Mkuu wa Polisi aua ndugu zake watatu, naye ajiua | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkuu wa Polisi aua ndugu zake watatu, naye ajiua

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Jan 24, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jan 24, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  Ni Mkuu wa Kituo cha Polisi, ndugu zake ni maofisa waandamizi serikalini

  Kaimu Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Magomeni, jijini Dar es Salaam, Inspekta Msaidizi, Nicodemus Senge (43), amejimaliza kwa kujipiga risasi baada ya kuwaua ndugu zake watatu wa familia moja.

  Kamanda wa Polisi mkoani Pwani, Ernest Mangu, alisema tukio hilo lilitokea juzi saa 2:00 usiku, katika kitongoji cha Bamba Kongowe, mkoani Pwani.

  Kamanda Mangu alisema Inspekta Senge, alichukua hatua hiyo ya kuwaua nduguze watatu kisha naye kijiua kutokana na kutoelewana baina yao katika kikao kilichohusu mgogoro wa ardhi ya familia hiyo.

  Alisema siku ya tukio hilo, wanafamilia hao ambao ni wazaliwa wa Mkoa wa Singida na wanaofanya shughuli zao katika mikoa ya Pwani, Dar es Salaam na Dodoma, walikubalina kukutana kwa ndugu yao anayeishi Kongowe mjini Kibaha, Pendael Senge (56), ili wafanye suluhu ya mgogoro huo wa ardhi uliodumu kwa muda mrefu huko kwao mkoani Singida.

  Kamanda Mangu alimtaja aliyekuwa mlalamikaji katika mgogoro huo kuwa ni Andrew Michael, akidai kuwa sehemu yake ya ardhi imechukuliwa na mmoja wa ndugu ambaye hakujulikana jina lake mara moja.

  “Walipokuwa wakiendelea na kikao katika nyumba ya ndugu yao huyo ambaye ni Mratibu wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (Tasaf), wa mikoa ya Pwani na Dar es Salaam, ilitokea hali ya kutoelewana kati ya wanandugu hao ambapo walianza kurushiana maneno na hatimaye risasi kurushwa,” alisema Kamanda Mangu.

  Alifafanua kuwa risasi hizo zilipigwa na Inspekta Senge kwa kutumia bastola ya Jeshi la Polisi aliyokuwa akiitumia wakati akiwa kazini kwa kuwafyatulia ndugu zake watatu na baadaye kujimalizia yeye mwenyewe.

  Aliwataja waliouawa kuwa ni Andrew Michael (30) ambaye alikuwa ni mfanyabiashara wa Kiwalani, Nkolo Senge (49), mfanyakazi wa Ofisi ya Bunge Dar es Salaam na Mratibu wa Tasaf mkoani Pwani, Pendael (53).

  Alisema miili ya marehemu wote wanne imehifadhiwa katika Hospitali Teule ya Tumbi mkoani Pwani.
  Kwa upande wa Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Charles Kenyella, alithibitisha pia kumfahamu Inspekta Senge ambaye alisema juzi saa 12:00 jioni alikuwa kazini kituoni kwake Magomeni.

  Kamanda mangu alisema kutokana na nafasi aliyokuwa nayo katika kikosi cha kupambana na uhalifu mkoani kwake, ililazimika kuwa na silaha wakati wote ili kumudu utendaji kazi zake.

  "Nimepokea taarifa hizo kwa mshtuko mkubwa kwa kuwa Nicodemus, alikuwa muadilifu kazini na hata siku ya tukio majira ya saa 12:00 alikuwa kituoni kwake kabla ya kwenda kufanya mauaji hayo na kujimaliza mwenyewe...mkoa wangu umeguswa sana na tukio hilo hatujui ni kitu gani kilimpata mpaka akachukua hatua hiyo. Naipa pole familia yake ambayo walimtegemea kwa hali na mali pamoja na ndugu zake waliobakia," alisema Kamanda Kenyella.

  Alifafanua kuwa kwa sasa mkoa wake unasubiri maelekezo ya msiba wa ofisa huyo utakuwa wapi kwa kuwa makazi yake yalikuwa nyumba za Polisi za Msimbazi jijini Dar es Salaam.

  "Suala la msiba kuwa wapi sisi kama jeshi hatuna mamlaka kwa kuwa wana familia wapo watatoa maelekezo ufanyike wapi kama ni Msimbazi au Kibaha... kama watasafirisha au kuzika hapa, tunasubiri maelekezo yao," alisema Kamanda Kenyella.

  Kamanda Kenyella alisema silaha iliyotumika kwenye tukio hilo ni mali ya Jeshi la Polisi ambayo Nicodemus aliitumia katika kupambana na wahalifu wakati wa uhai wake na kwamba hakuna wa kutuhumiwa wala wa kumhoji kwa kuwa mhusika ameshatangulia mbele za haki.

  Alisema hakuna ubishi kuwa silaha hiyo imetumika isivyo halali lakini kila kitu kimeishia hapo, cha msingi ni familia kuwa na subira katika kipindi hiki kigumu walichonacho kwa kupoteza ndugu wanne kwa wakati mmoja.
  CHANZO: NIPASHE
   
 2. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #2
  Jan 24, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,492
  Likes Received: 5,593
  Trophy Points: 280
  Askari huchukua maamuzi magumu sana wakati mwingine.
  Jeshi linahitaji mtizamo mpya!
   
 3. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #3
  Jan 24, 2012
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 9,003
  Likes Received: 585
  Trophy Points: 280
  jina la ukoo la huyo inspekta tu linajieleza ni mtu wa aina gani.
   
Loading...