Mkuu wa upelelezi aelezea alivyomnasa Tundu Lissu

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,227
5,287
MKUU wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai wa Wilaya (OCCID), Yustino Mgonja ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa alimkamata Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu baada ya Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalumu (ZCO), Camilius Wambura kumtaka afanye hivyo.

Mgonja ambaye ni shahidi wa nne katika kesi ya kutumia lugha ya uchochezi inayomkabili Lissu, alidai hayo jana mbele ya Hakimu Mkazi, Godfrey Mwambapa kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kusikilizwa.

Akiongozwa na Wakili Mwandamizi wa Serikali, Mutalemwa Kishenyi, shahidi huyo alidai kuwa Juni 28, mwaka jana, Wambura alimpa maelekezo ya kumkamata Lissu kwa kosa la kutoa lugha za uchochezi katika viwanja vya mahakama hiyo.

Alidai kuwa Juni 29 mwaka jana saa 7 mchana alienda nyumbani kwa Lissu maeneo ya Tegeta wilayani Kinondoni, ambapo alimkamata na kumfikisha katika ofisi ya ZCO na kumkabidhi.

“Nilipewa amri na ZCO nikukamate hivyo kwa mamlaka hayo bila kuwa na hati ya ukamataji naweza kukukamata; kwani makosa yoyote ya jinai unaruhusiwa kukamata bila kuwa na hati hiyo,” alidai Mhonja.

Pia alidai kuwa kumpinga Rais anapokosea sio kosa na kwamba tafsiri ya maneno aliyoyatoa, ndio yamesababisha kukamatwa na kushitakiwa kwa kutumia lugha za kichochezi.

Katika mashitaka yake, Lissu anadaiwa kuwa Juni 28, mwaka huu akiwa katika viwanja vya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, alitoa kauli za uchochezi kuwa “Mamlaka ya Serikali mbovu ni ya kidikteta uchwara inahitaji kupingwa na kila Mtanzania kwa nguvu zote, ‘huyu diktekta uchwara lazima apingwe kila sehemu’. Kama uongozi utafanywa na utawala wa kijinga nchi inaingia ndani ya giza nene.’’

Chanzo: Habarileo
 
nyie watu sijui mkoje kila siku mnampaisha Lissu BILA KUELEWA HIVI NYIE MKOJE,HUYU JAMAA MNAFANYA AWE TALK OF THE TZ AMEWAZIDI KILA IDARA,lisu.lisu,yaan msipomundika hamuuzi,duh hongera LISU
 
Ingekuwa vema hawa wapelelezi wapelekwe porini kibiti wafanye huo upelelez wao na wawakamate hao magaidi. Yani utadhani ni kama watoto wadogo mambo yao. Linchi maskini lakini wanapoteza nakuchezea hela ambazo ni za misaada kutoka kwa wahisani kufanya mambo ya kijingajinga
 
Chama cha makanikia wameamua kudeal na Lissu.
Baada ya kushindwa kibiti na Acacia sasa hiv ni mwendo na Lissu.
Teh teh teh
 
nyie watu sijui mkoje kila siku mnampaisha Lissu BILA KUELEWA HIVI NYIE MKOJE,HUYU JAMAA MNAFANYA AWE TALK OF THE TZ AMEWAZIDI KILA IDARA,lisu.lisu,yaan msipomundika hamuuzi,duh hongera LISU
Alafu kitu wasichokijua wengi ni kwamba Lisu analipwa Mamilioni ya pesa kwa kesi anazoishinda Serikaali.
 
Hivi dikteta uchwara ni tusi au wasifu wa kiongozi wa aina fulani?

Polisi wa Tanzania HAWANA AKILI, wakiambiwa kamata wanakamata bila ya kuhoji au kumuuliza ni kosa la mtu anayekamatwa. Katiba ya nchi imewapa wanasiasa nguvu kuliko wananchi na vyombo vya usalama havipo huru kufanya kazi zake kutokana na katiba kuwafanya wanasiasa kuwa na maamuzi ya kuhuni.
 
N

Ni kweli maana hata ukimuita hivyo baba yako atakupongeza sana!
mkuu, inategemeana na mental situation ya mtu na mtu.
kuna mtu anaweza kumuita baba yake kilaza, baba mtu anawweza asione ni big deal kwa kuwa huyo mtoto labda ni chizi tu!
 
Polisi wa Tanzania HAWANA AKILI, wakiambiwa kamata wanakamata bila ya kuhoji au kumuuliza ni kosa la mtu anayekamatwa. Katiba ya nchi imewapa wanasiasa nguvu kuliko wananchi na vyombo vya usalama havipo huru kufanya kazi zake kutokana na katiba kuwafanya wanasiasa kuwa na maamuzi ya kuhuni.
Ndio maana sishangai watendaji wengi wa serikali wanapostaafu huwa wanakuwa ombaomba na kuishi maisha magumu! Kama sikosei ni laana wanayokuwa nayo
 
MKUU wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai wa Wilaya (OCCID), Yustino Mgonja ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa alimkamata Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu baada ya Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalumu (ZCO), Camilius Wambura kumtaka afanye hivyo.

Mgonja ambaye ni shahidi wa nne katika kesi ya kutumia lugha ya uchochezi inayomkabili Lissu, alidai hayo jana mbele ya Hakimu Mkazi, Godfrey Mwambapa kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kusikilizwa.

Akiongozwa na Wakili Mwandamizi wa Serikali, Mutalemwa Kishenyi, shahidi huyo alidai kuwa Juni 28, mwaka jana, Wambura alimpa maelekezo ya kumkamata Lissu kwa kosa la kutoa lugha za uchochezi katika viwanja vya mahakama hiyo.

Alidai kuwa Juni 29 mwaka jana saa 7 mchana alienda nyumbani kwa Lissu maeneo ya Tegeta wilayani Kinondoni, ambapo alimkamata na kumfikisha katika ofisi ya ZCO na kumkabidhi.

“Nilipewa amri na ZCO nikukamate hivyo kwa mamlaka hayo bila kuwa na hati ya ukamataji naweza kukukamata; kwani makosa yoyote ya jinai unaruhusiwa kukamata bila kuwa na hati hiyo,” alidai Mhonja.

Pia alidai kuwa kumpinga Rais anapokosea sio kosa na kwamba tafsiri ya maneno aliyoyatoa, ndio yamesababisha kukamatwa na kushitakiwa kwa kutumia lugha za kichochezi.

Katika mashitaka yake, Lissu anadaiwa kuwa Juni 28, mwaka huu akiwa katika viwanja vya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, alitoa kauli za uchochezi kuwa “Mamlaka ya Serikali mbovu ni ya kidikteta uchwara inahitaji kupingwa na kila Mtanzania kwa nguvu zote, ‘huyu diktekta uchwara lazima apingwe kila sehemu’. Kama uongozi utafanywa na utawala wa kijinga nchi inaingia ndani ya giza nene.’’

Chanzo: Habarileo
Juni 28 mwaka huu...!!!? Terrible kama mashitaka yamefunguliwa kabla ya tarehe yenyewe kufika.
 
Hamna kesi hapo..

Ngoja huyo mpelelezi akikutana na maswali ya Lissu mwenyewe ataona boxer itakavyo mpwita.
 
MKUU wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai wa Wilaya (OCCID), Yustino Mgonja ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa alimkamata Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu baada ya Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalumu (ZCO), Camilius Wambura kumtaka afanye hivyo.

Mgonja ambaye ni shahidi wa nne katika kesi ya kutumia lugha ya uchochezi inayomkabili Lissu, alidai hayo jana mbele ya Hakimu Mkazi, Godfrey Mwambapa kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kusikilizwa.

Akiongozwa na Wakili Mwandamizi wa Serikali, Mutalemwa Kishenyi, shahidi huyo alidai kuwa Juni 28, mwaka jana, Wambura alimpa maelekezo ya kumkamata Lissu kwa kosa la kutoa lugha za uchochezi katika viwanja vya mahakama hiyo.

Alidai kuwa Juni 29 mwaka jana saa 7 mchana alienda nyumbani kwa Lissu maeneo ya Tegeta wilayani Kinondoni, ambapo alimkamata na kumfikisha katika ofisi ya ZCO na kumkabidhi.

“Nilipewa amri na ZCO nikukamate hivyo kwa mamlaka hayo bila kuwa na hati ya ukamataji naweza kukukamata; kwani makosa yoyote ya jinai unaruhusiwa kukamata bila kuwa na hati hiyo,” alidai Mhonja.

Pia alidai kuwa kumpinga Rais anapokosea sio kosa na kwamba tafsiri ya maneno aliyoyatoa, ndio yamesababisha kukamatwa na kushitakiwa kwa kutumia lugha za kichochezi.

Katika mashitaka yake, Lissu anadaiwa kuwa Juni 28, mwaka huu akiwa katika viwanja vya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, alitoa kauli za uchochezi kuwa “Mamlaka ya Serikali mbovu ni ya kidikteta uchwara inahitaji kupingwa na kila Mtanzania kwa nguvu zote, ‘huyu diktekta uchwara lazima apingwe kila sehemu’. Kama uongozi utafanywa na utawala wa kijinga nchi inaingia ndani ya giza nene.’’

Chanzo: Habarileo
Huyo Occid ukimfananisha na umbwa kiutendaji utakuwa umekosea nini!!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom