wilaya alienda kujifungua ndio kakutana na hiyo hali au aliipangilia toka ofisini?
Kama alipangilia ratiba kabisa:
Je, dk wa zamu alishtaki?
Au mgonjwa yeyote?
Au nesi mkuu wa zamu?
Ama ilikuwakuwaje! Panahitaji ufafanuzi zaidi hapa.

Alifungwa pingu, kwani aligoma kukamatwa!
 
Kosa ni kosa. Kutoshughulikia makosa mengine hakualalishi makosa mengine.

Huyu nesi kavunja sheria na wajibu wake wa eneo la kazi, sheria ifuate mkondo wake.

Watanganyika bado mnaendeshwa kwa hisia, acheni kutetea ujinga.
Kosa la huyo nesi ni lipi....mkuu mkeo ashawahi jifungua??tuanzie hapo kwanza
 
Lakini huyo DC kaenda mbali sana. Hospital kuna katibu wa Afya, kuna nurse in charge, mganga mfawidhi, bado ktk halmashauri kuna DMO, afisa utumishi na Mkurugenzi. Ina maana alishindwa kutoa maagizo ya utawala kudeal na hilo jambo hadi afanye yeye? Henry Fayol alieleza umuhìmu wa kufuata chain of command katika utawala, hawa wenzetu vipi?
 
Kosa la huyo nesi ni lipi....mkuu mkeo ashawahi jifungua??tuanzie hapo kwanza
Huoni kosa au unatetea tu? Wewe unaweza kwenda kuuza vitu unapofanya kazi?

Huu sio muda wa kuishi kama wanyama bila kufuata sheria vinginevyo mtalialia kila siku.
 
Back
Top Bottom