Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila asimamia ubomoaji wa nyumba ya Mwananchi

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,797
11,959
Mkuu wa mkoa wa Mbeya Albert Chalamila, amesimamia zoezi la kubomoa nyumba ya Atony Lyuba mkazi wa Kata ya Inyala, Halmshauri ya Wilaya ya Mbeya, baada ya kukaidi agizo la kubomoa kwa hiari nyumba yake.

CHALAMILA%20WEB.jpg

Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila.

Uamuzi wa RC Chalamila, ulitokana na Lyuba kukaidi agizo la kupisha mradi wa ujenzi wa barabara yenye urefu wa kilomita 16.7, ambao unajegwa kwa kiwango cha lami kuanzia Inyala hadi eneo la Simambwe, ambapo viongozi mbalimbali wa serikali walifika kumtaka avunje nyumba yake kwa hiari lakini aligoma.

"Nimeamua nije mwenyewe kubomoa nyumba yako, maana kila wakati tulikuomba kwa hiari yako lakini uligoma, haiwezakani wenzako wote wakubali kubomoa halafu wewe peke yao ugome kama ni Imani za kishirikinabasi tutaziona", amesema Chalamila.

Mkandarasi wa mradi huo, Imelda Ngailo, amesema kuwa kugoma kubomoa kwa nyumba hiyo kumechelewesha kuendelea na shughuli kwa sababu ya nyumba yake kuwa katikati ya hifadhi ya barabara na kwamba mradi huo ulitakiwa ukamilike Desemba mwaka huu lakini utachelewa kutokana na kikwazo hicho.

Akizungumza na EATV kuhusu suala ya kukaidi kubomoa nyumba yake, Antony Lyuba, alikanusha madai ya yeye kugoma kubomoa nyumba na kwamba hakuna kiongozi yeyote alimfuata kumpa maelekezo.

"Hakuna Mwenyekiti wa Kijiji wala Kata aliyekuja kwangu kuniambia nibomoe nyumba, zaidi ya kufika ofisini kwako mkuu wa mkoa na nikaamuriwa kuwa niko chini ya ulinzi kwa kukaidi agizo la kubomoa kwa hiari nyumba yangu," amesema Lyuba.

Chanzo: IPP Media
 
Hahaha ujinga huo hata mimi nisingeufanya, nijenge mimi halafu nibomoe mimi ili nisilipwe?!

Magufuli aliwaambia wananchi wa Kagera kwamba walibomoa nyumba zao baada ya tetemeko na hawalipwi.

Kwanini abomoe, na je mlimlipa fidia?!

Huo ni uhuni huo mmemfanyia.
 
Ma RC someni kisa cha Mwamwindi.Acheni hizi tabia.Mtu akigoma anapelekwa mahakamani na mahakama inatoa amri.

Tumeona DC alivyoshiriki kubomoa miundo mbinu ya umwagilaiaji kwa Mbowe.

Mkuchika anza tena kufunda watu wako!!!
 
Mkuu wa mkoa wa Mbeya Albert Chalamila, amesimamia zoezi la kubomoa nyumba ya Atony Lyuba mkazi wa Kata ya Inyala, Halmshauri ya wilaya ya Mbeya, baada ya kukaidi agizo la kubomoa kwa hiari nyumba yake.
CHALAMILA%20WEB.jpg

Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila.

Uamuzi wa RC Chalamila, ulitokana na Lyuba kukaidi agizo la kupisha mradi wa ujenzi wa barabara yenye urefu wa kilomita 16.7, ambao unajegwa kwa kiwango cha lami kuanzia Inyala hadi eneo la Simambwe, ambapo viongozi mbalimbali wa serikali walifika kumtaka avunje nyumba yake kwa hiari lakini aligoma.

"Nimeamua nije mwenyewe kubomoa nyumba yako, maana kila wakati tulikuomba kwa hiari yako lakini uligoma, haiwezakani wenzako wote wakubali kubomoa halafu wewe peke yao ugome kama ni Imani za kishirikinabasi tutaziona", amesema Chalamila.

Mkandarasi wa mradi huo, Imelda Ngailo, amesema kuwa kugoma kubomoa kwa nyumba hiyo kumechelewesha kuendelea na shughuli kwa sababu ya nyumba yake kuwa katikati ya hifadhi ya barabara na kwamba mradi huo ulitakiwa ukamilike Desemba mwaka huu lakini utachelewa kutokana na kikwazo hicho.

Akizungumza na EATV kuhusu suala ya kukaidi kubomoa nyumba yake, Antony Lyuba, alikanusha madai ya yeye kugoma kubomoa nyumba na kwamba hakuna kiongozi yeyote alimfuata kumpa maelekezo.

"Hakuna Mwenyekiti wa Kijiji wala Kata aliyekuja kwangu kuniambia nibomoe nyumba, zaidi ya kufika ofisini kwako mkuu wa mkoa na nikaamuriwa kuwa niko chini ya ulinzi kwa kukaidi agizo la kubomoa kwa hiari nyumba yangu," amesema Lyuba.

Chanzo: IPP Media

Uitaka nini kama vigezo na masharti
 
Back
Top Bottom