Mkuu wa Shule kizimbani kwa kumtomasa mwanafunzi

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
MWALIMU Mkuu wa Shule ya Sekondari St Thamos More Muchrine, Costantine Kirwanda (35) amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni kwa tuhuma za kumdhalilisha mwanafunzi wake.

Ilidawa mahakamani hapo kuwa mshitakiwa alimdhalilisha mwanafunzi huyo wa kidato cha tatu kwa kumshika kwenye matiti na kumbusu sehemu mbalimbali za mwili.

Mbele ya Hakimu Enediana Makabwa, Mwendesha Mashitaka Benedict Nyagabona alidai kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo Oktoba 20 mwaka huu saa 12 jioni katika eneo la shule.

Alidai kuwa kwa makusudi huku akijua kuwa kufanya hivyo ni kinyume cha sheria mshitakiwa alimshika mwanafunzi huyo (jina limehifadhiwa) anayesoma kwenye shule hiyo inayomilikiwa na Mkuu wa Kitivo cha Elimu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Profesa Justinian Galabawa.

Mshitakiwa alikana mashitaka na kurudishwa rumande hadi Januari mwakani kesi hiyo itakapotajwa tena.
 
alitomasa ? mwalimu kumlove dent wake inakuwaje karne hii , sijui tunakwenda wapi kimaadili. du hata hivyo wanafunzi wenyewe wa kike wanavyopenda kupozi kimatamanio hadi kuwaghiribu walimu wao , kaaazi kweli kweli
 
Back
Top Bottom