Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda awaapisha Wajumbe wa Mabaraza ya Ardhi

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,796
11,959
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, amewataka wajumbe wa mabaraza ya Ardhi kuwa makini na watu watakaokuwa wanawasimamia, katika kutatua migogoro na kuleta usuluhishi kwa kuwa mkoa huo, umejaa watu wajanja na wanaojifanya kujua kila kitu.

Hayo ameyabainisha leo Novemba 23, 2019, mara baada ya kuwaapisha wajumbe wa mabaraza ya ardhi ndani ya mkoa huo.

"Mkawe sehemu ya suluhisho na msaada kwa wale akina Mama wajane na kwa watu ambao hawakupata fursa ya elimu, Mkoa huu ni mkoa wa wajanja, matapeli wamejaa hapa na ni mkoa ambao kila mtu ni mjuaji, msipokwenda kutumia busara na hekima mkategemea tu yale yameandikwa kwenye karatasi watu wengi wataumia" amesema Makonda.

Aidha Makonda amewataka wajumbe wa mabaraza ya Ardhi ndani ya mkoa wake, kuhakikisha wanaimaliza migogoro na kutatua changamoto zote za masuala ya Ardhi kwa wananchi na kwamba hategemei kuwaona watu wamejazana kwa Mkuu wa mkoa ama kwa Waziri wa Ardhi na ikiwezekana watoke kuwatafuta watu na kutatua matatizo yao na si kujifungia ofisini

Walioapishwa ni;

KINONDONI

1.Balozi Selestine Christopher Liundi

2. Marina Paul Mulunde

3. Derick Murusuri
*Petro Mukani (hakutokea)

TEMEKE


1. Ignnasia Benedict Makota

2. Sikunjema Yahaya Shaban

3. Fatma Abdalla Chikwido
4. Rutami Chisumo
IMG_20191123_112543_6.jpeg

 
Hii ni hatua muhimu, mabaraza haya ni muhimu sana.
Hongera mwana fani Dereck Murusuri
P
Sijui kama itakuwa hivyo unavyofikiri
Ngoja uone watu watakavyodhulumiwa na huyo huyo mteua
Njia nyingine ya kujilimbikizia mali kwa dhuluma
This guy is a disaster hana jema hata moja.
 
Eti "watu wajanja wanaojifanya wanajua kila kitu"

Kwani ni uongo kua unavyeti feki?
 
Sasa mkiacha kununua ndege Canada mkaenda kununua Brazil na Jamaa akienda kupeleka hukumu yake pale by follow law enforcement procedure mtamlaumu na Neymar maana ni Kwa court Order?

Jinsi tunavyoendesha nchi zetu hapa African ni tofauti na ulaya
Yaani hapo tumedhihirisha kuwa hatuheshimu mihimili yetu mtu mmoja anaweza kucontrol sehemu zote sababu tu mwenye kasema

Hapana haviendi hivyo ndugu zangu
 
Mbona hawa watawala hawataki kuuona ukweli na kuutatua??

Hakuna njia nyingine bali, dawa ya deni ni kulilipa........

Wasidhani kuwa yule mkulima wa South Africa ni kama wale wakazi wanyonge wa Kimara-Mbezi, ambao mmewavunjia nyumba zao, wakati kesi yao bado ipo mahakamani.

Kule Canada ni kwingine ambako, sheria ni msumeno, unakata pande zote, siyo kama TZ petu ambako sheria ina macho, ambapo inaangalia aliyefanya ni nani??
 
Mikataba mlivunja wenyewe kwa mabavu yenu Lawama muwaangushie wengine hii imekaaje?.Kauli ya Makonda kuna Mtu inamlenga ,wakati Makosa mmefanya wenyewe Serikali.Hebu lipeni Deni la Watu ,Viongozi mnalinajisi Taifa kwa kulitia Hasara kwa Sababu ya maamuzi yenu yasio zingatia Sheria.
 
Back
Top Bottom