Mkuu wa Tume ya Uchaguzi ya Liberia ajiuzulu ! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkuu wa Tume ya Uchaguzi ya Liberia ajiuzulu !

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Yericko Nyerere, Oct 31, 2011.

 1. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #1
  Oct 31, 2011
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,240
  Likes Received: 3,782
  Trophy Points: 280
  ?Mkuu wa Tume ya Uchaguzi ya Liberia ambaye amekuwa akituhumiwa kumpendelea Rais Ellen Johnson Sirleaf amejiuzulu, siku chache kabla ya kufanyika duru ya pili ya uchaguzi wa rais nchini humo. James Fromayan anatuhumiwa na hasimu wa Rais Ellen Johnson Sirleaf, Winston Tubman anayegombea urais wa Liberia kwa tiketi ya chama cha CDC, kuwa anampendelea kiongozi huyo. Fromayan amesema kwamba ameamua kujiuzulu kwa ajili ya maslahi ya Liberia ili Tubman asipate kisingizo cha kutoshiriki katika kinyang'anyiro cha duru ya pili ya uchaguzi wa rais wa nchi hiyo.
  Wiki iliyopita mgombea huyo wa chama cha upinzani cha CDC alitishia kujiondoa katika duru ya pili ya uchaguzi wa rais itakayofanyika Novemba 8 iwapo uongozi wa Tume ya Uchaguzi hautabadilishwa.

  *

  *
   
Loading...