Mkuu wa mkoa wa Geita Apata ajali

WABHEJASANA

JF-Expert Member
Jun 22, 2011
4,225
869
Wakuu wa JF:

Taarifa za uhakika nilizozipata usiku huu zinasemea Mkuu wa Mkoa wa Geita Said Magalula Said amepata ajali katika eneo la Kijiji cha Buhalahala nje kidogo ya mji wa Geita baada ya gari lake kuwaparamia Ng'ombe aliokua akivuka Barabara kutoka malishoni.

Hata hivyo hakuna mtu aliyepoteza maisha kwenye ajali hiyo wala kujeruhiwa vibaya isipokuwa majeraha na maumivu ya kawaida tu,lakini gari lake limeharibika vibaya sana na sehemu ya mbele ya Gari,alikuwa akitokea jijini mwanza na amepata ajali majira ya aa moja na nusu usiku huu.
 
Ni kada wa ccm geita, nch hii hakuna wakuu wa mikoa bali ni makada wa mikoa, kwa kuwa hajaumia simpi pole
 
amfidie mwenye ng'ombe walioumia sio kutoa pole tu!
Mmh, hivi sheria ya barabarani inasemaje? Ng'ombe si ndiyo aliingia barabarani? Hapo nafikiri mwenye ng'ombe ndiyo anabanwa na si aliyegonga ngómbe.
 
Kuna ng'ombe aliyepoteza maisha?..,... Pole yangu iwafikie ng'ombe wote waliokutwa na mkasa huo!
 
Kuna ng'ombe aliyepoteza maisha?..,... Pole yangu iwafikie ng'ombe wote waliokutwa na mkasa huo!

Dah!!!!!!!!!!1hata kama,iweni na moyo wa huruma huyu ni binadamu mwenzio,mbona kwa sharo pole zilikuwa nyiingi,au ka sababu yeye alipotea kabisa?!
 
Watu kwa kweli mmepinda kama Mizengo P!!

Yaani wakuu mnahurumia ng'ombe kuliko binadamu? Ila kwa Msukuma atakuwa ameulizia kwanza ng'ombe wake hao waliogongwa kama wazima, ndo baadaye aulizie na wale binadamu kwenye gari!
 
nol no ulikua usingizi tu Mpwa hata Kaka Mkuu hua anakosea Pia au umesahau Kiranja Mkuu wa Bunge alipomwita Muhseshimiwa Supika, Mheshimiwa Waziri Mkuu.........

Kwani wewe hujawahi?!
 
Back
Top Bottom