Ambitious
JF-Expert Member
- Dec 26, 2011
- 2,143
- 877
Katika harakati za kuhakikisha kwamba wanaendana na kasi ya Mhesimiwa Rais,wakuu wa mikoa wamekuwa wakitembelea baadhi ya maofisi na viwanda.Mkuu wa Mkoa wa Tanga Bi.Mwantumu Maiza amekuwa akitembelea viwanda na ofisi mbalimbali ili kujionea ufanisi wake.
Miongoni mwa viwanda alivyotembelea katika ziara zake ni viwanda vya Mamujee na Afritex Ltd akiongozana na msururu wa maafisa wa serikali kuanzia terehe 5
na 6 January.
Lakini katika hali ya kushangaza ameshindwa kusikiliza madai ya wafanyakazi ambao wamekuwa wakifanya kazi ngumu katika viwanda hivi na kulipwa ujira mdogo wa chini Tsh.5000 kwa siku.Alichojibu ni kwamba ''Wenzenu wako getini wamekosa kuingia kupata kibarua cha siku nyie mmepata nafasi ya kuingia mnalalamika nini?'' pia aliwaambia ''kiwango kidogo cha elimu ndio kinachangia kulipwa kwenu mshahara mnaolipwa''
Hivi kiongozi hata kama hauna suluhisho kwa nini usitafute kauli nzuri za kuwajibu wananchi? Je,ni jeuri ya kukalia hizo VX V8 na kusahau wananchi wa kawaida?
Utendaji wa huyu mama unapaswa kuangaliwa kwa kweli amekuwa akitoa maamuzi yasiyo ya hekima ikiwemo sakata la kuhamisha kituo cha mabasi kukileta mjini kipindi cha uchaguzi ili kuwaridhisha wananchi na kukirudisha tena kwenye kituo rasmi cha Kange(nje kidogo ya jiji la Tanga) baada ya uchaguzi na hivyo kusababisha kero zisizo na msingi.
Kauli mbiu ya ''hapa kazi tu'' inaelekea kumshinda huyu mama.