Mkuu wa mkoa wa Dar unania njema ya kukomesha madawa ya kulevya lakini njia unayotumia sio sahihi.

lukoma

JF-Expert Member
Jul 1, 2013
2,995
2,245
Sikutegemea kumsikia kiongozi akisema kuwa nikotayari kupoteza ukuu wa mkoa, niko tayari hata kutangulia mbele za haki baada ya hapo akaanza kuwataja waajiliwa wake/wafanyakazi wake!!! Hii inamaana gani, ushujaa au anawaogopa hata wafanyakazi wake?. Kwenye uongozi na utawala tutaiitaje aina hii ya uongozi?

Tumepata pia kusikia mkuu wa mkoa akisema Dar yangu, watu wangu, wananchi wangu, yangu, yangu, yangu, wa kwangu, mimi ndiye bingwa wa vita, na mengineyo. Iweje leo muajiriwa wako, tena bado yuko kazini unamtangaza kwenye vyombo vya habari kuwa ndiye anayeshiriki katika madawa ya kulevya kama tuhuma badala ya kuchua hatua?

Napata shida kupata picha ya usahihi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa kuanza kuhoji washukiwa wa madawa ya kulevya! taaluma hiyo anayo? Kweli atawahoji au atawalazimisha wakubali? Je, askari hawa pia wataingia kwa mkuu wa mkoa kuhojiwa?

Hivi inawezatokea Rais kwa nafasi yake kuwaita watuhumiwa wa jambo fulani kuwahoji Ofisini kwake?

Miaka ile magazeti yangetusaidia kudadavua suala hili, lakini miaka hii magazeti yote yamebaki tu yanasimulia tu tukio!!!
 
lukoma sio lazima uanzishe thread ili uonekane.Unataka kumfundisha kazi Makonda,wewe na yeye nani ana nyenzo za kuwajua na kuwakamata wanaojihusisha na unga?Usiku mmoja tu amegundua mpaka aliekuwa RPC wa kinondoni yumo!
Makonda anatakiwa aungwe mkono badala ya kumkatisha tamaa na kebehei.
Halafu wala hujatoa maoni kama ingekuwa wewe ungefanyaje kazi kuwakatisha tamaa wanaothubutu
 
Aende akachukue list ya mapapa ya biashara ya Madawa ya Kulevya ipo Ikulu aliicha JK.

Drug smugglers wale wenyewe wengine ni washkaji zake..

Asilete utani kwenye serious issues.
 
angesema yupo tayari kupoteza maisha kupambana na yaliyosababisha shule sita dar kuburuzwa mkia !!!hiyo timing ni kudistruct attention tuu!!!
 
Back
Top Bottom