Mdg wangu na x Makongo mwenzangu Carol pole sana. Nikupe ushauri kiungwana kabisa. Unapenda siasa na hasa uanaharakati ambao si rafiki sana na serikali hasa watawala.
Hufanyi vibaya ni haki yako ya msingi na pengine ndio wito uliopewa na Mungu kusemea wengine. Lakini kwa nchi zetu hizi maskini na aina ya watawala wetu huwezi kufanya biashara zako kwa amani hata kama ni halali kwa kiwango kipi huku maneno, maandiko yako si rafiki kabisa kwa watawala.
Inawezekana hujamtukana Makonda wala kufanya ubaya wowote lakini umejijengea sura isiyo rafiki na watawala akiwemo huyo Makonda. Usidanganywe dunia hii sijui haki, usawa n.k hasa huku Africa kuna gharama lazima ulipe pale unapochagua namna ya kuishi na watawala/wanasiasa.
Wewe kujiondoa ACT na kutojiingiza kwenye siasa si "toba" kwao maana hata akina Maria Sarungi wanasema hawana vyama lakini mkondo wa maoni yao upo wazi sana na pengine wapo tayari kulipa gharama yake na ndivyo inavyopaswa ukiamua kusimamia jambo.
Wafanyabiashara wakubwa na walipa kodi wazito waki finance upande wa pili wanafinywa na kutiwa "adabu" kidogo itakuwa wewe!!! Kwani hujui kwanini CMG wanapata kibali kirahisi? Kwani umezaliwa juzi Carol hadi ushangae? Huoni wanavyounga mkono juhudi?
Dunia haiko hivyo utachanganyikiwa mdg wangu! Jifunze namna ya kuishi na watawala ili kulinda mkate wako au ingia kwenye harakati upambanie wananchi ukiwa tayari pia kwa matokeo yake na utapata heshima kubwa tu vizazi na vizazi!
Usitake kula huku na huku, harakati kidogo na biashara kidogo kwasababu tu ni haki yako, si Africa mdg wangu utakosa kote! Unafikiri Mengi amepenya vipi tawala zote? Hukujifunza hata manguli kama Rostam kuacha siasa enzi za JK na kuacha kabisa hata kuchangia/kutoa comment kuhusu siasa zetu ili alinde maslahi yake?
Asikudanganye binadamu yoyote jifunze kuwa mroma ukiwa roma full stop kama unataka usiumie kama ilivyo sasa. Kaa chini ujitafakari unataka uelekeo upi wa maisha yako then move on. Africa yenye uhuru wa kiwango hicho si ya leo wala kesho, jipambanue na pambana kwa kukubaliana na matokeo pia.
Hii ndio Afrika na wala si Tanzania tu au awamu hii tu au CCM tu! Hata kama wangeshinda Chadema lazima ujue namna ya kuishi nao kama unapenda kuendelea na biashara zako smoothly.
Ushauri wako, pamoja na kwamba unaweza kumsaidia yeye binafsi (japo kuna uwezekano mkubwa tu sio mawazo mapya kwake au umemfunza jambo asilojua) hauna msaada wowote kwa mtu yeyote pro progress. Huwezi kukubali kuwepo na upindishwaji wa haki kwenye hili au yanayofanana na hili tangu vizazi halafu ushauri wako uwe kuchagua moja kati ya haki yake ya maoni au biashara. Progress itatoka wapi akifuata njia ya Rostam na Mengi?
Tunakubali kuwa jamii isiyoprogress na hatuna jinsi bali tuwaachie watoto wetu mifumo iliyo zao la mapungufu ya wazazi wetu?
My guess is she knows what she's doing japo kuna wanaomuona naive humu. Habari za biashara zilizofail baada ya wamiliki wao kuonyesha misimamo fulani si mpya. Kuna tabia ya viongozi kudismiss malalamiko ya watu kwa kusema "alete ushahidi taratibu za ufanyaji kazi wa serikali zinajulikana". Kama Rostam na wenzake hawakulalamika basi hayatokei.
If for no other reason let this serve to crystallise these occurrences