Mkuu wa WHO asikitishwa na ongezeko la maambukizi ya Corona kuwahi kushuhudiwa kwa wiki 7

Emmanuel Kasomi

Verified Member
Oct 18, 2019
2,941
2,000
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la afya duniani amesema hii ni hali ya "kukatisha tamaa lakini sio ya kushangaza "

Baada ya idadi ya maambukizi mapya ya virusi vya corona pamoja na vifo kushuka kote duniani katika kipindi cha wiki saba, idadi ya maambukizi na vifo imeongezeka tena, Shirika la Afya duniani limeonya.

Mkurugenzi mkuu wa WHO, Tedros Adhanom Ghebreyesus, amesema "inasikitisha lakini haishangazi " ikizingatiwa kwa maoni yake, nchi nyingi "zimelegeza mashari na maagizo ya kujikinga na maambukizi ."

Tedros alieleza kuwa ongezeko la idadi ya maambukizi na vifo katika mataifa ya Ulaya, Marekani na Mashariki ya kati na Kusini mwa Asia, ingawa katika Afrika na Mashariki mwa Asia wastani wa maambukizi umesalia kuwa wa kiwango kilichokuwepo awali.

Amesema pia kwamba WHO inajaribu kubaini ni nini kinachoweza kuwa sababu za ongezeko hilo la maambukizi.

"Tunafanya juhudi za kuelewa ongezeko hili la maambukizi, ingawa katika baadhi ya visa, ni kutokana na kulegezwa ka hatua za afya ya umma, pamoja na kusambaa kwa aina mpya ya virusi na kwamba watu wameacha kujikinga " alisema.

"Kama nchi zinaamini kuwa zinategemea chanjo sana, wanafanya makosa . Hatua za kimsingi za afya ya umma zinasalia kuwa jibu la msingi la afya ," alisema.

Tedros pia amezikosoa nchi tajiri kwa kujilimbikizia dozi za chanjo na kusema kuwa ni maslahi ya kila mtu kwamba watu wenye uwezekano mkubwa wa kupata maambukizi wanalindwa kote duniani.

Inasikitisha kwamba baadhi ya nchi zinaendelea kupatia kipaumbele kuwachanja vijana, watu wazima wenye afya wenye kiwango cha chini cha hatari ya ugonjwa, kabla ya kuwachanja wahudumu wa afya na wazee ," alisema.

Taarisi ya udhibiti wa magonjwa nchini Marekani mapema wiki hii pia ilionya juu ya ongezeko la maambukizi na vifo ambavyo vimekuwa vikiripotiwa nchini humo katika kipindi cha wiki iliyopita.

"Wakati huu, ambapo aina mpya ya virusi inasambaa, tuna hatari ya kushindwa kufikia mafanikio ambayo tumekuwa tukiyafanyia kazi kwa muda mrefu kuyapata ,"anasema mkurugenzi wa taasisi hiyo, Rochelle Welensky.

Wiki iliyopita Marekani iliidhinisha chanjo ya tatu ya corona, ya kwanza ambayo dozi moja inatosha, kutoka kampuni ya madawa ya Johnson and Johnson, na nchi kadhaa pia zinatarajia kuiidhinisha na kuongezwa katika mipango yao ya kampeni ya chanjo mnamo wiki kadhaa zijazo.
 
marxlups

JF-Expert Member
Dec 12, 2011
14,786

Kuna mataifa yamegoma kutoa ushirikiano wa kupambana na gonjwa
 
Crocodiletooth

JF-Expert Member
Oct 28, 2012
11,565

Imeshuka imepanda?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom