Comi
JF-Expert Member
- Oct 2, 2011
- 3,328
- 955
Sasa ni takribani wiki moja na siku toka mawaziri watatu kusimamishwa na mmoja kujiuzulu kutokana na ripoti ya tokomeza majangili. Katika mawaziri hao kuna ambao wananchi walishawatilia shaka katika utendaji wao wa kuwahudumia wananchi. Kuna mawaziri wengine ambao kwa namna moja au nyingine shutma na hata viongozi waandamizi katika chama chao wamewatolea uvivu na kuwaambia kuwa ni mizigo na hiyo ni kabla ya rais kutengua uwaziri wa hao mawaziri wanne.
Swali langu ni kwamba, je! Rais hadi mda huu hana mawaziri wengine ambao tayari alishawafikiria? Au bado yuko mapumzikoni kama mwenzake Pinda aliyesema hawezi kuongea kwa mda huu. Au hajaona mbunge yeyote anayekidhi vigezo vya uwaziri?
Naomba kujuzwa kwa nini hakuna taarifa yoyote kuhusu swala la mawaziri.