Mkuu wa shule anapomlinda mwalimu anayejishughulisha na vitendo vya kishoga kwa wanafunzi

mbeyaman

Member
Sep 28, 2013
97
28
Mkuu wa shule moja mkoa wa Pwani wilaya ya Bagamoyo kwa muda mrefu amekua akishindwa kumchukulia hatua za kinidhamu mwalimu mmoja wa kiume mwenye tabia za kuwadhalilisha wanafunzi wa kiume kwa kuwaita ofisini kwake na kuwafanyia vitendo vya aibu. Shule hiyo ni ya sekondari iliyoanzishwa kwa nguvu za wananchi wakishirikiana na mbunge wao pamoja na diwani.

Shule hiyo ya kataa inayoanzia na jina la DU---- ipo km 5 kutoka mji wa Bagamoyo. Mkuu huyo mwenye jina linalofanana na Mkwe herufi za mwanzo alitokea katika shule moja yenye jina la wilaya hiyo na kuhamishiwa hapo kama mkuu wa shule baada ya mkuu wa mwanzo kustaafu kazi. Shule hiyo ipo kando ya barabara iendayo Dar es Salaam karibu na checkpoint ya vikosi mbalimbali vya wanausalama.

Kwa nyakati tofauti wanafunzi hao wamekuwa wakimweleza mkuu wa shule tabia za mwalimu huyo lakini amekuwa akimkinga kifua kwa kumtetea kwa kuwa ni swahiba wake. '' Tumekaa kwenye vikao vya madarasa na walimu wetu wa madarasa tukilalamikia tabia mbaya ya mwalimu huyo ya kutufanyia vitendo vya udhalilishaji na kupeleka muhtasari wa vikao kwa mkuu wa shule lakini hakuna kinachofanyika''. Alisikika mwanafunzi mmoja wa kiume akilalamikia tabia hiyo mbaya ya mwalimu huyo inayoenda kinyume na maadili ya kazi yake ya ualimu.

''Mwalimu huyo amekuwa akiwaadhibu hovyo wanafunzi wa kiume ambao wameonesha kupinga tabia zake mbaya. ''Mimi mwenyewe aliniita ofisini akafunga mlango kisha akaanza kunigusagusa sehemu za siri''. Alisema mwanafunzi mmoja wa kiume.

'Ni vyema serikali ichukue hatua mara moja kwani hivi vitendo anavyofanya mwalimu huyu ni vya aibu.
 
wewe kama mwananchi umechukua hatua zipi??
kama tuhuma hizi ni za kweli kwanini unalificha jina la shule

sasa usalama utaanzaje kuchukua hatua kama wewe utoi ushirikiano????
 
mwalimu Wa Dunda sec aliyehamia toka Bagamoyo sec huyo.si naskiaga wanafunzi Wa Dunda ni manunda kwanin wasimshughulikie yeye?halafu kwanin wakiitwa wanaenda?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom