Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Evarist Ndikilo 'Ageuka Mbogo' baada ya kukabidhi zawadi hewa Mei Mosi

Babu wa Kambo

JF-Expert Member
May 2, 2016
559
808
1.JPG

MKUU wa Mkoa wa Pwani, Evarist Ndikilo ameagiza ifikapo leo, wakurugenzi wa halmashauri za mkoa huo, wawe wamewapa zawadi zao watumishi bora wa mwaka huu baada ya kubaini walitoa zawadi hewa kwenye sherehe za Mei Mosi.

Ameagiza pia Ofisi ya Katibu Tawala Mkoa wa Pwani pamoja na mkurugenzi wa Shirika la Elimu Kibaha, nao kutoa zawadi ya fedha kwa wafanyakazi waliofanya vizuri kwenye vitengo vyao, badala ya kuwapa vyeti pekee.

Akizungumza juzi kwenye sherehe za Mei Mosi zilizofanyika kimkoa wilayani Mkuranga, Ndikilo alitoa siku tatu zinazoisha leo, taasisi hizo ziwe zimetekeleza agizo hilo. Alisema walichofanya ni masihara na yeye hayuko tayari kufanyiwa mzaha katika suala hilo, lililoandaliwa kwa muda mrefu.

“Katika risala ya Shirikisho la Vyama Huru vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) Mkoa wa Pwani walilalamika kuwa kumekuwa na tabia ya baadhi ya waajiri kuwakopa zawadi za fedha watumishi wanaofanya vizuri kama motisha,” alisema.

Aliendelea, “Lakini kwa hali hii siwezi kukubaliana nalo, nawapa siku tatu muwe mmewalipa watumishi hao vinginevyo atakayeshindwa aje ofisini kwangu akutane na adhabu niliyoiandaa.”
Alisema hawezi kuvumilia watu wazembe wanaofanya dharau kwenye mambo mazito na kwamba atachukua hatua kali kwa halmashauri ambazo zitashindwa kutoa zawadi hizo kwani zingine zimetoa kwa nini wengine washindwe.

“Mimi siyo mtani wenu, wala si saizi yenu, haiwezekani mniite nije kutoa zawadi hewa, ndo maana hatua zikichukuliwa za kinidhamu mnasema mnaonewa, ikifika Jumatano muwe mmeshawapa zawadi zao wahusika, huu ni mzaha umepitiliza kiwango anayedhani tunatania aendelee aone,” alisema Ndikilo.

Licha ya ofisi ya Katibu Tawala pamoja na Shirika la Elimu Kibaha, taasisi nyingine zilizotakiwa kutekeleza agizo ni Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo, Halmashauri ya Mji Kibaha na Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji.

“Hatutaniani hapa,huu ni mzaha uliopitiliza kiwango,.ujumbe umefika.Namna hii mnakatisha tamaa watumishi kwa kudai kuwa mchakato bado ni jambo ambalo halijanifurahisha na nisingependa hali hii ijitokeze tena,” alisema Ndikilo.

Awali, akisoma risala ya Tucta, Amini Msambwa alisema kuwa wafanyakazi wana haki ya kutimiziwa haki zao za msingi na siyo lazima zipatikane kwa shinikizo la maandamano, migomo na hata kufungia nje waajiri.

Msambwa alisema kuwa moja ya changamoto ni baadhi ya wawekezaji wa nje na wa ndani, kuwanyima fursa wafanyakazi kujiunga na vyama vyao sehemu za kazi, ambayo ni haki yao ya kisheria na kwa kuzingatia kauli mbiu ya mwaka huu ya Dhana ya Mabadiliko ilenge kuinua hali za wafanyakazi.
 
Tanzania ya hewa, kila kitu hewa wafanyakazi hewa,zawadi hewa,halmadhauri za Pwani nao walifikiri RC wao ni hewa wakampa atoe zawadi hewa.
 
Hata hii nchi inawezekana ni hewa haipo duniani,tunaishi kwenye hewa.
 
Mimi nadhani sielewi,hivi hii nchi tulikuwa tunaishi vipi?any way hii ni transition period ,tutafika tu katika kuishi kama inavyotakiwa.Maana inaonekana kila sehemu ilikuwa ni ujanja ujanja tu,haya tena zawadi hewa,real zawadi zililiwa na wakurungezi ama?
 
Hata hii nchi inawezekana ni hewa haipo duniani,tunaishi kwenye hewa.

Hapana nchi ipo,tatizo lipo kwa wananchi.Taifa hili linapaswa kutunukiwa tuzo za kimataifa kwa kuwa na watu vilaza.Ni Tanzania pekee ambako mtu anaweza kujitoa ufahamu kwa kushangilia maigizo ya serikali huku maigizo hayo yakimuumiza mwenyewe.

Serikali ilitoa tamko la kisiasa lililokosa weledi,tamko lililosemekana lilikuwa limesheheni sifa za uzito wa juu,tamko la kushusha bei ya sukari hadi kufikia sh.1800/kg.Leo hii hapa Kahama bei ya sukari kwenye maduka ni sh.2500/kg,uko wapi utekelezaji wa tamko hilo kama bei ya sukari imepaa maradafu?

Serikali ilijinasibu kutoa Elimu bure,Mh.Rais alizunguka nchi nzima akiinadi Sera ya Elimu bure,lakini leo hii Elimu bure ni Sera ya hovyo kabisa iliyolirudisha Taifa letu miaka mingi nyuma.Yaani wanafunzi ambao hapo awali kwa kushirikiana na wazazi wao walikuwa wanafanya Mitihani iliyochapishwa,leo hii wanafanya Mitihani kwa kuandikiwa maswali ubaoni?

Hili limetokea Kata ya Igwamanoni,Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu Kahama.Wanafunzi wa Drs VII wamefanya Mitihani wa mock kwa kuandikiwa maswali ubaoni.Katika hali hiyo lengo la kufanya Mitihani hiyo litafikiwa?

Wanasiasa wetu wanaweza kucheza na mambo mengine,lakini kitendo cha kuchezea Elimu ya watoto wetu huku wao wakitumia mabilioni ya mshahara,posho na malupulupu yatokanayo Na kodi zetu kusomesha watoto wao shule bora hilo halikubariki.Haiwezekani watuandalie Sera ambazo wao wenyewe hawaziamini,sisi watuaminishe kuwa wanafanya hayo ili kulipeleka Taifa kwenye kipato cha kati,kipato cha kati wakati sehemu kubwa ya Taifa linagubikwa na upofu wa kielimu?

Tunawaomba viongozi wetu wazipitie upya Sera Na ahadi zote walizozitoa wakati wa uchaguzi,waondoe zile zote zilizokuwa Na lengo la kuwahadaa wananchi ili wapate vyeo,badala yake wajikite katika kuwahimiza Watanzania watambue wajibu wao kwa Taifa,badala ya serikali kujitwisha zigo la huduma bure huku haina uwezo wa kutoa huduma za bure.
 
1.JPG

MKUU wa Mkoa wa Pwani, Evarist Ndikilo ameagiza ifikapo leo, wakurugenzi wa halmashauri za mkoa huo, wawe wamewapa zawadi zao watumishi bora wa mwaka huu baada ya kubaini walitoa zawadi hewa kwenye sherehe za Mei Mosi.

Ameagiza pia Ofisi ya Katibu Tawala Mkoa wa Pwani pamoja na mkurugenzi wa Shirika la Elimu Kibaha, nao kutoa zawadi ya fedha kwa wafanyakazi waliofanya vizuri kwenye vitengo vyao, badala ya kuwapa vyeti pekee.

Akizungumza juzi kwenye sherehe za Mei Mosi zilizofanyika kimkoa wilayani Mkuranga, Ndikilo alitoa siku tatu zinazoisha leo, taasisi hizo ziwe zimetekeleza agizo hilo. Alisema walichofanya ni masihara na yeye hayuko tayari kufanyiwa mzaha katika suala hilo, lililoandaliwa kwa muda mrefu.

“Katika risala ya Shirikisho la Vyama Huru vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) Mkoa wa Pwani walilalamika kuwa kumekuwa na tabia ya baadhi ya waajiri kuwakopa zawadi za fedha watumishi wanaofanya vizuri kama motisha,” alisema.

Aliendelea, “Lakini kwa hali hii siwezi kukubaliana nalo, nawapa siku tatu muwe mmewalipa watumishi hao vinginevyo atakayeshindwa aje ofisini kwangu akutane na adhabu niliyoiandaa.”
Alisema hawezi kuvumilia watu wazembe wanaofanya dharau kwenye mambo mazito na kwamba atachukua hatua kali kwa halmashauri ambazo zitashindwa kutoa zawadi hizo kwani zingine zimetoa kwa nini wengine washindwe.

“Mimi siyo mtani wenu, wala si saizi yenu, haiwezekani mniite nije kutoa zawadi hewa, ndo maana hatua zikichukuliwa za kinidhamu mnasema mnaonewa, ikifika Jumatano muwe mmeshawapa zawadi zao wahusika, huu ni mzaha umepitiliza kiwango anayedhani tunatania aendelee aone,” alisema Ndikilo.

Licha ya ofisi ya Katibu Tawala pamoja na Shirika la Elimu Kibaha, taasisi nyingine zilizotakiwa kutekeleza agizo ni Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo, Halmashauri ya Mji Kibaha na Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji.

“Hatutaniani hapa,huu ni mzaha uliopitiliza kiwango,.ujumbe umefika.Namna hii mnakatisha tamaa watumishi kwa kudai kuwa mchakato bado ni jambo ambalo halijanifurahisha na nisingependa hali hii ijitokeze tena,” alisema Ndikilo.

Awali, akisoma risala ya Tucta, Amini Msambwa alisema kuwa wafanyakazi wana haki ya kutimiziwa haki zao za msingi na siyo lazima zipatikane kwa shinikizo la maandamano, migomo na hata kufungia nje waajiri.

Msambwa alisema kuwa moja ya changamoto ni baadhi ya wawekezaji wa nje na wa ndani, kuwanyima fursa wafanyakazi kujiunga na vyama vyao sehemu za kazi, ambayo ni haki yao ya kisheria na kwa kuzingatia kauli mbiu ya mwaka huu ya Dhana ya Mabadiliko ilenge kuinua hali za wafanyakazi.
hahahaha naangua kicheko yaani watanzania tumekuwa wezi sugu khaaaaaaaaa sasa hii ni nini
 
Hewa, hewa, hewa! Badala ya elimu, elimu, elimu. Hebu tuambiane ukweli juu ya elimu bure kwa karne hii kweli? Ni nchi gani duniani inapractice hii kitu na imefanikiwaje na uchumi wako unalingana na wa kwetu? Kupeleka shs. 200/=kwa mwezi kwa kila mwanafunzi wa shule ya msingi ndio bure. Hii utaifanyia nini kwa mwezi? Hebu vaa viatu vya mwl mkuu uiendeshe hii shule ya msingi ambayo kila kitu unanunua kisha useme utafanyaje? Wazazi nao ni walewale wa kila kitu hureeeeh kama siyo heko? Wakija kushtuka watoto wao wanabaki nao majumbani wanachunga mifugo kwa kutawaliwa na watoto wa waliowapa elimu bure bwerere! Amkeni, elimu bure haipo sayari hii rudini kuchangia muwakomboe watoto wenu kwenye hii kitu. Vinginevyo mtajutia na kulaumiwa na watoto hawa.
 
Ni upuuzi kuiita Tanzania hewa,kama wewe ni hewa kiri wewe ni hewa usituhusishe wote kuwa hewa.
 
Tanzania HEWA!! Wafanyakazi HEWA walitoa zawadi HEWA kwa wafanyakzi HEWA kupitia kwa mkuu waliyedhani ni HEWA ili atoe zawadi HEWA kwa wafanyakazi HEWA!!!
 
Back
Top Bottom