Mkuu wa Shule ya Msingi Kagecha jela miaka minne kwa kutoa zabuni kwa upendeleo

sinafungu

JF-Expert Member
Feb 13, 2010
1,527
865
MWALIMU Mkuu wa Shule ya Msingi Kagecha iliyopo Kowak, Kata ya Nyathorogo wilayani Rorya mkoani Mara, Mabogo Wambura (47), amehukumiwa kwenda jela miaka minne baada ya kupatikana na hatia ya matumizi mabaya ya madaraka kwa kutoa upendeleo wa zabuni wa ujenzi wa choo.

Amesomewa hukumu hiyo jana katika kesi ya matumizi mabaya ya madaraka mbele ya Hakimu wa Mahakama ya Wilaya Tarime, Amon Kahimba, iliyowasilishwa mahakamani hapo na Mwanasheria wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Mwinyi Yahaya.

Mshitakiwa alikiri kutoa zabuni kwa mshirika wake, Abich Yongo ya ujenzi wa choo cha shule hiyo iliyogharimu Sh milioni tatu bila kufuata utaratibu wa kamati za shule hiyo.

Awali, Mwendesha Mashitaka wa Takukuru, Yahaya alidai kuwa mshitakiwa Wambura akiwa Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kagecha, kati ya Desemba mosi na 30, mwaka 2014 alitoa zabuni bila kutangaza katika mbao za matangazo wa ujenzi wa choo cha shule hiyo kilichokuwa kimebomoka na hakufuata utaratibu hivyo alitumia madaraka vibaya.

Mshitakiwa alikiri kutoa zabuni hiyo bila kufuata utaratibu kama nakala ya mashitaka ilivyodai.

Mwalimu huyo aliiomba mahakama hiyo kumpa adhabu ndogo akidai kuwa na familia inayomtegemea wakiwemo mke na watoto wanaosoma kwani ndiye tegemeo la familia yake.

Mwanasheria wa Takukuru alipigilia msumari wa mwisho wa kuiomba mahakama kutoa adhabu kali kwa mshitakiwa ili iwe fundisho kwa wengine.

Hakimu Kahimba aliungana na upande wa mashitaka na kumhukumu kwenda jela miaka minne ili iwe fundisho kwa watu wengine wanaotumia vibaya madaraka.

Chanzo: Habari Leo
=====

Tazama mjadala wa habari hii ukisomwa ktk JamiiLeo
 
Hamna, labda kuna sababu nyingine. Acheni kuonea watu. Choo kimebomoka, wanafunzi wajisaidie wapi, labda mngesema choo hakikujengwa. Acheni kuonea watu.
 
MWALIMU Mkuu wa Shule ya Msingi Kagecha iliyopo Kowak, Kata ya Nyathorogo wilayani Rorya mkoani Mara, Mabogo Wambura (47), amehukumiwa kwenda jela miaka minne baada ya kupatikana na hatia ya matumizi mabaya ya madaraka kwa kutoa upendeleo wa zabuni wa ujenzi wa choo.

Amesomewa hukumu hiyo jana katika kesi ya matumizi mabaya ya madaraka mbele ya Hakimu wa Mahakama ya Wilaya Tarime, Amon Kahimba, iliyowasilishwa mahakamani hapo na Mwanasheria wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Mwinyi Yahaya.

Mshitakiwa alikiri kutoa zabuni kwa mshirika wake, Abich Yongo ya ujenzi wa choo cha shule hiyo iliyogharimu Sh milioni tatu bila kufuata utaratibu wa kamati za shule hiyo.

Awali, Mwendesha Mashitaka wa Takukuru, Yahaya alidai kuwa mshitakiwa Wambura akiwa Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kagecha, kati ya Desemba mosi na 30, mwaka 2014 alitoa zabuni bila kutangaza katika mbao za matangazo wa ujenzi wa choo cha shule hiyo kilichokuwa kimebomoka na hakufuata utaratibu hivyo alitumia madaraka vibaya.

Mshitakiwa alikiri kutoa zabuni hiyo bila kufuata utaratibu kama nakala ya mashitaka ilivyodai.

Mwalimu huyo aliiomba mahakama hiyo kumpa adhabu ndogo akidai kuwa na familia inayomtegemea wakiwemo mke na watoto wanaosoma kwani ndiye tegemeo la familia yake.

Mwanasheria wa Takukuru alipigilia msumari wa mwisho wa kuiomba mahakama kutoa adhabu kali kwa mshitakiwa ili iwe fundisho kwa wengine.

Hakimu Kahimba aliungana na upande wa mashitaka na kumhukumu kwenda jela miaka minne ili iwe fundisho kwa watu wengine wanaotumia vibaya madaraka.

Chanzo: Habari Leo
Vidagaaaaaaaaaaaaaa.
 
Yaani hii ndo kazi ya Takukuru, usanii mtupu.
Watuambie Chato na huko Ruangwa kama utaratibu ulifuatwa.
Nchi hii tumejaa mafaatani kabisa.a
 
Huyu Mkuu amefungwa miaka minne kwa matumizi mabaya ya ofisi, mzee Yoner na Mramba walifungwa siku kadhaa na kwenda kupiga deki now wanapeta uswazi.Je sheria zinatofautiana???
 
Mimi sina shida na hii adhabu. Lakini kwa maoni yangu, Hakimu angetusaidia waTanzania kama huyo Mwalimu Mkuu angeambiwa arudishe hela yetu kama adhabu! Sasa tunapata hasara mara mbili. Ya hela zilizojenga choo substandard na jukumu la kumlisha bure kwa miaka hiyo minne akiwa gerezani. Kwa umri wa 47 hawezi kufanya kazi ya maana.

High time adhabu zilenge kurudisha tulipoumizwa.

Kama akina Kitilya, Shose, na mafisadi wenzao..waambiwe warudishe mpunga wetu. Kama wakishindwa wafilisiwe.
 
Ni hilo tu au kuna jingine?

Kwani choo kimejengwa au hakijajengwa?

Hivi ameitia serikali hasara kiasi gani?

Ni bora wangemwambia azirudishe kuliko kwenda kumtesa mzee wa watu.

3m ndio mnamdhalilisha mwalimu hivyo wakati kuna watu wameitia hasara serikali mabilioni na bado mpaka leo wanatanua mtaani?

Kwa uonevu huu na dhuluma hizi bado kuna watu wanataka tuombe mvua?

Nyie watu Mungu hajalala wala hajachoka...........endeleeni tu hata farao na goliath hawakuishi milele
 
Back
Top Bottom