Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Hapi afichua siri ya Peter Msigwa kujiunga CHADEMA: Adai ana mikakati ya kumrudisha CCM kupitia Kampeni ya Iringa mpya.

Na wao wana mawivu kibao tu mzee but nilikuwa nikiongelea incidence iliyotokea mkoani Iringa 2015 hasa kwenye majimbo yaliyokuwa hot ya Iringa Mjini na Kilolo.
Naamini wazee wa iringa waliompa hata uchifu wamemuelezea namna ya kuishi na wana Iringa. Wanapenda heshima sana tena , ila akileta ujanja ujanja Iringa sio mahala rahisi sana.
 
View attachment 852236

Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Hapi, akiwa kwenye studio ya Mwananchi jana, jijini Dar es Salaam, amefichua siri ya Mbunge wa Iringa Mjini Mchungaji Peter Msigwa kujiunga Upinzani kuwa, ilitokana na udhaifu ulioonyeshwa na Watendaji ndani ya Halmashauri na kupata ajenda kwa sababu ya udhaifu wa CCM (ya kipindi hicho).
Hata hivyo, Hapi alielezea juu ya Kampeni yake mpya inayolenga kuboresha sekta ya utumishi wa umma, kilimo, utalii, misitu na afya. Hapi alisema kuwa, hana sababu ya kugombana na Msigwa bali anapaswa aone mwenyewe kwamba Mkuu wa Mkoa amekuja kufanya kazi ili wananchi wawe na imani na Rais wao na Serikali yao, hadi Msigwa aseme: "Jamani sasa huku niliko nafanya nini?"
Hapi alieleza kuwa, Ilani ya Uchaguzi inayotekelezwa sasa ni ya CCM na hata Msigwa anatekeleza Ilani hiyo.
"Nina imani kwa kazi ninazofanya wala sitakuwa na sababu ya kumshawishi Msigwa arudi CCM. Nina imani kabisa mwenyewe nafsi inamsuta na ataona hana namna nyingine isipokuwa kujiunga CCM."

View attachment 852275

View attachment 852238

Kwa vyovyote iwavyo ujio mkoani Iringa wa dogo huyo utamsumbua sana Msigwa come 2020. Nakumbuka mwaka 2015, Mwakalebela wa CCM, alikuwa hot sana kiasi kuwa, wengi walijua Msigwa atapigwa chali basi tu. Na kwa kipindi kile, kulikuwepo msuguano mkubwa sana Mjini Itinga baada ya kuwa watu maarufu walishindwa kufurukuta kwenye kura za maoni za CCM, wakiwemo: Augustine Maiga, Abbas Kandoro (marehemu), Jeca Msambatavangu na wengine. Sasa, Msambatavangu aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama (M) aliposhindwa alikuwa na kinyongo na kumsaidia kisirisiri Peter Msigwa ili ashinde. Kumbuka Msambatavangu alikuwa mtu wa Lowassa na kwa kuwa Lowassa alihamia Upinzani, it seemed as if no one cared that much in Urban Iringa, mpaka baadaye Kampeni kali ya kutumia fedha ilipoubadilisha kabisa Mji wa Iringa kuwa kama umechukuliwa na Mwakalebela. Ndiyo maana Mwakalebela hakuamini kushindwa kwenye Uchaguzi ule na kukataa kusaini matokeo mpaka baadaye ilipomlazimu baada ya hali kuwa worse Mjini Iringa.
So, niki-recall ile situation ya 2015, halafu uweke ujio wa Hapi, wazee kiukweli Msigwa atapata tabu sana mbele ya yule (pichani) jamaa mbobezi wa IR.
Hata hivyo, shida ya Wagombea ubunge wa kinyalukolo wa CCM kipindi kile tangu kwenye Kura za Maoni, ni kuwa walikuwa wakiombeana mabaya dhidi yao wenyewe hasa kwa wale waliokuwa Mawaziri kwani walihofia wenzao kuwa anaweza kuchukua nafasi ya uwaziri ambayo ingeangukia Mkoa wa Iringa. Nadhani wivu huu uko katika kila Mkoa ila huwezi ukaugundua kirahisi, so na wenyewe umesaidia kwa kiwango fulani kuwasaidia Wapinzani. I'm sure you know what am talking about, right?
Unashabikia kabisa..hiyo ndiyo kazi ya RC??

Sent using Nokia Torch 2108
 
Kimsingi wakuu wa mikoa na wilaya ni kama hawana kazi ya kufanya yaani hawana JD japo zimewekwa kwenye sheria mama yaani Katiba na au wameamua kuziweka pembeni na kuamua kutekeleza yasiyokuwepo!
Kuhusu Iringa asahau kabisa kwenda kwa staili ya kumnunua msigwa kwani hatoweza na hauziki kwa bei ndogo ya waitara et al! Msigwa is there to lead wanyalukolo wenzake na siyo kujiuza!
Hebu kama amekosa kazi akaombe vinyungu kule kitwilu au itamba na mawelewele akalime mchicha kwani unalipa!
 
Kazi ya kuwarejesha watu kutoka upinzani kuingia chama tawala ndiyo iliyompeleka huko au ndiyo majukumu ya Mkuu wa Mkoa? Kazi ya mwenyekiti wa CCM mkoa na wenzake mpaka wale wa matawi ni nini sasa?

Yeye ajikite kwenye hayo mengine aliyoyataja ya uboreshaji afya, elimu utalii, usalama wa raia nk bado ataonenekana ni bora kuliko kujiingiza kwenye majukumu mengine kana kwamba ndiyo aliyetumwa vipi pamoja na juhudi hizo bado msigwa akabaki upinzani itakuwaje au ndiyo atatumia njia mbadala ili atimize azma yake?

Mkuu wa mkoa jikite katika kufanya kazi zako za msingi bado wana Iringa watakukumbuka mentality ya kuvuna wapinzani achana nayo haitakusaidia mwishowe utajiingiza kwenye migogoro isiyo na maana Rais kakuamini usimuangushe
Viongozi wa serikali ya awamu hii ni wa hovyo sana mkuu toka kuumbwa kwa ulimwengu huu
 
View attachment 852236

Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Hapi, akiwa kwenye studio ya Mwananchi jana, jijini Dar es Salaam, amefichua siri ya Mbunge wa Iringa Mjini Mchungaji Peter Msigwa kujiunga Upinzani kuwa, ilitokana na udhaifu ulioonyeshwa na Watendaji ndani ya Halmashauri na kupata ajenda kwa sababu ya udhaifu wa CCM (ya kipindi hicho).
Hata hivyo, Hapi alielezea juu ya Kampeni yake mpya inayolenga kuboresha sekta ya utumishi wa umma, kilimo, utalii, misitu na afya. Hapi alisema kuwa, hana sababu ya kugombana na Msigwa bali anapaswa aone mwenyewe kwamba Mkuu wa Mkoa amekuja kufanya kazi ili wananchi wawe na imani na Rais wao na Serikali yao, hadi Msigwa aseme: "Jamani sasa huku niliko nafanya nini?"
Hapi alieleza kuwa, Ilani ya Uchaguzi inayotekelezwa sasa ni ya CCM na hata Msigwa anatekeleza Ilani hiyo.
"Nina imani kwa kazi ninazofanya wala sitakuwa na sababu ya kumshawishi Msigwa arudi CCM. Nina imani kabisa mwenyewe nafsi inamsuta na ataona hana namna nyingine isipokuwa kujiunga CCM."

View attachment 852275

View attachment 852238

Kwa vyovyote iwavyo ujio mkoani Iringa wa dogo huyo utamsumbua sana Msigwa come 2020. Nakumbuka mwaka 2015, Mwakalebela wa CCM, alikuwa hot sana kiasi kuwa, wengi walijua Msigwa atapigwa chali basi tu. Na kwa kipindi kile, kulikuwepo msuguano mkubwa sana Mjini Itinga baada ya kuwa watu maarufu walishindwa kufurukuta kwenye kura za maoni za CCM, wakiwemo: Augustine Maiga, Abbas Kandoro (marehemu), Jeca Msambatavangu na wengine. Sasa, Msambatavangu aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama (M) aliposhindwa alikuwa na kinyongo na kumsaidia kisirisiri Peter Msigwa ili ashinde. Kumbuka Msambatavangu alikuwa mtu wa Lowassa na kwa kuwa Lowassa alihamia Upinzani, it seemed as if no one cared that much in Urban Iringa, mpaka baadaye Kampeni kali ya kutumia fedha ilipoubadilisha kabisa Mji wa Iringa kuwa kama umechukuliwa na Mwakalebela. Ndiyo maana Mwakalebela hakuamini kushindwa kwenye Uchaguzi ule na kukataa kusaini matokeo mpaka baadaye ilipomlazimu baada ya hali kuwa worse Mjini Iringa.
So, niki-recall ile situation ya 2015, halafu uweke ujio wa Hapi, wazee kiukweli Msigwa atapata tabu sana mbele ya yule (pichani) jamaa mbobezi wa IR.
Hata hivyo, shida ya Wagombea ubunge wa kinyalukolo wa CCM kipindi kile tangu kwenye Kura za Maoni, ni kuwa walikuwa wakiombeana mabaya dhidi yao wenyewe hasa kwa wale waliokuwa Mawaziri kwani walihofia wenzao kuwa anaweza kuchukua nafasi ya uwaziri ambayo ingeangukia Mkoa wa Iringa. Nadhani wivu huu uko katika kila Mkoa ila huwezi ukaugundua kirahisi, so na wenyewe umesaidia kwa kiwango fulani kuwasaidia Wapinzani. I'm sure you know what am talking about, right?
Yataenda Mungu alivyopanga. Akili yako na mapenzi yako ni vyako tu siyo vya kijamii

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Inasikitisha kwa mkuu wa mkoa miongoni mwa vipaumbele vyake viwe ni KUUA UPINZANI, kana kwamba upinzani ni adui kwa mustakabali wa maisha ya wananchi! Cha ajabu majority ya watu wetu wanafurahia move kama hii iliyojaa ujinga, husuda, roho mbaya na ubinafsi. Hapa cha kujifunza ni kuwa CCM wapo kama walivyo kulinda madaraka yao, just imagine kiongozi kama RC badala ya kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sheria ya bunge yeye anamuwaza Mhe Msigwa kumpeleka kwenye chama kilichochokwa cha ccm. Wakati huo huo tunatarajia kupata maendeleo. Maendeleo gani hayo, never ever, tutaendelea kupiga mark time hivi hivi hadi hapo tutakapojitanbua kama taifa.
CCM licha ya kuwa na uongozi kila mkoa, mkuu wa mkoa naye anajivika kazi za ccm za propaganda chafu dhidi ya vyama vya upinzani.
Kuna matatizo kadhaa miongoni mwa jamii yetu yanayofanya tusipige hatua stahiki ya maendeleo kama yalivyoainishwa na Mwl Nyerere kuwa ni ujinga, umaskini na maradhi, ccm ya leo imeongeza na UPINZANI kuwa adui wa maendeleo.
Sad!
 
Badala ya hoja za maendeleo, yeye anawaza nonsense

Sent using Mikoyan MiG-29
 
Back
Top Bottom