Mkuu wa mkoa wa Iringa una taarifa kuwa wachuuzi wa nyanya kule Mgama wanawataka wakulima wawauzie tenga moja 4,000/?

Elice Elly

JF-Expert Member
Dec 9, 2018
1,268
1,593
Mh. Rc Tafadhali tunakuomba achana kwanza kuwa mtetezi wa wabunge waliofukuzwa uanachama huko Chadema, badala Yake Shughulikia kwanza tatizo la bei ya nyanya kule Mgama.

Kilimo cha nyanya ni kilimo kigumu sana kinachohitaji uangalizi wa karibu sana,sasa watu wamehudumia nyanya na sasa wamefikia msimu wa kuvuna cha ajabu tenga linalouzwa 40,000/ msimu wa mavuno walanguzi wanataka kununua kwa 4,000/.

Wakulima wanaumia sababu hawana mtu wa kuwatetea katika hili sababu Mbunge wao (Mgimwa) wa CCM hawajamuona tangu wamuone wakati wa kampeni, na mbaya zaidi wanaugulia tu wanapoona mtetezi wao Mkuu wa mkoa upo busy kuwatetea wabunge wa Chadema waliovuliwa uanachama wakati wao wapo jirani na ofisi YAKO lakini hawaoni jitihada zozote za kuwatetea.

Wanaomba huo ukarimu ulio nao uanzie kwanza nyumbani sababu nyanya zao zinaozea shambani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi wewe unajua kuporomoka kwa bidhaa?
Wakinunua 100,000 hilo Tenga watauzia wapi?

Hebu lima nawe ujue mchezo ulivyo.

Mpunga hapa geita gunia hupanda hadi 80,000 ila sasa gunia lile lile ni 35,000-25,000

Kama vipi watunze hadi bei ipande
 
Huko Iringa si niliona kuna mwaka nyanya zilikuwa nyingi hadi ng'ombe wakawa wanalishwa nyanya.
kwenye uchumi kuna theori inasema " the higher the supply the lower the price" kwamba bidhaa ikiwa nyingi kwenye soko bei yake nayo inashuka
 
Back
Top Bottom