Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, tusaidie wakazi wa Luchelele. Anzia kwetu kutatua kero zetu

Moja ya tabia mbaua niliyoiona Mwanza ni daladala kubadilisha route hovyo hasa nyakati za jion na trafki wapo. Sijui huwa hawajui au. ndio tusemeje, yaani ikifika jioni gari zote za Malimbe zinaenda Butimba tena wanatangazia abiria bila aibu. Chalamila hajawahi nianangusha akipata taarifa naamini hii tabia itakima.
 
Nianze kwa kukupongeza kuweza kuteuliwa kuwa mkuu wa mkoa wetu. Kwa niaba ya wakazi wa Luchelele wilaya ya Nyamagana nawasilisha kero zetu zinazotusibu kwa muda mrefu.

Kwanza, ubovu wa barabara. Barabara yetu ni mbovu sana,ina mashimo na makorongo huwezi kuamini kuwa hii barabara ipo sehemu ya jiji. Pamoja na ubovu huo unaosababisha magari kupita kwa shida pia kuna kero ya vumbi. Kuna msururu wa malori yanayokuja kuchukua udongo wa moramu ambapo wanashindwa hata kumwagilia maji.

Pili, usafiri. Kuna shida sana ya usafiri kwa sisi wakazi Luchelele inayopelekea matumizi makubwa ya pesa kwa kupanda bodaboda. Sasa 12 jioni ikikukuta mjini hesabu maumivu. Zile Hiace za Luchelele zinabadili route na nyingine zinaishia Malimbe - SAUT na wanawatangazia abiria pale stendi ya Igombe bila kuogopa, panakuwepo hakuna askari pale ya kufuatilia hizi hujuma.

Vilevile, zile hiace za route ya Luchelele- Usagara haziendi tena kule,zimeajianzishia route ya Luchelele- Kona ya Nyegezi kwa siku nzima na nauli wanatoza ile ile, cha kushangaza hakuna polisi wanaowachukulia hatua wakati wanageuzia barabara kuu na wenyewe wakiona na ikifika saa 12 jioni wanapeleka abiria mjini na kurudi Buhongwa.

Tatu,huduma ya maji na afya. Kuna mgao mkubwa sana wa maji na sehemu nyingine mabomba yapo kama mapambo,maji hayatoki kabisa,mabomba yanaharibika na hayatengenezwi kwa wakati. Kuhusu afya, kata nzima hakuna kituo cha afya.

Kwa machache ni hayo tu, mengine nipende kukukaribisha uje ujionee mwenyewe.

Kwa msisitizo zaidi ni kwamba masuala mawili ya mwanzo yapo ndani ya uwezo wako kabisa ni suala la kutoa amri tu kwa mfano kwenye suala la ubovu wa barabara ni kama TARURA hawana fedha za matengenezo basi ni kuwaambia wenye kampuni iyochimba moramu huku kuhakikisha wanaziba hayo mashimo maana ndo waharibifu wakubwa wa barabara na miundombinu ya maji.

Hiyo moramu wanaipitisha tu bila kutengeneza wanapoharibu. Pia kwenye suala la kero ya usafiri ni kumuamuru RTO kuweka askari kufuatilia madreva wanaoenda kinyume na route zao na kuchukuliwa hatua za kisheria.
Mkuu naona kama majibu ya kero zenu unayo unataka kumsumbuwa tu mkuu wa mkoa. Yaani umekata tiketi na kulipa nauli ya kwenda Luchelele halafu konda na dreva wake wawili tu wanawashusha wati 16 amabo ni abiria halali kwenye HAICE na nyinyi mnakubali kushuka - halafu unaiita hiyo KERO! KIZAZI GANI HIKI?
 
Acha kukurupuka mkuu,ulishaona wapi mtu anakata tiketi kwenye daladala kwa nauli ya tsh 400?Malalamiko yake ni sahihi hata huko ulipo hao watu wawili wana nguvu kuliko abiria mia

Mkuu shs 400 haina tiketi?
 
Nianze kwa kukupongeza kuweza kuteuliwa kuwa mkuu wa mkoa wetu. Kwa niaba ya wakazi wa Luchelele wilaya ya Nyamagana nawasilisha kero zetu zinazotusibu kwa muda mrefu.

Kwanza, ubovu wa barabara. Barabara yetu ni mbovu sana,ina mashimo na makorongo huwezi kuamini kuwa hii barabara ipo sehemu ya jiji. Pamoja na ubovu huo unaosababisha magari kupita kwa shida pia kuna kero ya vumbi. Kuna msururu wa malori yanayokuja kuchukua udongo wa moramu ambapo wanashindwa hata kumwagilia maji.

Pili, usafiri. Kuna shida sana ya usafiri kwa sisi wakazi Luchelele inayopelekea matumizi makubwa ya pesa kwa kupanda bodaboda. Sasa 12 jioni ikikukuta mjini hesabu maumivu. Zile Hiace za Luchelele zinabadili route na nyingine zinaishia Malimbe - SAUT na wanawatangazia abiria pale stendi ya Igombe bila kuogopa, panakuwepo hakuna askari pale ya kufuatilia hizi hujuma.

Vilevile, zile hiace za route ya Luchelele- Usagara haziendi tena kule,zimeajianzishia route ya Luchelele- Kona ya Nyegezi kwa siku nzima na nauli wanatoza ile ile, cha kushangaza hakuna polisi wanaowachukulia hatua wakati wanageuzia barabara kuu na wenyewe wakiona na ikifika saa 12 jioni wanapeleka abiria mjini na kurudi Buhongwa.

Tatu,huduma ya maji na afya. Kuna mgao mkubwa sana wa maji na sehemu nyingine mabomba yapo kama mapambo,maji hayatoki kabisa,mabomba yanaharibika na hayatengenezwi kwa wakati. Kuhusu afya, kata nzima hakuna kituo cha afya.

Kwa machache ni hayo tu, mengine nipende kukukaribisha uje ujionee mwenyewe.

Kwa msisitizo zaidi ni kwamba masuala mawili ya mwanzo yapo ndani ya uwezo wako kabisa ni suala la kutoa amri tu kwa mfano kwenye suala la ubovu wa barabara ni kama TARURA hawana fedha za matengenezo basi ni kuwaambia wenye kampuni iyochimba moramu huku kuhakikisha wanaziba hayo mashimo maana ndo waharibifu wakubwa wa barabara na miundombinu ya maji.

Hiyo moramu wanaipitisha tu bila kutengeneza wanapoharibu. Pia kwenye suala la kero ya usafiri ni kumuamuru RTO kuweka askari kufuatilia madreva wanaoenda kinyume na route zao na kuchukuliwa hatua za kisheria.
Mkuu w mkoa wenu keshawaambia pigeni ulabu kwanza😃😃😃
 
Back
Top Bottom