Mkuu wa Utumishi Jeshini, Meja Jenerali Paul Kisesa: Jeshi la Wananchi halina chama

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
21,271
47,271
Wakati Taifa likielekea kwenye Uchaguzi Mkuu Mwezi Oktoba 2020, Mkuu wa utumishi Jeshini Meja Jenerali Paul Kisesa Simuli amewatahadharisha Askari wa Jeshi la wananchi kujihadhari na ushabiki wa Kisiasa.

JESHI%201.jpg

Mkuu wa utumishi Jeshini Meja Jenerali Paul Kisesa Simuli

Meja Jenerali Simuli ametoa tahadhari hiyo wilayani arumeru Mkoani Arusha katika kikosi cha Jeshi 833 Oljoro, Wakati wa kufunga mafunzo ya askari wapya kundi maalumu la nne la mwaka 2020 mchepuo wa sayansi, ambapo wakiwa katika mafunzo, Askari hao wapya walipitia mafunzo mbalimbali ya kijeshi ikiwemo ujasiri na matumizi ya silaha nzitoo za kivita.

Meja Jenerali Simuli amesema kwa kufanya hivyo wanaweza kuhatarisha amani ya taifa, huku akiongeza kuwa Askari hao bado wanao Uhuru wa kumchagua kiongozi wanaye mtaka kama walivyo raia wengine.
 
Hii ndo taasisi pekee ambayo bado haijanajisiwa Tanzania. Ndo taasisi pekee iliyobaki na weredi wake.

Asante sana kwa jaribio la kumuondoa Mzee wa Butiama mwaka1964 lililoifanya hii taasisi ijengwe free from political influence.

Tunategemea mtasimama upande wa wananchi hapo October 2020 baada ya matokeo ya uchaguzi kutangazwa.
 
Huwa nashindwa kuelewa.

Kwamba jeshi halina chama lakini wanajeshi wanaruhusiwa kumchagua/ kumpigia kura mgombea wa chama cha siasa wampendaye!

Makes no sense.
Unaweza chagua mgombea na Usiwe na chamaa...!! Hata wanaopiga kura wengi hawana vyamaaa..
 
Mbona wanajeshi wanateuliwa kuwa MaRc? Ambao Ni wajumbe Wa kamati za siasa za ccm mkoa?

Kwani kuingia kwenye vikao vya chama ni kujihusisha na siasa?

Chama kinaunda serikali na serikali imewaajiri kwa hiyo huwezi kusema wasifanye kazi ya inayofanywa na chama tawala.

CCM inatekeleza ilani kwa wananchi wote bila kujali itikadi cheo au kabila.

Kwa hiyo jeshi nalo lipo chini ya amiri jeshi ambaye ni mwana-CCM tena ni mwenyekiti.
 
Huwa nashindwa kuelewa.

Kwamba jeshi halina chama lakini wanajeshi wanaruhusiwa kumchagua/ kumpigia kura mgombea wa chama cha siasa wampendaye!

Makes no sense.


Wapiga kura wengi Mimi nikiwemo si wanachama wa chama chochote cha siasa.

Wanachama wa vyama vyote vya siasa hawazidi 10 million,wapiga kura ni zaidi 30 millions.

Natumaini umenielewa na siku nyingine utaelewa zaidi na zaidi bila chenga.

Wasalamu

Ngongo kwasasa safarini Masasi.
 
Huwa nashindwa kuelewa.

Kwamba jeshi halina chama lakini wanajeshi wanaruhusiwa kumchagua/ kumpigia kura mgombea wa chama cha siasa wampendaye!

Makes no sense.
Nchi ngumu hii. Viongozi wanatuambia Serikali haina dini. Afu unamuona Kiongozi anaenda kutolea Matamko ktk Nyumba ya Ibada. Serikali haiamini UCHAWI lkn mara kadhaa Serikali unaskia inayafanyia kazi mambo km hayo! Huku Kijijini kwetu kuna Mwl Mkuu wa Shule kahamishwa kisa tuhuma za Uchawi.
 
Huwa nashindwa kuelewa.

Kwamba jeshi halina chama lakini wanajeshi wanaruhusiwa kumchagua/ kumpigia kura mgombea wa chama cha siasa wampendaye!

Makes no sense.
Wana haki ya kuchagua lakini hawana ya kuchaguliwa?
 
Back
Top Bottom