Mkuu wa Upelelezi Arusha: Niliona mapungufu kwa Sabaya, alikuwa mteule wa Rais sikufanya chochote

Akitoa ushahidi wa kesi ya Sabaya, Mkuu wa upelelezi amesema alipigiwa simu na aliyekuwa DC wa Arusha Kenani Kihongosi akiniarifu kuwa DC wa Hai ana watuhumiwa hapa Arusha hivyo nimpe ushirikiano.

Mara baada ya kufika ofisini kwangu akiwa na watuhumiwa wawili niliambiwa hawa ni wahujumu uchumi, nikamuomba aandike maelezo, Sabaya akagoma. Niligundua kuna mapungufu kwa mshitakiwa No 1(Sabaya) hivyo sikuweza kufanya lolote kwa kuwa mshitakiwa No 1 alikuwa mteule wa Rais.

Mteule wa Rais aweza vunja sheria badala ya kusimamia sheria na akapoteza ushahidi.

KATIBA INAHITAJIKA?

Hapo wala sio katiba. Acha Utoto. Hakuna mahali ambapo Rais au katiba itaruhusu mtu kufanya uharifu kisa mteule. Na anajua huyo mtu.
 
Ni ngumu mtu kuelewa nini maana ya siasa, kwa mtu anaejua maana ya siasa sabaya hana kesi. Endeleeni na ujinga tu kuna siku watamuachia wenyewe.

Kama sio siasa mbona hakuna anaemgusa makonda?
Kuipotezea mahakama muda ni ujinga hayo makesi ya kipuuzi yafutwe.

Utawala ule umetoka bado hamuelewi somo? Kesi za kipuuzi sana hizi, huyu mama nae kha!
Wonder shall never end.. Usikute Kuna mtu nyuma yako uwa anawasimulia marafiki zake kuwa Ana wife material.
 
Hata ikiwepo KATIBA MPYA bado itasimamiwa na wanadamu....

Kubwa ni umuhimu wa umakini katika VETTING kuanzia juu kabisa mpaka chini....

#KaziIendelee
nakubaliana na wewe kwa asilimia kubwa lkn pia kama binadam hatutakiwi kuishi kwa kudra za mtu lazima tuwe na taratibu na sheria zitakazo tulazimisha kuishi kwa kutenda haki na kutimiza wajibu na tukishindwa kutekeleza yale tuliyopaswa kutekeleza basi yatupasa tuadhibiwe kwa mujibu wa sheria. Lazima tukubali kwa sasa katiba yetu inamapungufu makubwa na yakimsingi na ukweli mpaka sasa tunaishi hivi ni kwa kudra za viongozi wetu lkn wanauwezo WAKUTUZINGUA kuliko awamu zote sbb katiba ipo loose kimtindo.
 
Angalau wewe unauona mwanga! Katiba ni kitabu kama vilivyo vingine, kama hii iliyopo haiheshimiwi, hiyo tunayoitaka utekelezaji wake utalindwa na nani?
Point to make! Katiba itokanayo na wananchi Ina tabia ya kujilinda na haihitaji ulinzi wa yeyote yule awaye! Hii mnayoivunja haikutokana na wananchi Bali viongozi wachache na ndio maana haiwezi kujilinda, kujisimamia na kujiongoza yenyewe kwani ni Mali ya kikundi kidogo Cha watu!
 
Point to make! Katiba itokanayo na wananchi Ina tabia ya kujilinda na haihitaji ulinzi wa yeyote yule awaye! Hii mnayoivunja haikutokana na wananchi Bali viongozi wachache na ndio maana haiwezi kujilinda, kujisimamia na kujiongoza yenyewe kwani ni Mali ya kikundi kidogo Cha watu!
Angalia vizuri hata Kenya inavunjwa. Je, kenya ufisadi umeisha baada ya katiba mnayoisifia? Kumbuka hakuna mtu anaweza kuingiza kichwa katika mdomo wa mamba. Katiba mpya ni kuinyang’anya ulaji Ccm na kumnyang’anya madaraka Samia ya kuchukua Airbus kwenda asubuhi Dodoma na chakula cha mchana akala Dar ikulu. Ningelikuwa ni nyie kwanza ningepambana wabadili bungeni ile sheria ya kipuuzi ambayo lazima Rais awe final say katika mchakato wa kutengeneza katiba mpya. Na washiriki wa mchakato pamoja na Rais wasigombee uongozi wowote kwa muda wa miaka 20. Hapo itapatikana katiba ya maana
 
Hata ikiwepo KATIBA MPYA bado itasimamiwa na wanadamu....

Kubwa ni umuhimu wa umakini katika VETTING kuanzia juu kabisa mpaka chini....

#KaziIendelee
Katiba haikwepi.
Watakaovunja Katiba tutakula nao sahani moja muda ukifika.
 
Back
Top Bottom