Mkuu wa mkoa wa Kagera unatia aibu

wembeee

JF-Expert Member
Jan 16, 2015
2,708
1,353
Mkuu wa mkoa wa Kagera, John Mongella ameagiza wakuu wa shule zilizofanya vibaya kwenye mtihani wa taifa wa darasa la saba na kidato cha nne waweke vinyago milangoni mwao ili kila
wanapoingia waone udhaifu wao.

Je, unadhani hii itasaidia kunyanyua kiwango cha elimu?
 
Mkuu wa mkoa wa Kagera, John Mongella ameagiza wakuu wa shule zilizofanya vibaya kwenye mtihani wa taifa wa darasa la saba na kidato cha nne waweke vinyago milangoni mwao ili kila
wanapoingia waone udhaifu wao.

Je, unadhani hii itasaidia kunyanyua kiwango cha elimu?

Hiyo ni mbinu ya kizamani sana aliitumia mkoloni sasa nashangaa hat wakati wa digitali bado inapendekezwa...shame on u RC.
 
Mlichapwa viboko (Kagera), kunyimwa likizo (Simiyu) & sasa kuwekewa vinyago mlangoni (Kagera); Walimu wa Tanzania bhana...
 
Kati ya wakuu wa mikoa mizigo Tanzania hili limoja wapo,yaani hamna kitu kabisa na UCCM umemzidia hadi majukumu yake ya kazi anashindwa kuyatekeleza. Litoto la mama lilikuwa limezuia na sherehe kabisa yaani ................... ukibebwa bebeka sasa hili limeshindwa hadi kujibeba. Jamani Masawe lilikuwa jembe.
 
Hizi nafasi za kupeana zinaleta kero sana. Hakuna taaluma inayotumika kuteua mtu zaidi ya kujuana na matokeo yake ndio haya.
 
Anatapatapa ili aonekane anachapa kazi. Ama kweli ule usemi wa piga mkia uone kichwa kilipo awamu hii unatimia kiulaini. Kudos "mzee wa hapa kazi tu".
 
Tuwe wabunifu kuliko kuwa wadhalilishaji,ukipata shule ya kwanza lazima na ya mwisho iwepo,kufanya vizuri kunategemea lojistikia na stratejia mahali shule ilipo.Shule zingine walimu hawatoshi mzigo unakuwa mkubwa,mtu anaona bora liende tu,hasa mazingira magumu ya vijijini.
 
Back
Top Bottom