mshumbue-soi
JF-Expert Member
- Aug 28, 2013
- 1,842
- 1,148
Nikiwa mkazi wa Dar Ambaye wewe ni kiongozi wangu.
Mambo ambayo yanakuandama mpaka sasa nimesikia ni kumsingizia Askofu Gwajima kuhusu madawa ya kulevya imeonekana umemsingizia kwa kuwa vipimo vya mkemia mkuu vimeonyesha hajatumia na hata kufunguliwa Kesi waendesha mashtaka wakasema upelelezi haujakamilika bado hilo limeshindikana.
Katika hili kwa kuwa binadamu tunasaidiana kushauriana bado una nafasi ya kuujuza umma ulikosea kumtuhumu na kumuomba radhi na wote ambao hamna hata ushahidi wa vipimo unaweza eleza hata waliokupotosha kuwa ni watumiaji.
Askofu Gwajima ametaka tuu uwambie umma kuwa si mtumiaji na kumwomba radhi bado Mimi naona ni njia bora ya kuondokana na tuhuma hii.
Pili ni kuwa vyeti vyako matokeo sio mazuri ni division zero na pia umetumia jina ambalo sio lako jambo hili tumejuzwa sana na kuaminishwa na ikizingatiwa ulikuwa mastari wa mbele kumuunga mkono Mhe Rais zoezi la vyeti vyeki ambapo wengi ilionekana wanapata mshahara ambao hauwastahili na uwezo wao ni vyeki.
Nikusihi utujuze Ukweli wa jambo hili kama yule kiongozi aliyelalamikiwa Mhe Rais akaimaliza kwa yeye kuonyesha vyeti hata Kenya viongozi wa Umma akiwemo Mayor wa Nairobi ameonyesha vyeti vyake huku akijua anacheti vyeti mpaka umma ulipotambua ana cheti vyeki hakupuuza sauti ya wengi kuwaondoa mashaka kutokana na elimu.
Nami nimewaza hili ni njia gani unaweza kutusaidia jinsi tumeaminishwa we ni zero na umetumia majina ya wengine kuendelea kielimu nikakuta una nafasi kueleza umma Ukweli hebu nikusihi jipange uujuze umma kuhusu elimu yako ya kidato cha NNE mbona mwanzoni umma ulikuwa ukisema lolote ulikuwa unajitokeza kwa ujasiri na kusema ukweli.
Kiongozi usisubiri usemewe na mamlaka ya vyeti au yeyote ni jambo dogo maana ulisoma wewe na unajua ulivukaje ngazi zote za elimu ulizopitia.
Sio vibaya kujibu hili au kuulizwa kuhusu vyeti kati mambo ya kuhoji kwa human resource ni Taaluma maana licha ya kipawa na kipaji MTU alicho nacho ktk kuongoza elimu ni ya muhimu kumuongezea maarifa ya kutumia vyema kipaji na kipawa alicho nacho haaa ktk kuwaongoza binadamu wengine.
Sijakusikia ukizungumzia elimu yako niliwasikiliza wazazi walipohojiwa na kituo kimoja cha Television ila sakata hili lilipoibuka walisema we ni MTU mzima unaweza kusema waandishi wakashindwa kutupa taarifa.
Tunajua una majukumu mengi we tuandiekie hata taarifa kwa umma kuhusu tuhuma hii tutaisoma na kupata upande wako ambao utatusaidia ktk yale tuliyo nayo kichwani.
Kimya chako cha muda mrefu kinaniacha ktk mawazo najiuliza huyu ni yule mkuu wangu wa Mkoa niliyemjua aliyekuwa anaenda na kasi ya 4G kujibu maswali ya wananchi na kuumbua uuongo unaotaka kuchukua nafasi?
Uvamizi wa kituo mpaka sasa changamoto hii njia ya kutatua ni kuomba radhi kukaa kimya wakati imebainika ni kweli yule anayeonekana ni mkuu wa Mkoa ni ngumu kuamini hili hukuhusika kuvamia kituo hichi jambo hili halijapata sikia upande wako kuhusu hili tukio.
Tunakuomba kwa kuwa waliovamia waliujuza umma nini kilitokea siku ile nawe hebu tujuze umma nini ulichotenda siku hiyo kiongozi wetu.
Inawezekana kuna mhalifu ulikuwa umeenda kumkamata au ulipata taarifa za kiitelejinsia
Kuna issue ya magari unayomiliki Mimi nashauri utujuze Ukweli maana jumejuzwa hukuyanunua na watu wamejenga hoja kidato chako
Tuhuma ya bunge umechukua hatua na tunajuzwa umeomba radhi kwa taarifa zisizo rasmi.
Kwa kuwa tuhuma hii umeanza kuishugulikia na tumekuona Dodoma hizi nyingine tunakuombea nazo uzishughulikie kwa wewe kusema.
Mimi bado naamini uwezo wako wa kukabiliana na changamoto ni mkubwa na hasa hizi za kusema Ukweli ambao umeuishi na unaufahamu.
Nimekaaa kimya cha muda mrefu ila kila nikiwaza jinsi ulivyo na uwezo wa kuwa kiongozi mbeleni Waziri wa Mambo ya Ndani au Serikali za Mitaa Tamisemi na badaye Waziri Mkuu au hata Rais wa nchi yetu kutokana na uwezo wako.
Najiuliza itawezekanaje kwa kimya cha vyeti?
Na tuhuma zingine ikikumbukwa zinasemwa na watu ambao wanaheshima katika nchi ambao hawategemewi kumsingizia mtu au kiongozi tena mbele ya vyombo vya habari.
Mwisho nikuombe urudishe imani kwa Rais na viongozi wote wa serikali na dini na sisi wananchi wa kawaida kuhusu elimu yako, tuhuma kwa Askofu Gwajima na wengine Watanzania ukiwaambia Ukweli hata kama ni mchungu wanaelewa na wanaangalia unapoweza kufiti.
Sasa wanakusubiri useme lolote waseme vyeti kwanza.
Wana jukwa tuhuma zinazomkabili kiongozi WETU ukivaa uhusika wake unamshauri nini afanye kuzitatua ili aendelee vyema na majukumu ya kututumikia.
Ushauri wako ulenge ktk tuhuma za vyeti unamshauri nini?
Kumtuhumu Askofu na wengine unamshauri nini?
Kuvamia clauds
Mali anazomiliki.
Inawezekana hatujapata majibu ya kuondokana na tuhuma dhidi ya kiongozi wetu kwa kuwa hatujamshauri afanye nini kuzitatua bali tumekuwa tukizijadili hebu tuanze kumshauri kama kiongozi wetu au mdogo WETU au kaka yetu au ndugu yetu aliyekutana na tuhuma naamini waliotuhumiwa tumewapa ushauri, waliovamiwa hebu tumshauri kiongozi WETU sasa imetosha kusema bila kumshauri afanyaje?
Tukikumbuka haijawahi sema nimechukua fomu mwenyewe nimegombea mwenyewe
Ni kiongozi WETU ingawa ameteuliwa amekuwa akifanya mambo kama kila mmoja kamchagua na akithamini umma kana kwamba umemchagua kuwaaongoza.