Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

Ndugu zangu mimi nilikuwepo ndani ya kivuko kile cha MV NYERERE,tumepona tu kwa sababu tulikuwa nje,waliokaa ndani ni ngumu sana kupona kwakuwa kivuko kiligeuka gafla chini juu na kina uzito,
mtu ukifunikwa vile ata waokozi wakifika ndani ya robo saa kukuta bado mzima ni ngumu sana.
Kama hauamini na unazani masihara jaribu kuzama ndani ya pipa la maji kwa dakika 10 bila kupumua uone.
Mimi naomba wale waliozidisha abiria na uzito wakamatwe kama Mhe Rais alivyosema
na sisi abiria tujiongeze
Tukifika standi kwenye basi ama bandarini tuwe tunauliza, je hiki kivuko kina beba watu wangapi ?
na huo uzito ubandikwe kwenye mbao za matangazo,ukiona watu wamezidi usipande ila wa afrika sisi tunalazimisha na wengine tunatoa rushwa ili turuhusiwe kupanda madhara ndio haya,
ni ngumu sana kupona ukifunikwa vile ata kama baada ya dakika 10 kivuko kinge ondolewa majini lazima maiti zingekuwa nyingi sana,
watu waangalie ata Marekani boat ili wahi kuzama kwa kugeuka tu watu 17 wakaaga dunia,,waokozi wanafika wakakuta tayari na wenzetu wameendelea sana lakini kifo cha maji kinaua haraka hasa kama mtu unakuwa umefunikwa kama hawa walikuwa ndani.

Hiki kivuko kime karabatiwa mwaka jana na kote huko kimeenda vizuri tu tunakaribia kupaki watu wa ndani wanagombea kutoka nje

kwa kuwa watu walizidishwa uzito ukaenda sehemu moja kikageuka wajuu tukarushwa kwenye maji ndio pona yetu, wavuvi jirani wakaja kutuokoa,,walipoingia ndani ya kivuko kwa chini mda ule ule wakakuta watu washakufa kwa kukosa hewa sasa watu wasilaumu tu bila kujua.
nawaambia usiombe kufunikwa na kivuko, Sikia tu kwenye mitandao.......

mimi John Kisekwa..."
Mbona kama hatiririki kama mhusika!? Kuna kitu
 
Alivyojipaka oil alizuia metabolism mkuu. Ameziba matundu ya vinyweleo mwilini hivyo kufanya mambo ya metabolism yaende taratibu sana mkuu. Pia imekuwa kama insulator dhidi ya maji maana mwili ungeanza kumenyeka kama magome ya mti.
Kama alishtuka akaenda kujifungia mle kwenye chumba chao yaani alikuwa ameshakosa pumzi ya kuongea akawa anagonga gonga kwa ndani hadi waokoaji wakamsikia
 
Hiyo kazi ngumu sana...

Inasemekana meli inapopataza tatizo na hatimae kuzama wanatakiwa wawe watu wa mwisho kabisa kutoka kwenye meli...


Cc: mahondaw
 
Ni tukio la kusikitisha sana hili.Kifo cha maji ni cha kuogofya sana.Hasa kufa kabisa ukijiona.Mungu azilaze Roho za Marehemu mahala pema peponi na Manusura namwomba Mungu wetu mwema abariki kila watakachofanyiwa cha kuwaponya na hatimaye warudi katika hali zao za kawaida.
 
Alivyojipaka oil alizuia metabolism mkuu. Ameziba matundu ya vinyweleo mwilini hivyo kufanya mambo ya metabolism yaende taratibu sana mkuu. Pia imekuwa kama insulator dhidi ya maji maana mwili ungeanza kumenyeka kama magome ya mti.
Unafahamu maana ya metabolism?
 
Alivyojipaka oil alizuia metabolism mkuu. Ameziba matundu ya vinyweleo mwilini hivyo kufanya mambo ya metabolism yaende taratibu sana mkuu. Pia imekuwa kama insulator dhidi ya maji maana mwili ungeanza kumenyeka kama magome ya mti.
Unafahamu maana ya metabolism?
 
Dak mbili tu kwa mtu wa kawaida hazimalizi ndani ya maji sembuse masaa 24? mnashangaza sana. Hata kama waokoaji wangepeleka kwa chop maafa bado yangekuwa yaleyale tu maana chombo kilipinduka suddenly na kufunika watuna dakika 10hata daiva mzoefu hamalizi nani ya maji lazima afariki maana hatumii gills kupumua, lawama nyingine za kipuuzi kabisa.
Je huyu fundi mkuu aliyekaa saa 48 vipi? Usicheze na MUNGU mkuu
 
Mongela you need to be proactive.
Ungeanza kujipanga mapema na mahema. Majenereta. Bulbu.fedha kidogo na chakula kwa waokoaji. Huyu aliyeokolewa hai leo angetoka na wengine wengi wasio na hatia.
Mongela alifika eneo na tukio na smart phone minus washauri wake na hakua na mkakati wowote zaidi ya kupigwa picha.
Sasa mtu kama huyo ukmwita ndo kawatoa kafara utakataaa??
Mita 50 kutoka nchi kavu, watu wanateketea kisa giza? How comes. Huyu ni kupiga risasi hadharani!
 
Engine room kuna watertight doors na bulkhead ambazo haziruhusu maji kuingia. Na kuwa na oil mwili mzima hii huenda imetokana na chombo kupinduka so oil imemwagika tu hovyo
 
Back
Top Bottom