Mkuu wa nchi amewafukuza, je amewafikisha mahakamani?

Mwiba

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
7,607
1,745
Kifahamu kichwa ,kichwa cha habari kwa kuona ndani, inawezekana kwa Mkuu wa nchi kuonekana akifukuza waliochini yake kwa umbali mkubwa ?

Naomba tujadili hoja ,kwani ninachokiona kikifanywa na Mkuu ni aibu kwa Taifa,au pengine alikuwa akionyesha mfano kwa wale aliowachagua na kuwakopesha nafasi za UWAZIRI,kwa maana ikiwa itatokea kwa aliyoyafagia basi wa kumuwajibisha si mwanakijiji kule shambani kwa bibi bali ni msimamizi aliemkabidhi kazi ya kulisimamia shamba na waliomo ndani ya shamba.

Kama nia ni kuonyesha njia basi waliosimamishwa waliofukuzwa isingewakuta peke yao bali wale waliopewa dhamana nao wangeunganishwa kwani uzembe wao wa kuzembea ndio uliopelekea wakulima kulewa chakari na kuchakarika,na kulisababishia shamba la bibi kupoteza mazao.

Amewafukuza amewafikisha mahakamani ? Au ndio imetoka na show kumalizika ,mahakamani kuna mambo mazito yanaweza kuibuka na kusababisha wasiokamatika watake kukamatwa,so bora tuwafukuze tu ,huku ikisemwa uchunguzi unaendelea.

Ndio nikasema Mkuu wa nchi kumfukuza mwanakijiji ni uonevu au mnaonaje ?
 
Mkuu mi siamini kama hawa wanakijiji walifanya huu uzembe makusudi au walikua na uwezo wa kufanya haya mambo. Wangewezaje kule shambani kuna manyapara ya kila aina. Kwa kweli ni uonevu tu kwa wanakijiji hawa.
 
Mwanakijiji siku zote ndie mlaji wa mwisho..
Manyampara wao pia hua wanafuata maagizo ya mwenye shamba..

upande wangu sina ushauri NAangalia show itakavyopelekwaa
 
Kwa ujumla kuna watu waliotoa kibali cha nini kifanyike pale bandarini. Kuna watu wenye nyadhifa waliotoa vibali ili kila kikichofanyika lakini leo wanaobanwa ni wale waliotekeleza maelekezo na wanapata gharama kubwa sana kwa kutekeleza maelekezo ya wenye mamlaka halali.
 
MIE NAONA KAZI HIYO ANAIELEWA TUWE WAVUMILIVU NA KUMUOMBEA ATIMIZE AZMA YAKE
 
Tanzania chini ya CCM siyo nchi ya kujivunia kabisa!

Yeye mwenyewe angeanza kujfukuza. Huyu jamaa angekuwa katika nchi za wanaojielea kamwe asingekuwa Kwenye iyo nafas yakufukuza watu ilhali yeye hajifukuzi yani ni boriti. Angekuwa nyuma ya nondo.
 
awezi kuwafikisha mahakamani kwani DPP na TAKUKURU hizi kesi hawajawahi kuzishinda mpaka hapo watakapokuwa na uwezo wa kuwashitaki na wakapatikana na makosa, na ni pale mawakili wa tanzania watajaa uzalendo kuweka maslahi yao pembeni.
 
Mkuu mi siamini kama hawa wanakijiji walifanya huu uzembe makusudi au walikua na uwezo wa kufanya haya mambo. Wangewezaje kule shambani kuna manyapara ya kila aina. Kwa kweli ni uonevu tu kwa wanakijiji hawa.

Ninaamini Mkuu wa kaya anajua wahusika wakuu ni akina nani. Bila shaka kaanza na wakulima ili atakapowakashughulikia wasimamizi na waliowatuma wasimamizi ionekane kuwa sio chuki binafsi bali ni kwa kuwa wakubwa hao wametajwa na wakulima. Ila huo ni unafiki wa hali ya juu. Kama kweli tuna nia ya dhati, basi kwa kadiri ya uhusika wao, hata hao wakubwa na wasimamizi wote wangesombwa na kufikishwa katika mkono wa sharia wakati mali na utajiri wao vikichunguzwa na kutaifishwa.
 
Tunaanzia chini kwani wanakijii ndio watendaji, wanakijiji wanatakiwa wawe na msimamo na sio kufuata yanayosemwa na wakubwa zao kama wanaona siyo sahihi. Lowassa aliondoka serekalini kwa sababu ya kutie maelezo ya boss wake JK.
 
Mkuu kuanza na wanakijij sio sahihi.ww angalia Jana makontena yamegundulika yamepitishwa kinyemela amekamata wanakijij na wengine bado wanatafutwa.ila wale wamepewa Sikh kadhaa walipe kodi
 
Back
Top Bottom