Mkuu wa mkoa wa geita amfukuza afisa elimu sekondari wilaya ya bukombe kwenye semina ya sensa. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkuu wa mkoa wa geita amfukuza afisa elimu sekondari wilaya ya bukombe kwenye semina ya sensa.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by NG'OMBE, Jul 16, 2012.

 1. NG'OMBE

  NG'OMBE JF-Expert Member

  #1
  Jul 16, 2012
  Joined: Mar 26, 2011
  Messages: 362
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Wakuu habari nilizozipata hivi punde kutoka Geita leo mida ya mchana mkuu wa mkoa huo alimfukuza Afisa elimu Taaluma wilaya ya Bukombe kutoka katika semina ya sensa iliyoanza leo mjini humo. Chanzo cha habari kinasema kuna walimu aliwateua kuhuzulia semina hiyo, lakini juzi (jumamosi) akawaeleza kuwa zoezi limeahilishwa lakini baadhi ya walimu wakazipata kuwa majina yao yamechakachuliwa na kupewa watu wasiostahili. Ndipo mmoja wa walimu hao akaamua kwenda eneo la tukio (jina kapuni) leo alishangaa kuwaona maafisa mbalimbali kutoka Bukombe wakija kwenye tukio wakiwa pamoja na wake zao, masecretaries na watu wengi tu wasiostahili kulingana na maelekezo ya ofisi ya takwimu. Serikali imeagiza watakaohusika na zoezi hili ni walimu na wawe chini ya miaka 45 na wachapa kazi.
  Mwalimu huyu alijikuta ana barua tofauti na wote ndipo alizuiwa kuingia kwenye semina. Kuona hivyo alikwenda kumuona mkuu wa mkoa naye akatoa amri ya kuondolewa Afisa elimu huyo na mwalimu kuchukua nafasi yake, hii ni baada ya kukiri kuwa anaitambua barua hiyo na kwa nini alimdanganya mwalimu kuwa zoezi limeahilishwa na wakati si kweli.
  Sasa matumbo moto maafisa wote wa wilaya ya Bukombe wanajiuliza nini kitafuata baada ya hapo. Mtoa taarifa amedokeza kuwa ni kweli watu waliohuzulia semina hiyo toka Bukombe wengi wao si walimu. Miongoni mwao ni wakuu wa idara mbalimbali na ni wazee sana pamoja na wake zao.
  MY TAKE: Zoezi muhimu kama hili linaanza mizengwe mwanzoni tu, hofu yangu huenda tukapata takwimu za kupikwa tu na watu wakagawana pesa za walipa kodi.
  Naomba kuwasilisha.
  source: Mwalimu aliyeko kwenye semina.
   
 2. tatanyengo

  tatanyengo JF-Expert Member

  #2
  Jul 16, 2012
  Joined: Mar 30, 2011
  Messages: 1,140
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Ahsante sana Ng'ombe. Kila jambo linachukuliwa kama ulaji. Baadhi ya viongozi wanatumia madaraka yao vibaya. Tafadhali ndugu zanguni sie viongozi tusome alama za nyakati, vinginevyo tutakukwa tunaumbuka kila kukicha.
   
Loading...