Mkuu wa Polisi wa Hai alishirikiana na Ole Sabaya kwenye Uhalifu, naye akamatwe haraka sana

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
116,463
215,272
Iko wazi kwamba OCD wa Hai alinyamazia unyama wote ulioambatana na uchafu wa kutia aibu wa Mhalifu Ole Sabaya, kwa vyovyote vile Mtu mwenye mamlaka ya kuzuia Uhalifu anapounyamazia ili uendelee kutendwa huyu naye ni kwamba anashiriki uhalifu huo, anapaswa kukamatwa na kuunganishwa kwenye kesi husika.

Ujumbe huu umfikie Simon Sirro ambaye ndie IGP wa Polisi Tanzania, huwezi kuendelea na OCD wa namna hii na bado ukadhani utaaminiwa. Jeshi letu la Polisi bado lina watu wengi sana waadilifu na wanaojua majukumu yao vizuri sana wanaoweza kuchukua nafasi ya huyo mhalifu.

 
Mzee Sirro ameshachoka na kuezeeeka sasa hivi anatafutia tu mabinti zxake wachumba at least apate Wajukuu wa kucheza nao. Yaani bora liende tu, nina appoitnment nae keshokutwa, kuna jambo nataka nikamshirikishe yule Mzee wa watu wa ki RC.
 
Unachotaka kusema ni sawa na ghorofa likidondoka, wakamatwe vibarua waliomimina zege badala ya kumkamata injinia.
 
17 Reactions
Reply
Back
Top Bottom