Mkuu wa Polisi wilaya ya Geita, unamjua Trump wa kituo cha Nyarugusu?

Dragon Kulala

Member
Jan 24, 2020
53
125
Asalaam aleikum mkubwa wa mapolisi Wilaya yetu ya Geita.Hivi bwana mkubwa huwa unatembelea vituo vyako vya polisi na kuzungumza na raia japo wawili watatu?Kama hufanyi hivyo, basi nikuombe uanze Ziara hizo na ikikupendeza uanzie huku Nyarugusu.

Hapa mzee kuna mbabe mmoja anajiita TRAMP!Sijui alijiita jina hilo kwa sifa zipi zinazomlinganisha na Trump tunayemfahamu na kumsikiliza kila leo kwenye vyombo vya habari, lakini itoshe kusema huyu Trump wa kuchonga wa hapa Nyarugusu ni mbabe na katili kupindukia.

Nimesoma uzi mmoja katika uwanja huu unaomwomba bosi mmoja kuwachunguza maaskari wawili,ikiwezekana bwana wakubwa fanyeni hivyo mapema ili mtuondolee manyanyaso tunayoyapata sisi raia wa Nyarugusu kutoka kwa wababe hawa wakiongozwa na AFANDE TRUMP.

Yapo maonevu mengi tunayofanyiwa hasa hasa vijana, itoshe kukueleza kwamba ukifanya ziara na kuongea na sisi Wananchi utayapata mengi ili ujue jinsi gani ya kusafisha uozo huu.

Machache kati ya manyanyaso yanayofanyika hapa Nyarugusu ni Kubambikiwa kesi.Bwana huyu mkipishana kauli sehemu yoyote ile,utaambiwa umetorosha wahalifu,umewazuia polisi kufanya kazi,umeiba kirungu cha polisi au ulitaka kumnyang'anya siraha nk.

Utapigwa, utaswekwa ndani na kutoka ndani ni shughuli mpaka hapo utakapokubali kutoboka, la sivyo gereza linakuhusu.

Watu wanapelekwa Gerezani kwa kesi za kupewa eti ni uzembe na uzurulaji.Wakati Rais anataka watu wapungue magerezani, huku Trump na washirika wake wanapingana na kauli hiyo na kuwasweka watu huko kwa kasi waitakayo, hii si sawa hata kidogo.

Askari wanawajibu wa kulinda raia na mali zao na kuhakikisha amani na utulivu katika jamii, Trump huyu wa Nyarugusu na washirika wake wanakuwa wa kwanza kuvuruga amani yetu, tutafika kwa mfumo huu?Raia ukiwa na tatizo polisi, umkute Trump huyu unatamani uahirishe tu kulikoni ufike na kufokewa, kutukanwa na pengine kuswekwa ndani.

Nadhani kwa ubabe wa huyu jamaa, anaweza kukuzulia kesi ya kutaka kuvamia kituo, hana dogo!Chonde chonde wahusika tunusuru raia na kero hizi zinazotuandama.Inafika mahali tunajiuliza, huyu ndiye mkuu wa kituo au ni zaidi ya mkuu wa kituo?

Jeuri hii anaipata wapi?Nani yuko nyuma yake?Ameshindikana kweli?Tazameni jambo hili kwa mapana yake,fikeni mzungumze na wananchi ili mpate mengi zaidi na msaidie kuyatatua

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Loftins

JF-Expert Member
Oct 1, 2017
8,549
2,000
Uzi umo humu tayari kwanza umeanza na salamu ya mapepo ushindweee katika jina la Yesu
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom